Jinsi ya kutengeneza mwili bila kuingia Gym

Jinsi ya kutengeneza mwili bila kuingia Gym

Ongeza sekunde kumi (hivyo badala ya skeunde 10 zitakua 20) katika kupumzika kati ya hizo 10 na 10 zingine. Ukihama namna ya kupiga push up (mfano ulianza za kawaida unataka uhamie

Oooh
 
Fanya crunches, sit ups, na kama una roller itumie.
Kwa kua unaanza.
Sit ups, Roller na Crunches fanya seti nne, kila seti fanya mara kumi.

Yapo mazoezi mengi ya tumbo naamini kuna wadau watakutajia ila anzia na hayo ukiwa advanced tutazidi kuongeza spices.
Mkuu ungetuwekea na picha kabisa ya hayo mazoezi ingekua poa kwani huu uzi ni mzuri sana kwa sisi wapenda mazoez so ni vyema kabisa tukawa deily tuna update na kila expert akaongeza anachokijua yeye ili kila mwanamazoezi aweze jivunia uzi huu
 
Mada nzuri sana.mi huwa nafanya mazoezi kila siku asubuhi na jioni ratiba yangu kama ifuatavyo
Nakimbia uwanja x10,nafanya/kunyosha viungo kwa 15min,nafanya mazoezi ya tumbo hapa Nina mazoezi kama 6 ya tumbo(six pack),push up napiga kwa seti 3@set30.namaliza na mazoezi rejeshi
 
Wakuu plank ndio kitu gani?
plank2.jpg
 
CASTRY IKIWEZEKANA TUUNDE NA GROUP YETU YA WASAP ILI TUZIDI PEANA VITU VIZURI ZAIDI NA ITASAIDIA KUJUANA KWA WALE PENGINE TUKO ENEO MOJA TUKAWEZA JUMUIKA KWA PAMOJA NAPENDA MAZOEZI JAPO SIO EXPERT SANA NANINAKIRI YAMENISAIDIA KUPATA AJIRA AMABAYO NDIO KILA KITU KWANGU
 
Mkuu ungetuwekea na picha kabisa ya hayo mazoezi ingekua poa kwani huu uzi ni mzuri sana kwa sisi wapenda mazoez so ni vyema kabisa tukawa deily tuna update na kila expert akaongeza anachokijua yeye ili kila mwanamazoezi aweze jivunia uzi huu
Mkuu nilijaribu kutafuta muda wa kuandika uzi kabisa jinsi ya kufanya plank lakini bahati mbaya muda haujawa rafiki ila hatujachelewa sana tutafanya hivyo.
 
Hii safi sana mkuu, nilikuwa nafanya push-ups mia moja nikienda round mbili, hamsini kwa hamsini, ngoja nii-break kama maelekezo yako yalivyo.
 
Mada nzuri sana.mi huwa nafanya mazoezi kila siku asubuhi na jioni ratiba yangu kama ifuatavyo
Nakimbia uwanja x10,nafanya/kunyosha viungo kwa 15min,nafanya mazoezi ya tumbo hapa Nina mazoezi kama 6 ya tumbo(six pack),push up napiga kwa seti 3@set30.namaliza na mazoezi rejeshi
Ahsante kwa mchango wako mkuu sema tudadavulie hii namna yako ya kunyosha viungo tujifunze.
 
CASTRY IKIWEZEKANA TUUNDE NA GROUP YETU YA WASAP ILI TUZIDI PEANA VITU VIZURI ZAIDI NA ITASAIDIA KUJUANA KWA WALE PENGINE TUKO ENEO MOJA TUKAWEZA JUMUIKA KWA PAMOJA NAPENDA MAZOEZI JAPO SIO EXPERT SANA NANINAKIRI YAMENISAIDIA KUPATA AJIRA AMABAYO NDIO KILA KITU KWANGU
Mkuu hii kitu imeofa ajira kwa watu, hata gym ninayifanyia mazoezi watu wengi wapo Next Door na Casino zingine, mimi niliwahi kua kwenye peak nikawekwa kwenye parking Azura. Hongera sana.

