Jinsi ya kutengeneza mwili bila kuingia Gym

Jinsi ya kutengeneza mwili bila kuingia Gym

Daaaah nashindwa hata kunyanyua mkono pushup 5 kwa kila kipengele [emoji85]
 
Mkuu asante kwa Uzi mzuri, ndo nimemaliliza zoezi hapa, japo hua nafanya Mara 2 kwa wiki, j3 na alhamis

Ila Mkuu ungetoa tu ushauri kua hii no intense workout, pushup 320!! Mtu asipige kila siku maana misuli haitapata muda wa ku recover, na recovering period ndio misuli inakua,

Unless mtu anatumia supplements, kupiga hili tizi zaidi ya Mara 3 kwa wiki ni overworking, ukistress sana misuli ukuaji wake unakua taratibu sana,

Ndio maana hata gym hushauriwi kufanya mazoezi ya misuli mikubwa kama kifua au miguu kwa siku mfululizo,lazima upumzike kupisha recovery period ili misuli ikue

Misuli kama ya tumbo ni midogo na INA recover mapema ndo maana unaweza kufanya kila siku
Mkuu umetoa observation nzuri natamani ingekua juu kabisa kila mdau aione.

Ila uandishi wangu katika zoezi hili umelenga zaidi upper body, bado sijaweza kuandikia lower body. Idea yangu ni kua siku unayopumzisha upper body unakua unatrain lower body.

Na ni ukweli hii ni intense work out, siyo kwa vile ni push ups 320 ila kwa vile tunafuatisha Tabata Workout, tunafanya explosive work out inatuchoma na kutajaza pale pale huku ikituachia lasting effects, lakini pia recovery katika mtindo huu huja haraka sana.
 
Daaaah nashindwa hata kunyanyua mkono pushup 5 kwa kila kipengele [emoji85]
Kudos [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122]
Kaza hivyo hivyo mkuu.
 
Nina mitoto mitatu ya kiume nimekataa kulipia gym nikakuta imetengeneza simenti home inanyanyua...ulaji saasa hatari. Kuna njaa jamani chakula kidogo mtatufilisi
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
hivi wadau unapofanya plunk huwa unaenda chini kama push up au unaganda tu huku umeunyosha mwili,
 
Unakua umeganda huku umeunyoosha mwili
mkuu kuna push up za kupiga magoti kwenye ngazi halafu unapiga kama vile style ya magufuli ila umepiga magoti nyayo za miguu zinaangalia chini vp hizi zinasaidia nini sehemu ya mwili
 
mkuu kuna push up za kupiga magoti kwenye ngazi halafu unapiga kama vile style ya magufuli ila umepiga magoti nyayo za miguu zinaangalia chini vp hizi zinasaidia nini sehemu ya mwili
Zinatengeneza kifua, mgongo mpaka mabegani.

Mazoezi yote ya hapa yamelenga sehemu hizo, isipokua kuna mengine yatakutengenezea mstari kati ya ziwa moja na jingine
 
Inakuaje wadau?

Nimeanza mazoezi ya kunyanyua uzito (I hate saying vyuma) mwaka 2013. Katika mazoezi hua tunasema majukumu ndiyo mchawi wa mazoezi, hivyo majukumu ya chuo yalikua yakinifanya nisiingie gym vile ninavyotaka iwe.
Wakati mwingine unajikuta unakosa pesa ya kuingia gym hivyo unajikuta huna option zaidi ya kukaa nyumbani ukiangalia ulivyoviingiza kwa wiki sita vikipukutika.

Lakini kwa muda nimekua nikitumia njia ambayo inanifanya kuubakisha mwili kwa kuujaza na kuukata.
Best of all, hili zoezi unaweza ukafanya popote na ndani ya dakika 45 (kutegemea na unavyotaka kua challenged).

Ili kuyafikia malengo ya hapo inabidi tufanye haya mazoezi kwa kutumia mtindo unaoitwa Tabata Protocol.

Zoezi tutakalolifanya litakua ni push ups (pushapu).

Na kanuni yetu itakua;

Zoezi moja litajumuisha seti nne.
Seti moja itajumuisha reps 20.
Kupumzika kati ya seti na seti ni sekunde 10.
Kupumzika kati ya zoezi moja na jingine ni dakika moja.

