CK Allan
JF-Expert Member
- Aug 14, 2013
- 2,781
- 6,139
UTANGULIZI
Makala hii inajikita katika kuangalia namna Bora ya kuwa na umoja na ushirikiano wa kitaifa wenye tija Bila kumuathiri mtu au kikundi chochote Cha Watu katika nchi yetu! Ingawa mara nyingi tunaambiwa hakuna mabadiliko yasiyo na maumivu hata hivyo Kwa njia hizi zikitumika ipasavyo changamoto pekee itakuwa kwenye muda, kwani itachukua miaka kadhaa kuanza kuona matokeo! Hata hivyo ni Bora kupata suluhisho la kudumu kuliko kuwa na faida za muda mfupi ambazo sio za kudumu,
UMOJA WA KITAIFA NI NINI BASI? Kunaweza kuwa na maana nyingi za umoja wa kitaifa lakini kwa Namna nilivyoona Mimi, umoja wa kitaifa ni Ile Hali ya Watu kuwa na mtazamo sawa ama kukubaliana katika mambo ambayo Yana faida Kwa nchi nzima bila kujali ni wangapi wamekubali au kukataa jambo Hilo! Mfano halisi wa umoja wa kitaifa ni pale ambapo Mfumo wa vyama vingi vya siasa uliingizwa nchini, pamoja na idadi kubwa ya watu kukataa, Bado mwalimu JK Nyerere aliona ni vyema kufanya maamuzi yenye faida Kwa nchi nzima yaani wale wengi pamoja na wale wachache! Na mfumo huo ukakubalika rasmi!
KWANINI TUWE NA UMOJA WA KITAIFA?
kama tujuavyo baada ya mfumo wa vyama vingi kuingia ndipo mawazo na malengo ya uongozi wa nchi na matarajio ya watu yakabadilika watu wakaacha kuamini katika mfumo wakaanza kuamini katika sera na watu! Na hivyo kupekelekea kutofautiana wazi wazi na hata wengine kupoteza uhai au uhuru wao wakati wa uchaguzi! Na hivi tutakubalina kuwa ni muhimu kuwa na umoja wa kitaifa ili kupunguza au kuondoa nadharia hii ya upinzani kuwa ni uadui! Sasa tuangalie namna Bora ya kuwa na umoja wa kitaifa Bila kuwa na migongano..
1. Kuwe na vipaumbele vya nchi badala ya kuwa na vipaumbe vya kiongozi anayekuwa madarakani! Ukiangalia nchi yetu hatuna vipaumbele wazi wazi wa Nini tunataka kufanya kwa miaka 10, 20, 30 au 50 ijayo! Na vipaumbele Gani vya muda mfupi vinatakiwa kuwepo! Utaona Kila kiongozi anayeingia madarakani huamua yeye ni kipi afanye kipi asifanye! Kwamfano katika nchi yetu Raisi Magufuli kwa miaka zaidi ya mitano hakuongeza mishahara Wala kupandisha madaraja watumishi wa Uma, na badala yake alipeleka Nguvu kwenye miundombinu, kujenga Madaraja, kununua ndege n.k
Na hivyo kupekelekea wafanyakazi na viongozi wengine wa vyama vya siasa kulalamika! Na tunaona pia Baada ya Raisi Samia kuingia yeye anaboresha maslahi ya wafanyakazi! Sasa nani wa kusifiwa au kulaumiwa? Jibu ni hakuna!! Hii ni kwasababu hakuna muongozo au Dira Nini kifanyike Bali ni hekima za Kiongozi aliyeko madarakani kwa kipindi husika!! Hivyo kama tunataka kuwa na umoja wa kitaifa lazima kwanza tukubaliane tunataka Nini kifanyike? Ili hata kiongozi akiwa Mimi au wewe sote tuwe na malengo sawa!
