Kusajili jina la biashara sio kupata leseni halmashauri... Ukishapata certificate of Reg, nenda halmashauri na Tin yako ujipatie leseni hardcopy.. Brela huendi.
Kuhusu hoja ya Bujibuji, nadhani sio dhambi endapo kunatokea watu wenye weledi, muda na uzoefu ktk mchakato huu wakajinafasi kuwasaidia wasioweza mchakato huu kwa namna moja au nyingine. Ukiona elimu aliyotoa mtoa post imekufaa na unaweza mwenyewe Go ahead.. Ila maisha ni kugawana vijikazi. Huwezi fanya hiyo wape watu wakusaidie najua malipo kidogo yapo.. Maana hiyo pia ni kazi.. Sio kila mtu anajua, na huo mchakato hauna sura ya mtu kukutapeli, madam ujue unadeal Vipi.
Kuhusu NIDA, serikali wameamua kutumia vitambulisho hivi maana taarifa za kila mtu zinakuwa easily verified by authorities.. Ukigusa mfumo wowote online kwa no ya id hiyo taarifa zako zinaonekana, hapa wameepusha mambo mengi sana ya utapeli, uhujumu uchumi nk nk. Wananchi tukubaliane na mpango huo, nenda kajiandikishe NIDA,