Jinsi ya kutumia mfumo wa utumishi Ess na PEPMIS

Jinsi ya kutumia mfumo wa utumishi Ess na PEPMIS

Kwani huu mfumo wanaoshindwa kuutumia ni walimu peke yake?
 
EWE MWALIMU USIIOGOPE MIFUMO BALI JIFUNZE KUITUMIA

Mwishoni Kuna link ya channel follow hiyo channel Kwa Mafunzo zaidi.

MAFUNZO MAFUPI YA MFUMO WA EMPLOYEE SELF SERVICE NA MODULI YA UPIMAJI KWA MWAJIRIWA

1.UTANGULIZI
Mfumo wa Employee Self service unamuwezesha mwajiriwa/mwajiri kupanga malengo, shabaha na kazi ndogondogo ili kufanikisha utekelezaji wa upimaji kwa muda uliopangwa na kwa uzito uliowekwa kwa Kila lengo/shabaha/shughuli ndogondogo.

2. NAMNA YA KUJISAJILI KWENYE MFUMO WA essutumishi.go.tz

A. Ingia Google.... andika
[emoji3591]essutumishi...bofya Employee Self Service Utumishi

Baada ya hapo mfumo utafunguka, Utaona boksi ya username na password chini yake Utaona

CLICK HERE TO REGISTER bofya hapo
Watumishi Portal itafunguka,

Ingiza taarifa zako KUJISAJILI, taarifa hizo ni
[emoji736]Check namba, [emoji736]NIDA namba na [emoji736]Email Yako, utarudia Tena email Yako Kisha bofya sign up,

Kama ukifanikiwa kusajili Utaona sms Registration successful

B. Kama taarifa zako ni sahihi na zipo kwenye mfumo wa HCMIS (Taarifa za kiutumishi na Mishahara ) baada ya sekunde chache utapokea ujumbe kwenye email Yako wenye check namba na password a.k.a credentials

C. Toka kwenye mfumo na uingie tena kwa kutumia check namba Yako na password/credentials ,

Mfano check namba 11116032444 na

Password /credentials QdglKR6f.

D.Baada ya hapo mfumo utahitaji uingize old Password,

Ingiza ile uliyotowa kwenye email Kisha Ingiza password mpya utakayokuwa unaitumia .

Namna ya kuunda password ukianza na neno au jina herufi ya kwanza iwe kubwa ikifuatiwa na alama mfano@#$+ n.k Kisha namba.

Mfano wa password "Karanga@6788"
Ukifanikiwa kubadili password itakujulisha kwamba Change password successful

Kisha bofya ok.

E.Kama usajili wako haujakamilika Utaona ujumbe ukikuelekeza Nini ufanye hii ni pamoja na kwenda kwa "HRO"

Afisa Utumishi ili kurekebisha taarifa zako kwenye mfumo wa HCMIS yaani Taarifa za kiutumishi na Mishahara. Baada ya hapo utaendelea utarudia hatua za KUJISAJILI na usajili wako utakamikika.

F. Baada ya kipengele 2D kukamilika Utaona moduli mbalimbali kama vile

[emoji736]My profile,
[emoji736] Salary Slip,
[emoji736]e-loan n.k

Hapo zoezi la usajili litakuwa limekwenda vizuri

G. Hatua inayofuata ni kubofya eneo la set supervisor.

Itaoneka dialogue box na utaingiza jina la mkuu wako wa shule herufi chache za mwanzo mfano RAINEL

Orodha ya majina itatokea utabofya kuingiza jina la mkuu wako ambaye ndiyo supervisor wako Kisha bofya Save.

3. Hatua inayofuata ni kwenda kwa IT wa manispaa ili akuwezeshe kuona moduli ya upimaji PEPMIS.

NB: Kuna halmashauri nyingine ma-IT wanawezesha moduli hii bila ya wewe kwenda ofisini kwao.

Moduli hii itaonekana pamoja na moduli zingine nimezitaja hapo juu kama vile My profile, Salary Slip, e-loan n.k.

4.MODULI YA UPIMAJI (PEPMIS )
Moduli ya upimaji kwa mtumishi unaitwa PUBLIC EMPLOYEE PERFORMANCE MANAGEMENT INFORMATION SYSTEM (PEPMIS)

A. Baada ya kuiona hiyo moduli ibofye, itafunguka angalia juu kushoto

Utaona nembo ya taifa na alama ya sawasawa mistari mitatu bofya hiyo alama.

Moduli ya PEPMIS itafunguka na itakuonyesha hatua zake sita. Hatua hizo ni

i. Annual Institutional performance planning

ii. Implementation and Monitoring

iii. Annual Institutional performance plan update

iv. Employee performance Assessment

v. Employee performance Assessment Referral and Appeal

vi. Report

B.NAMNA YA KUWEKA/KUANDIKA/KUJAZA TASK NA SUBTASK

i. Bofya kipengele Cha kwanza Cha PEPMIS

ii. Utaona Dashboard/Home/ Task +Create Task
No
Task
Subtask
Start date
End date
Weight
Performance indicators
Action

Utajaza hapo jedwari.

iii. Bofya+Create Task

iv. Utaona dialogue box andika lengo la kwanza na bofya save kuhifadhi.