2. Kutengeneza mfumo wa viongozi kuwajibika na sio kuwajibishwa! Kwa Namna ilivyo sasa viongozi wengi wa kuteuliwa ni ngumu sana wao wenyewe kuwajibika wasipowajibishwa na viongozi wao, inatakiwa tufike mahali kiongozi anapoharibu au kushindwa kufikia malengo basi akubali kujiuzulu yeye mwenyewe, kwanini? kwasababu atakuwa amewekewa kazi za kufanya kuwe na upimaji kwa viongozi kwa kazi zao! Tofauti na ilivyo sasa kama mtu asipotenguliwa basi ndio atafanya vyovyote anavyojisikia, lakini pia anapofanya vizuri asichukue sifa yeye Bali taasisi aliyopo, na akifanya vibaya yeye awajibishwe yeye na sio taasisi!
Yaani Tusiambiwe pesa zimetolewa na Raisi Fulani.. Bali pesa zimetolewa na Serikali Fulani!
Kuwe na sheria za viongozi kuwajibika na sio kuwajibishwa!
3. Mchakato wa uchaguzi uwe sawa na wazi kwa wote! Mfumo wa kupiga kura uwe wa wazi na ikibidi kura zihesabike Kwa njia za kisasa kwa mfumo wa wazi ili kuondoa kulaumiana! Wale wanaofikia idadi Fulani ya kura basi wapate idadi Fulani ya viti na mfumo wa kutengeneza hizo kanuni uwe wazi, tofauti na Sasa ambapo baadhi ya viongozi wa uchaguzi wanapatikana kwa kuteuliwa na Raisi aliyeko madarakani! Lazima lawama ziwepo! Kidogo kwa Upande wa Zanzibar wanaweza kujivunia kwa hatua walizofikia! Na maboresho kadhaa yakifanyika basi wanaweza kuwa sawa,
4. Somo la maadili na uzalendo lifundishwe na kuwekewa mkazo shuleni! Kwasasa kumekuwa na uozo sehemu za kazi na hata waajiriwa wapya wengi ofisini akili zao za kwanza ni kwenda 'kupiga' , 'kunufaika' kupitia njia zisizo halali, pamoja na kwamba suala la maadili huanzia nyumbani lakini Kuna ulazima wanafunzi waanze kujifunza uzalendo,
Uzalendo ninaozungumzia hapa sio wa kupenda Chama au serikali! Huu ni uzalendo wa kuweka maslahi ya Taifa/nchi mbele! Ni ngumu sana kuwa na umoja wa kitaifa kwenye nchi ambayo watu wake wanaiba vyuma vya reli, wanaiba taa za barabarani, na kujisifia pindi wanapokwepa kulipa Kodi!
Ni ngumu kuwa na umoja wa kitaifa kwenye Taifa ambalo mtu anauza kura yake Kwa kupewa kofia au tisheti!
Hivyo ni lazima uzalendo uwe mioyoni mwa watu na ndipo sasa tunaweza kukaa meza Moja na kuzungumzia umoja wa kitaifa!
5. RAIA wapewe Nguvu kisheria! Wananchi wapewe Nguvu na Kila kiongozi anayeingia madarakani au kushika wadhifa basi ajue Wananchi ndio waajiri! Hapa kwetu Kuna ''marufuku' nyingi sana Kwa Raia, mara ni marufuku kukaa hapa, ni marufuku kupiga picha hapa, ni marufuku kuongea hapa n.k zipo nchi ambazo unaruhusiwa kumrekodi Polisi akiwa katika majukumu yake! Lakini Leo hii kwetu traffic akusimamishe barabarani halafu jaribu kutoa simu Yako mfukoni uone!! Duniani kote Raia Wana Nguvu sana kama wakiwa na mtazamo sawa katika Yale ambayo wanaamini! Kama Taifa tunatakiwa kuwa na heshima na uzito kwa raia wa kawaida kwasababu wao Ndio wapiga kura, wao Ndio walipa Kodi, wao Ndio wanakuja kwenye mikutano, wao Ndio wagonjwa hospitalini, wao Ndio wasafiri kwenye ndege zetu, meli n.k
HITIMISHO:
Kwa Kila namna hakuna jinsi ya kuweza kukwepa umoja wa kitaifa na amani! Umoja wa kitaifa ukiwepo basi amani nayo inakuwepo tu kwasababu Kila mmoja atakuwa ameridhika na mambo ya yanayoendelea katika nchi husika!

Upvote
2