Jinsi ya Kusajili kampuni katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mkuu in mtaji kiasi gani angarau unafaa kuanzisha Microcredit company
 
Habari mkuu Singo na wataalum wengine ninaomba kufahamu business arrangement nzuri kama ninataka kuanzisha kiwanda kidogo cha product 1 mkoa A na kiwanda kidogo kingine cha product 2 mkoa B.

Lakini pia ninataka kuanzisha Sales stores mkoa C, mkoa D na mkoa E. Hizi sales stores ninataja ziuze product zangu na related products za manufacturers wengine.

Je ni business arrangement gani inaweza kuleta ufanisi in terms of management, revenue,cost control, profitability na tax liability.
•Sole propieter or limited company?
•One business entity or a number of entities?

Ninatanguliza shukran
 
Itafaa usajili Limited company ambayo ita ainisha shghuli zote za company.Hapo utakuwa na Uhuru wa kufanya biashara popote,Ila utatakiwa kuwa na leseni ya biashara na branch TIN kwa kila mkoa utakokuwa na hayo maduka au huduma.

Sole proprietorship haitafaa kwa sababu eneo la ilipo biashara huandikwa kwenye Extract from registrar ambayo hutolewa pamoja na Certificate of registration,hivyo hutoweza kutumia hiyo business name kupatia leseni za biashara mikoa tofauti tofauti.

Ila limited company inaweza miliki majina ya biashara zaidi ya moja ambazo zinafanyika maeneo tofauti tofauti na biashara tofauti tofauti.
 
Wana JF naomba mwenye taarifa za taratibu za kusajili kampuni ya madini pale nyumbani Tanzania anisaidie.

Natanguliza shukrani zangu.

-------------------------------------








Gharama halisi n Tsh ngap ..?
 
Gharama halisi n Tsh ngap ..?
Mtaji wa mil 1 ni 177,200
Mtaji zaidi ya mil 1- 5 ni 267,200
Mtaji zaidi ya mil 5 - 20 ni 357,200
Mtaji zaidi ya mil 20- 50 ni 387,200
Mtaji zaidi ya mil 50 ni 532,200
NB hizo ni gharama za usajili wa limited company ynye mtaji na shares na zinajumuisha registration fee,filling fee na stampduty
 
ahsante mkuu
Hv mtaji ukiongezeka itabidi ulakafanye tena usajiri..?
Utawajulisha kwa kutumia special resolution ,kisha utafanyiwa assessment na kulipia kadri ya assessment itakavyokuwa.

Memorandum haibadiliki ukiongeza mtaji.

Baada ya kuongeza mtaji majibu ya kwamba mtaji umeongezeka yatapatikana kwa kuomba barua ya official search.
 
Mkuu nimechasajili jina na limekuwa approves. Nafanyaje ili nipate certificate ya kuonyesha jina limesajiliwa.
 
wadau naombeni mwenye uelewa wa taratibu zakufata ili nifanye new registration ya kampuni .asanteni
 
Habar wana jamii forum,naomba kwa yeyote anaejua nifanyaje ili nijisajili nafanya biashara ya kukopesha pesa ingawa sina mtaji Mkubwa sana

Sent from my TECNO-Y3 using JamiiForums mobile app
 
Kwanza,nenda wizara ya viwanda na biashara na shilingi laki sita tu utapat leseni
 
Nimeelewa maana ya neno Limited
 
Habari wapendwa, ninaomba kwa mtu anayefanamu au anayeweza nisaidia kusajiri kampuni anielekeze tafadhali, nahitaji kufungua kampuni ya software ila sijajua utaratibu wa kusajiri ukoje, please mwenye mawazo mazuri tusaidiane.
 
1.Hapo ni kumuona Mwanasheria akuandalie Memarts(Memorandum and articles of association)...halafu gharama za usajili Brela zitategemea mtaji(capital) wa kampuni ni kiasi gani, pia kuna gharama za filing fees, stamp duty..gharama zote za Brela utajua baada ya kufanyiwa assessment na unalipia..na ku-file nyaraka zako.

Zikiwa successful basi kampuni itasajiliwa na tapewa hati ya usajili na utaweza kuanza kuendesha kampuni. Hii ni baada ya kujaza fomu za uadilifu(integrity) na kuweka muhuri wa kampuni yako kwenye fomu hiyo.

Hatua zote nilizoeleza hapo zinatanguliwa na stage ya name clearence..hatua hii imelenga kupata jina la kampuni na kuangalia kama halifanani na majina mengine yaliyokwisha sajiliwa. Nayo hufanyika Brela, physicaly au online.

2. Baada ya Brela unaenda TRA kwa ajili ya kuipatia kampuni utambulisho wa kulipa kodi ambako directors nao watahitajika kupata utambulisho wa kulipa Kodi...baada ya makadirio na kulipa utapewa Tax clearence ambayo itakuwezesha kupata Leseni ya biashara katika halmashauri uliyopo.

3. Kama biashara yako itahitaji leseni/compliance certificates za mamlaka nyinginezo za usimamizi basi utahitajika kufika huko na kupata leseni zao eg TCRA, OSHA,

4. Baada ya hapo basi utakuwa umekamilisha taratibu za usajili wa kampuni na post incorporation requirements. Kampuni litaanza kazi.

5. End.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…