baada ya kuona mada humu jf inayohusiana na astral projection niliipenda na nikaanza kuifuatilia google ili nipate ujuzi zaidi, katika pitapita zangu kuna sehemu niliona kuwa kusikiliza tune flani ambayo ipo kama music inaweza kukusaidia kufanikisha lengo lako kirahisi,
ili kurahisisha mambo nikatafuta application kabisa yenye beats zote hizo ili nijaribu mwenyewe , niliipata application moja inaitwa binaural beats na ipo playstore na usiku bila kulaza damu nikaanza kuijaribu, sasa kwa vile nilikuwa na mteru at first nilikuwa naishia hatua za njiani,
sasa juzi nikasema ngoja nijaribu tena kama kawaida nikafungua ile app nikaweka beat ya astral projection na nikalala chali , lengo langu lilikuwa sio kutoka nje ya mwili bali nlitaka tu nisikilize zile beats kwani nligundua vilevile zinanisaidia kupata usingizi mapema kwahio kama una matatizo ya usingizi hii ni dawa tosha niamini mimi nimejaribu kwa vitendo
ghafla nilisikia ganzi ambayo haitofautiani sana na ile tunayosemaga ni ya kukabwa na jinamizi , kwa vile nlikuwa nishajua ni nini kinaendelea , nikainuka kutoka pale nilipo na nikageuka na aisee niliuona mwili wangu, nilishtuka ila kwa vile nilijua ni nini hiki na sijafa nikajikaza, kwa kweli kutokana na woga nilichofanya nilijaribu nikapaa hadi dirishani nikaona hapana , nnachokifanya hakina maana , nikarudi kitandani nikautikisa mwili nkajikuta nimeamka,
tangu imenitokea hivo siajalala tena chali japo natumia bado beats kunisaidia kupata usingizi kwani nahisi sipo tayari kiroho wala kiakili kufanya hio kitu , kama hujaelewa hii issue kuna uzi unaohusu astral projection ni nini na ndio huo hata mimi ulinipa mwanga kwa hio sipo hapa kuelezea nimekuja kusema njia rahisi tu kwa wale onja onja wenzangu,
NB: ni lazima utumie headphones au earphones ili kupata matokeo kwani hizo beats zina frequency tofauti kati ya L and R ambayo huiwez kuisikia kama ukisikiliza kawaida