Jinsi ya kutengeneza mwili bila kuingia Gym

Jinsi ya kutengeneza mwili bila kuingia Gym

Mkuu nikianza kupika night baada ya kula kuna ubaya na vipi mtu ukipiga na kurusha ciku matokeo bado yatakuwa mazuri?
 
Ndani ya siku tatu tangu kuanza mazoez nyama za tumbo ziliuma saaaana.... Sikuweza kutembea nikiwa nimenyooka... Maumivu kila sehemu...

Kidogo niache kufanya mazoezi... Nashukuru mungu recently Niko poa kabisa napiga tizi kama kawa. Na si kutumia sawa yoyote
Hongera mkuu.
Hata hivyo maumivu hayo hayahitaji dawa.
 
Mkuu nikianza kupika night baada ya kula kuna ubaya na vipi mtu ukipiga na kurusha ciku matokeo bado yatakuwa mazuri?
Hakuna ubaya ni sawa, ila baada ya chakula kushuka vizuri.

Unakua umelenga kurusha siku ngapi?
 
[emoji23] [emoji23] 3] [emoji23] [emoji23] ushaanza matani au siyo?
mkuu mm kila siku huwa napiga push-ups 1000 (napiga 250 mara mbili asubuhi then jion namalizia 500 zingine). Any problem with that mkuu? Ain't that too excessive?
 
mkuu mm kila siku huwa napiga push-ups 1000 (napiga 250 mara mbili asubuhi then jion namalizia 500 zingine). Any problem with that mkuu? Ain't that too excessive?
Kama unapiga push ups za aina moja utaingia kwenye peak haraka, pia unakua unatengeneza kitu kimoja kila siku hatimaye hiko kitu hakiendi kokote ila kitaanza kuonekana kimekata mfano triceps na kifua.
Kwa ishu ya push ups baada ya kuzizoea kinachofata ni kuhisi hauko challenged kama zamani ulivyokua unaanza.

Hii routine ya hapa inalenga kutegua baadhi ya ambavyo vingekukuta ikiwa ungekua unapiga push ups za aina moja.
 
ok good, bas ntajaribu ku-improvise na aina zingine za push-ups kama walivoshauri wadau pamoja na hizo squats. push-ups za aina moja pekee zinanifanya ni-feel unchallenged kama ulivonena mkuu
 
Motivation ya kufanya mazoezi yote haya na kujitesa ni ili niendelee kujizolea maujiko mbele ya baby mama (wanawake bwana!)
 
Hakuna ubaya ni sawa, ila baada ya chakula kushuka vizuri.

Unakua umelenga kurusha siku ngapi?
Yaani ikitokea tu kama ciku labda nimechelewa au kuna ishu ya msingi nafanya

Ninamaana ya kuruka ciku moja na sio kila ciku badi ile ciku ambayo nimetingwa sana..na pia mkuu vipi labda Leo nikipiga night kesho asubhi si bado ni poa tu?
 
Inakuaje wadau?

Nimeanza mazoezi ya kunyanyua uzito (I hate saying vyuma) mwaka 2013. Katika mazoezi hua tunasema majukumu ndiyo mchawi wa mazoezi, hivyo majukumu ya chuo yalikua yakinifanya nisiingie gym vile ninavyotaka iwe.
Wakati mwingine unajikuta unakosa pesa ya kuingia gym hivyo unajikuta huna option zaidi ya kukaa nyumbani ukiangalia ulivyoviingiza kwa wiki sita vikipukutika.

Lakini kwa muda nimekua nikitumia njia ambayo inanifanya kuubakisha mwili kwa kuujaza na kuukata.
Best of all, hili zoezi unaweza ukafanya popote na ndani ya dakika 45 (kutegemea na unavyotaka kua challenged).

Ili kuyafikia malengo ya hapo inabidi tufanye haya mazoezi kwa kutumia mtindo unaoitwa Tabata Protocol.

Zoezi tutakalolifanya litakua ni push ups (pushapu).