Endelea na zoezi Hilo hadi umalize kuingiza malengo Yako yote uliyojiwekea kutekeleza kwa mwaka mzima

NB: Kumbuka kubofya save ili kuhifadhi taarifa zako.

iv. Hapo kwenye kibox Cha Action Kuna viduala viwili Kila kamoja kina vidoti vitatu hapo Kuna option za
[emoji736]+create subtask,
[emoji736]View Subtask, [emoji736]edit subtask, [emoji736]delete subtask na
[emoji736]submit subtask

Tuanze na hiii ya

[emoji3591]+Create Subtask bofya hapo kuingiza subtask kwa Kila task na save ,

Rudia zoezi kama una subtask zaidi ya Moja kwa Kila task

[emoji3591]View Subtask -inatumika kuona Subtask ulizoziweka kwa Kila task

[emoji3591]Edit subtask- inatumika kufanya mabadiliko ya subtask kama yapo

[emoji3591]Delete Subtask - hutumika kufuta subtask

[emoji3591]Submit Subtask - hutumika kutuma mpango wako wa mwaka kwa supervisor wako

[emoji3591]Note Ukitaka kufuta Task, futa Subtask ulizoziweka kwanza

'ANGALIZO'
i.kamwe usibofye eneo la submitt subtask mpka ujiiridhishe kuwa ulichokijaza/ Taarifa zako ni sahihi kwani ukisha submitt hautaweza kuona Tena ulichokifanya. Anayeweza kuona ni supervisor wako tu.

ii. Baada ya kukamilisha ujazaji wa taarifa zako na kuziwasilisha kwa supervisor wako, na supervisor akakamilisha sehemu yake sasa unaweza kuona muda wa kuanza na kumaliza task na subtask ulizoweka.

Hatua zingine za moduli utaendelea kulingana na mahitaji.

NB.
Mfumo/moduli ya PEPMIS Una alarm/alert za aina tatu kwa mwajiriwa/mwajiri

1. RANGI YA KJANI- Inakutaarifu kuwa Bado una muda wakutosha kuona malengo Yako,kuyafanyia kazi na kuyatuma kwa supervisor wako

2. RANGI YA NJANO - Inkutaarifu kuwa muda wa kuona malengo Yako na kuyafanyia kazi na kutuma kwa supervisor wako umebaki kidogo hivyo Fanya hima ushughulikie.

3. RANGI NYEKUNDU - Inakutaarifu kuwa muda wa kuona malengo Yako na kuyafanyia kazi upon ukingoni hivyo Fanya hima ushughulikie haraka

KUMBUKA MFUMO HUU WA PEPMIS WENYEWE UNATOA TAARIFA KWA KILA UNACHOKIFANYA KWA NGAZI ZOTE

Yaani ngazi ya
[emoji3591]Shule,
[emoji3591]Wilaya,
[emoji3591]mkoa na
[emoji3591]Taifa Kwa ujumla

Zingatia maelekezo unayopewa na supervisor wako ili kuleta ufanisi.
Serikali ya ajabu sana, kwa hiyo huyo mtumishi atumie mshahara wake kununua bundle kwa ajili ya haya mambo, hivi mnajua kuna watu wanakosa hata nauli ya daladala kwenda kazini bado mnawaongezea mzigo wa kununua bundle!!! Mfumo wenyewe unazunguka siku nzima mpaka watu wakajazie kwenye cyber cafe kila siku walipe Sh. 1000, did you consider this challenge?
 
Huu mfumo umefail kabla hata haujaanza. Hivi hawo walimu nani atawanunulia smartphones/iPads/laptops na kwajazia babdo ili kufanikisha hili zoezi? Nchi ngumu sana hii.

Sasa watu wa internet cafes au wajanja wamepata ulaji mwingine kutoka kwa walimu kwani sio walimu wote watakaoweza kufuata hizi complex procedures ili kujisajiri kwenye mfumo na ku create tasks pamoja na kuzijaza vizuri. Hapa lazima wajitokeze madalali wa kuwapiga hela walimu kwa ajili ya kuwajazia tasks.
Umeongea bila kufikiri. Kila mwalimu Kwa Sasa ana iPad, ndipo walipewa mwongozo wa kutumia ess, kubwa zaidi mwl. Ndiye mtu pekee ana uwezo wa kuutumia mfumo huu kwani yeye ndiye mwenye account na kila kimoja kwenye mfumo. Kubwa zaidi anazishikilia ajili za wengi. Huoni kuwa tayari umeropoka?
 
Hivi ni kweli kama mtu hujaona badiliko la cheo kwenye ESS sehemu ya designation, ni kweli kwamba inamaanisha hujabadilishiwa mshahara?Kwamba kuna uhusiano wowote kati ya ESS na badiliko la mshahara
 
Wajuzi wa mambo tusaidieni kutanzua hii sintofahamu kuhusu mahusiano ya mabadiliko ya cheo kwenye Pepmiss na badiliko la mshahara kwa mwezi huu. Hii ni kwa wale wanaostahili kupanda madaraja.
 
Hivi ni kweli kama mtu hujaona badiliko la cheo kwenye ESS sehemu ya designation, ni kweli kwamba inamaanisha hujabadilishiwa mshahara?Kwamba kuna uhusiano wowote kati ya ESS na badiliko la mshahara
Hapana.

Hivyo vyeo vinajazwa kwa mkono.
 
Back
Top Bottom