Jinsi ya kutengeneza hair removal wax nyumbani

Jinsi ya kutengeneza hair removal wax nyumbani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532

Chukua Kikaangio, bandika jikoni moto usiwe mkali sana, weka sukari ya kutosha.
Anza kukoroga hadi sukari ianze kuyayuka.



Ikisha yeyuka vizuri chukua asali kidogo na ndimu huku ukiendelea kukoroga hadi ichemke vizuri.




Kama ukiona mchanganyiko ni mzito sana ongeza maji kidogo huku ukiendelea kukoroga.
Ikishachemka vizuri, ipua na uache ipoe katika temperature ya kawaida kwa muda wa lisaa 1.




Ikishapoa itakua tayari kutumia, kutunza weka katika container yako kisha weka kwenye fridge.



Jinsi ya kutunza ngozi yako baada ya kuwax:

  1. Hakikisha unapaka moisturizer baada ya kufanya wax.
  2. Unaweza pia ukachukua kitamba na kukilowesha kisha kuwa kama unakanda sehemu uliyowax ili kusikakamae.
  3. Epuka kwenda juani baada tu ya ku wax, au kama inakubidi kutoka hakikisha unapaka sunscreen.
  4. Usioge kwa maji ya moto baada ya kuwax, itaondoa mafuta yako mwilini yanayofanya ngozi kuwa laini.
  5. Mahali ulipopawax pakianza kuwasha na kuwa kwekundu paka talcum powder au kanda kwa barafu.
 
wenyewe ngoja waje, mana me natumia old version!!!
 
je inaweza tumika hata kwa wanaume katika kuondoa garden love zisizo na mpango
 
Jinsi ya kuitumia ni vipi? miss zomboko
Ukishamaliza kutengeneza na ikiwa imeshapoa unapaka sehemu ambako unataka kuondoa nywele ukishamaliza kupaka utafunika au kuweka nguo au karatasi ngumu halafu utavuta kwa kinyume [namaanisha uelekeo tofauti na nywele zilivyoota].
 
Ila wax huwa inauma icho tu ndiyo kinakera
 
Doh maumivu yatavumilikaje sasa? Au tunywe chroloform? Teh teh teh
 
Nyoeni tu mavuzi na topaz au Gillette maana hiyo wax inauma balaa unaweza poteza utamu
 
Sijawah jaribu hii njia [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji12] [emoji2] ila yaonekana kutokana na maelezo si ya mchezo mchezo. Ushauri wangu kama unaona hali ni tete tafuta shaving cream nzuri hasa ya natural extracts (hasa zile ambazo hazitaleta darkening ya ngozi kutokana na kushave) kisha na gillete yako swafii (I recommend maxx 3) vuta ngozi kisha...... songa mbele
 
Back
Top Bottom