Nitajaribu kutengeneza na mie
Shostee, shukrani nyingi kwa toleo la leo ! ntajaribu kadri ya uwezo itokezee.
Shikamooo Chef
Mahitaji
Strawberries nusu kilo
Sukar robo kilo
Limau kipande.
Namna ya kutaarisha....
Osha na katakata strawberries zako
Kamua limao kwenye kibakuli....
Weka sufuria jikon bila ya kuweka maji mimina strawberries,sukati ikifuatiwa na limao
Pika moto mdogo mdogo huku unakoroga ili visigandie.....
Pika kwa nusu saa hadi jam yako iwe nzito na inaganda.
Jam tayar kwa kuliwa
Chef? Hamna chef mie napenda pika tu
Jazaakh Allah Khayraan Strawberries inapatikana wapi dar?
Hiv hujui kwamba ww ndo chef wetu!! Asante mamitoπ
Hahahaha sawa jaan tukutane uwanjani kule kushereheka timu yangu yacheza leo
Hahhahaha kila la kheir (kwa sauti ya chiini) π
Usijal ulipotoea habibty
Wallah ya bint nilikuwa safarini, atamanilik Shahar mubarak al-kareem "shahr Ramadhan al-fadhilla"
Basi nasubiri al-Futar yangu!
Shukraan futar yako ipo la tahauf
Shukraan.....subir waje watakuambia mie dar mgeni lol
Mimi shamba ni kwangu hapa Dar ninazo, nashauri watu watumie miti hii kwa ajili ya maua badala ya kutumia miti isiyo na matunda
jaan tumetoka droo ila nimenuna kidogo