Kama wewe ni mtoto wa mkulima kama mimi (huna jina kubwa na hufahamiki, ni mwananaume, huna mshiko) fanya yafuatayo:
1.Soma magazeti hasa Dailynews,the Gurdian
2.Mtandao (kuna blog zinazotangaza kazi)
3.Kama ukifanya Field, fuatilia hiyo sehemu uliyofanyia Field kwa ukaribu
4.Using'ang'anie kukaa DSM, kubali kwenda interior.....
5.Hakikisha una CV yako na application letter electronically....inapotokea kazi wewe una'edit' tu....pata ushauri toka walio senior wako jinsi ya kuandaa CV na barua ya kuomba kazi!
6.Unaweza kutafuta sehemu ya kufanya kazi kwa kujitolea na ukajitolea kufanya kazi bila kuwa na ajira ya kudumu (kama watakukubali) mpaka hapo watakapokupa ajira.
7.Funga na kuomba sana na usikate tamaa
8 Uwe nadhifu
9. Fahamiana na jichanganye na watu ili upate habari zinazohusu nafasi ya kazi yako, kazi nyingi hazitangazwi, na hata zikitangazwa tayari zina mtu.... zinatoka kwa kujuana.
10Fikiria kujiajiri pia (Usijidharau)
11...........
12...........
13...........