Naona mpaka sasa hakuna mdau aliyekujibu swali lako hata mmoja, pole mkuu.
Kwa uzoefu wangu mfupi ebay unaweza kuuza, kikwazo kikubwa utakachokumbana nacho ni kwamba njia pekee ya malipo inayokubalika kule ni PAYPAL, na account za PayPal kwa Tanzania haziruhusu kupokea malipo hivyo hata ukicreate business account itakuwia vigumu kupokea malipo kutoka kwa wateja wako. Amazon sina hakika sana lakini wacha nifuatilie kidogo nitakujuza kidogo nitakachokipata. Na kuhusu kuibiwa hilo suala liko wazi lazima utalizwa mara chache, mtu atalipia mzigo utatuma kisha anarudi kuwalilia ebay kuwa hajapata mzigo wake, ebay wanaskiliza sana mteja kuliko muuzaji huyo mteja lazima atarudishiwa tu pesa yake akisisitiza kuwa hakupata mzigo, hiyo inakuwa imekula kwako,,,,lakini usiogope, hakuna bishara isiyo na hasara. Angalia bidhaa zilizo huku ambazo ni unique na zinaweza kuvutia walio nje, kuna dada mmoja Mghana huwa napiga naye story, anauza shanga za kuvaa kiunoni, shanga ya string mbili mpaka tatu anauza mpaka dola sitini...na anawateja wengi marekani na ulaya!! Sasa fikiria wewe hizi shanga za wamasai huku zinauzwa shngapi, ukipata wamama kadhaa wanaojua kudesign shanga nzuri unapata faida nzuri kisi kwamba ukipoteza mara mojamoja wala haiumi! Angalia vitu vya kiutamaduni, pia unaweza kufuatilia bei za vito vilivyochongwa vya mawe adimu kama Tanzanite kwa sonara, ukadesign na boksi zako unakuwa unahudumia maharusi wa huko mbele...eventualy brand yako inasimama wakati hujui hata kukata jiwe, mjini kulala na njaa kupenda!