Anza na Pushap za Kawaida.
Hii ni ile aina ya pushap ambayo watu wengi wameizoea. Kama alizopiga Magufuli ila wewe usikunje ngumi.
View attachment 462249
Utaanza kwa kwenda juu ukishuka chini hiyo ni moja, utafanya hivyo mara 20. Utapumzika sekunde 10 na kurudia tena mara nne.

Hapo tunakua tumemaliza zoezi moja tunaenda jingine.

Pushap za miguu ikiwa imeinuka.
Mimi hua naweka miguu kitandani, unaweza ukaiweka kwenye stuli, jiwe au hata ndoo ukiigeuza juu chini. Pale daraja la Manzese miguu hua inawekwa kwenye ngazi.
View attachment 462252
Utaanza kwa kwenda juu ukishuka chini hiyo ni moja, utafanya hivyo mara 20. Utapumzika sekunde 10 na kurudia tena mara nne.

Hapo tunakua tumemaliza zoezi la pili, tunaenda jingine.

Tunakuja na Spartan Pushap.
Mikono yako inatakiwa ipishane, mmoja uwe mbele kushinda mwingine. Lakini ukiwa unaenda juu mkono uliokua mbele utaurudisha nyuma na uliokua nyuma unaupeleka mbele.
View attachment 462253
Utaanza kwa kwenda juu ukishuka chini hiyo ni moja, utafanya hivyo mara 20. Utapumzika sekunde 10 na kurudia tena mara nne.

Hapo tunakua tumemaliza zoezi la tatu tunaenda jingine.

Tunamalizia na Pushap za Magoti kugusa Chini.
Unaweka mikono kama unataka kupiga pushap alizopiga Magufuli, ila magoti yako yatakua yamegusa chini na usikunje ngumi kama Magufuli.
View attachment 462255
Utaanza kwa kwenda juu ukishuka chini hiyo ni moja, utafanya hivyo mara 20. Utapumzika sekunde 10 na kurudia tena mara nne.

Hapo tunakua tumemaliza zoezi letu.

NB.
-Utavuja sana jasho ndani ya dakika moja
-Kama hujawahi kufanya mazoezi, usifanye spartan pushap na hii ya magoti kugusa chini kwa sasa mpaka utakapozoea. Pia punguza idadi ya seti na reps, jiongezee na muda wa kupumzika.
-Natumia uzoefu na kujifunza kwa wengine, sijasomea, ushauri wangu siyo wa kidaktari.
-Comment workout yako tupate kujifunza.
Mkuu,hongera sana.mm ni Mzee wa pushups sana.hata sasa hivi nipo napasha.Next time jaribu kuelimisha namna ya kuondoa kitambi bila kwenda Gym,,,! Pamoja sana
 
Mazoezi sio kuwa na mwili mkubwa tu.mazoezi ni afya na ni tiba vile ni kinga Kwa baadhi ya magonjwa.tufanye mazoezi!
 
Mkuu,hongera sana.mm ni Mzee wa pushups sana.hata sasa hivi nipo napasha.Next time jaribu kuelimisha namna ya kuondoa kitambi bila kwenda Gym,,,! Pamoja sana
Haina shida mkuu, na karibia mazoezi yote ya tumbo ninayoyajua unaweza kufanyia nyumbani.

Pasha kwa huu mfumo halafu tupe mrejesho mkuu.
 
Kwa kuongezea Mimi hua najipa Free day kwa siku 7 moja najipa free kuweka muscles zijipange kwa next day workout ...so nashauri pia si vibaya pia ukawa inajipa off ili ujione ulivyo jengeka
 
Kwa kuongezea Mimi hua najipa Free day kwa siku 7 moja najipa free kuweka muscles zijipange kwa next day workout ...so nashauri pia si vibaya pia ukawa inajipa off ili ujione ulivyo jengeka
Kabisa kabisa mkuu
 
Lakini niulize muda maalumu wa workout ni upi ukiacha Asubuhi....??
Kuna article moja ilionesha kua kufanya mazoezi jioni ni vizuri zaidi kushinda asubuhi.
Binafsi ninaweza kufanya mazoezi kabla ya kulala.
 
Ndani ya siku tatu tangu kuanza mazoez nyama za tumbo ziliuma saaaana.... Sikuweza kutembea nikiwa nimenyooka... Maumivu kila sehemu...

Kidogo niache kufanya mazoezi... Nashukuru mungu recently Niko poa kabisa napiga tizi kama kawa. Na si kutumia sawa yoyote
 
Back
Top Bottom