Wazo la whatsapp litazingatiwa tutaona mwitikio wa wadau wengine.
 
jichanganye sass

Acha mkwara mkuu, hata hivyo tatizo lako ni kubwa sana. Unahitaji mtu wa karibu kukupatia elimu ya Mara kwa Mara juu ya maana, nia, na umuhimu wa mazoezi kwa maendeleo na ukuaji mzuri wa mwili wa binadamu. Hivi karibuni makamu wa Rais, (imagine, sio Mkuu wa mkoa au waziri, Makamu wa Rais) alihimiza wananchi wafanye mazoezi, tena akaenda mbali hadi kupendekeza siku.

Acha mkwara mkuu Fanya mazoezi kwa afya yako. Asante mkuu.
 
Inakuaje wadau?

Nimeanza mazoezi ya kunyanyua uzito (I hate saying vyuma) mwaka 2013. Katika mazoezi hua tunasema majukumu ndiyo mchawi wa mazoezi, hivyo majukumu ya chuo yalikua yakinifanya nisiingie gym vile ninavyotaka iwe.
Wakati mwingine unajikuta unakosa pesa ya kuingia gym hivyo unajikuta huna option zaidi ya kukaa nyumbani ukiangalia ulivyoviingiza kwa wiki sita vikipukutika.

Lakini kwa muda nimekua nikitumia njia ambayo inanifanya kuubakisha mwili kwa kuujaza na kuukata.
Best of all, hili zoezi unaweza ukafanya popote na ndani ya dakika 45 (kutegemea na unavyotaka kua challenged).

Ili kuyafikia malengo ya hapo inabidi tufanye haya mazoezi kwa kutumia mtindo unaoitwa Tabata Protocol.

Zoezi tutakalolifanya litakua ni push ups (pushapu).

Na kanuni yetu itakua;

Zoezi moja litajumuisha seti nne.
Seti moja itajumuisha reps 20.
Kupumzika kati ya seti na seti ni sekunde 10.
Kupumzika kati ya zoezi moja na jingine ni dakika moja.

Anza na Pushap za Kawaida.
Hii ni ile aina ya pushap ambayo watu wengi wameizoea. Kama alizopiga Magufuli ila wewe usikunje ngumi.
View attachment 462249
Utaanza kwa kwenda juu ukishuka chini hiyo ni moja, utafanya hivyo mara 20. Utapumzika sekunde 10 na kurudia tena mara nne.

Hapo tunakua tumemaliza zoezi moja tunaenda jingine.

Pushap za miguu ikiwa imeinuka.
Mimi hua naweka miguu kitandani, unaweza ukaiweka kwenye stuli, jiwe au hata ndoo ukiigeuza juu chini. Pale daraja la Manzese miguu hua inawekwa kwenye ngazi.
View attachment 462252
Utaanza kwa kwenda juu ukishuka chini hiyo ni moja, utafanya hivyo mara 20. Utapumzika sekunde 10 na kurudia tena mara nne.

Hapo tunakua tumemaliza zoezi la pili, tunaenda jingine.

Tunakuja na Spartan Pushap.
Mikono yako inatakiwa ipishane, mmoja uwe mbele kushinda mwingine. Lakini ukiwa unaenda juu mkono uliokua mbele utaurudisha nyuma na uliokua nyuma unaupeleka mbele.
View attachment 462253
Utaanza kwa kwenda juu ukishuka chini hiyo ni moja, utafanya hivyo mara 20. Utapumzika sekunde 10 na kurudia tena mara nne.

Hapo tunakua tumemaliza zoezi la tatu tunaenda jingine.

Tunamalizia na Pushap za Magoti kugusa Chini.
Unaweka mikono kama unataka kupiga pushap alizopiga Magufuli, ila magoti yako yatakua yamegusa chini na usikunje ngumi kama Magufuli.
View attachment 462255
Utaanza kwa kwenda juu ukishuka chini hiyo ni moja, utafanya hivyo mara 20. Utapumzika sekunde 10 na kurudia tena mara nne.

Hapo tunakua tumemaliza zoezi letu.

NB.
-Utavuja sana jasho ndani ya dakika moja
-Kama hujawahi kufanya mazoezi, usifanye spartan pushap na hii ya magoti kugusa chini kwa sasa mpaka utakapozoea. Pia punguza idadi ya seti na reps, jiongezee na muda wa kupumzika.
-Natumia uzoefu na kujifunza kwa wengine, sijasomea, ushauri wangu siyo wa kidaktari.
-Comment workout yako tupate kujifunza.
Hii IPO vizur hebu nianze
 
Back
Top Bottom