ZINGATIA HAYA UNAPOTAKA KUSAJILI KAMPUNI
1. Jina.
Unapotafuta jina jitahidi jina liwe linatamkika kirahisi ili isikusumbue katika marketing lakini kikubwa ni maana ya jina. Kuna maneno mengine ni matusi kwa lugha nyingine, hivyo jitahidi sana kufanya utafiti wa kina wa jina hilo.
2. Mtaji:
Maamuzi ya mtaji kiasi gani kiandikishwe ni ni jambo la msingi sana. Wengi hupenda kuweka mtaji mdogo ili kupunguza gharama za usajili na kodi, vema, lakini hicho kisiwe kigezo mama cha kukuamulia mtaji uwe kiasi gani. Tambua kwamba mtaji unawakilisha ukomo wa kuwajibika kwa kampuni katika wajibu wake.
3. Wanahisa:
Wanahisa mnatakiwa kuwa watu mnaofahamiana vema, wenye mrengo unaofanana na mnaelewana. Tofauti na hilo itasababisha kuchelewa kwa maamuzi muda wote na kuhatarisha ustawi wa biashara.
4. Uandishi wa katiba:
Ni hatari kutegemea mtu yeyote asiye na utaalam wala ujuzi wa kuandika katiba akuandikie. Kibaya zaidi wengine huandika wao wenyewe hata kama hana utaalam na uzoefu huo. Hata kwa wanasheria, si kila mwanasheria anaweza kukuandikia katiba iliyo standard.
Kitu kibaya zaidi watu hudhani kwamba unaweza kuchukua katiba yoyote na kubadili majina tu kisha ukaendelea na usajili. Hawaangalii mpangilio wa maneno na malengo, hawazingatii kama katiba ina vipengele vya kuruhusu mambo Fulani Fulani kufanyiwa mabadiliko,
Hawazingatii ni namna gani founders wanalindwa na katiba, na mengine mengi. Hivyo unashauriwa kuwatumia wataalam wenye uzoefu kufanya kazi hiyo.
Kwa huduma za uhakika na weledi katika masuala hayo yote, waone essence consult company limited.
Pia tunatoa usaidizi katika kusajili NGO, Huduma za kihasibu, kuandika michanganuo ya biashara, na usaidizi kwa wale wanaotaka kuanzisha taasisi za mikopo n.k Wasiliana nasi kwa namba 0768597186 au email
doricelucas21@gmail.com