Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Shikilia msimamo wako. Ikiwa unampa mtoto wako kila kitu anachotaka kwa sababu tu analipuka kwa hasira, yaelekea ataendelea kufanya hivyo kila mara anapotaka kitu fulani. Kwa utulivu mwonyeshe mtoto wako kwamba hutalegeza msimamo wako.
Elewa hali yake. Mtoto wako si mtu mzima. Kwa kuwa hajui jinsi ya kushughulika na hisia zake, anaweza kukasirika sana anapofadhaika. Jaribu kuona mambo kama yeye anavyoyaona.
Uwe mtulivu. Mtoto wako anapolipuka kwa hasira, kukasirika hakutakusaidia. Kwa kadiri inavyowezekana, puuza mlipuko wake wa hasira na udhibiti hisia zako. Kukumbuka kwa nini milipuko ya hasira hutokea kutakusaidia kuwa mtulivu.
Pia jaribu mambo yafuatayo:
Mlipuko wa hasira unapoanza mshikilie mtoto wako (ikiwa inawezekana) na, bila kumwumiza, mzuie asijigaragaze. Usimfokee mtoto wako. Subiri tu mpaka hali itulie. Hatimaye, mtoto atatambua kuwa kulipuka kwa hasira hakukumsaidia kwa njia yoyote.
Tenga mahali utakapomweka mtoto wako anapolipuka kwa hasira. Mwambie kwamba atatoka humo mara tu anapotulia, na kisha umwache humo.
Ikiwa mtoto wako analipuka kwa hasira mbele za watu, mwondoe hapo. Usimpe anachotaka eti kwa sababu tu amelipuka kwa hasira mbele za watu. Ukimpa, hilo linaweza kufanya afikiri kwamba ikiwa atalipuka kwa hasira, anaweza kupata chochote anachotaka.