Jinsi ya kutumia mfumo wa utumishi Ess na PEPMIS

Kwani huu mfumo wanaoshindwa kuutumia ni walimu peke yake?
 
Serikali ya ajabu sana, kwa hiyo huyo mtumishi atumie mshahara wake kununua bundle kwa ajili ya haya mambo, hivi mnajua kuna watu wanakosa hata nauli ya daladala kwenda kazini bado mnawaongezea mzigo wa kununua bundle!!! Mfumo wenyewe unazunguka siku nzima mpaka watu wakajazie kwenye cyber cafe kila siku walipe Sh. 1000, did you consider this challenge?
 
Umeongea bila kufikiri. Kila mwalimu Kwa Sasa ana iPad, ndipo walipewa mwongozo wa kutumia ess, kubwa zaidi mwl. Ndiye mtu pekee ana uwezo wa kuutumia mfumo huu kwani yeye ndiye mwenye account na kila kimoja kwenye mfumo. Kubwa zaidi anazishikilia ajili za wengi. Huoni kuwa tayari umeropoka?
 
Hivi ni kweli kama mtu hujaona badiliko la cheo kwenye ESS sehemu ya designation, ni kweli kwamba inamaanisha hujabadilishiwa mshahara?Kwamba kuna uhusiano wowote kati ya ESS na badiliko la mshahara
 
Wajuzi wa mambo tusaidieni kutanzua hii sintofahamu kuhusu mahusiano ya mabadiliko ya cheo kwenye Pepmiss na badiliko la mshahara kwa mwezi huu. Hii ni kwa wale wanaostahili kupanda madaraja.
 
Hivi ni kweli kama mtu hujaona badiliko la cheo kwenye ESS sehemu ya designation, ni kweli kwamba inamaanisha hujabadilishiwa mshahara?Kwamba kuna uhusiano wowote kati ya ESS na badiliko la mshahara
Hapana.

Hivyo vyeo vinajazwa kwa mkono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…