Na kanuni yetu itakua;

Zoezi moja litajumuisha seti nne.
Seti moja itajumuisha reps 20.
Kupumzika kati ya seti na seti ni sekunde 10.
Kupumzika kati ya zoezi moja na jingine ni dakika moja.

Anza na Pushap za Kawaida.
Hii ni ile aina ya pushap ambayo watu wengi wameizoea. Kama alizopiga Magufuli ila wewe usikunje ngumi.
View attachment 462249
Utaanza kwa kwenda juu ukishuka chini hiyo ni moja, utafanya hivyo mara 20. Utapumzika sekunde 10 na kurudia tena mara nne.

Hapo tunakua tumemaliza zoezi moja tunaenda jingine.

Pushap za miguu ikiwa imeinuka.
Mimi hua naweka miguu kitandani, unaweza ukaiweka kwenye stuli, jiwe au hata ndoo ukiigeuza juu chini. Pale daraja la Manzese miguu hua inawekwa kwenye ngazi.
View attachment 462252
Utaanza kwa kwenda juu ukishuka chini hiyo ni moja, utafanya hivyo mara 20. Utapumzika sekunde 10 na kurudia tena mara nne.

Hapo tunakua tumemaliza zoezi la pili, tunaenda jingine.

Tunakuja na Spartan Pushap.
Mikono yako inatakiwa ipishane, mmoja uwe mbele kushinda mwingine. Lakini ukiwa unaenda juu mkono uliokua mbele utaurudisha nyuma na uliokua nyuma unaupeleka mbele.
View attachment 462253
Utaanza kwa kwenda juu ukishuka chini hiyo ni moja, utafanya hivyo mara 20. Utapumzika sekunde 10 na kurudia tena mara nne.

Hapo tunakua tumemaliza zoezi la tatu tunaenda jingine.

Tunamalizia na Pushap za Magoti kugusa Chini.
Unaweka mikono kama unataka kupiga pushap alizopiga Magufuli, ila magoti yako yatakua yamegusa chini na usikunje ngumi kama Magufuli.
View attachment 462255
Utaanza kwa kwenda juu ukishuka chini hiyo ni moja, utafanya hivyo mara 20. Utapumzika sekunde 10 na kurudia tena mara nne.

Hapo tunakua tumemaliza zoezi letu.

NB.
-Utavuja sana jasho ndani ya dakika moja
-Kama hujawahi kufanya mazoezi, usifanye spartan pushap na hii ya magoti kugusa chini kwa sasa mpaka utakapozoea. Pia punguza idadi ya seti na reps, jiongezee na muda wa kupumzika.
-Natumia uzoefu na kujifunza kwa wengine, sijasomea, ushauri wangu siyo wa kidaktari.
-Comment workout yako tupate kujifunza.
Hyo ni kweli mm mwenyewe ndo njia nayotumia
 
Yaani ikitokea tu kama ciku labda nimechelewa au kuna ishu ya msingi nafanya

Ninamaana ya kuruka ciku moja na sio kila ciku badi ile ciku ambayo nimetingwa sana..na pia mkuu vipi labda Leo nikipiga night kesho asubhi si bado ni poa tu?
Kufanya mazoezi kunahitaji kupumzika ili kuipa misuli muda wa kurecover. Siku ambayl unakua umetingwa ichague iwe ndiyo siku yako ya kupumzika.

Haina ubaya kufanya mazoezi usiku na kisha ukafanya asubuhi.
 
Just stumbled kwenye huu uzi najihisi kubarikiwa! By march tjis year Bye bye kitambi mchuchumio!
 
Just stumbled kwenye huu uzi najihisi kubarikiwa! By march tjis year Bye bye kitambi mchuchumio!
Hongera kwa malengo mkuu. Mpaka March utakua umepata unachotaka.
 
Mkuu naomba mazoezi ya kuipa miguu stamina na ukakamavu ,
 
Back
Top Bottom