Jinsi Ya Kuwa Mwekezaji Kwenye Viwanja Na Majengo Mwenye Mafanikio Mkubwa Mwaka 2022

Jinsi Ya Kuwa Mwekezaji Kwenye Viwanja Na Majengo Mwenye Mafanikio Mkubwa Mwaka 2022

Aliko Musa

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2018
Posts
209
Reaction score
315
Takwimu zinasikitisha sana linapokuja suala la wawekezaji wenye mafanikio makubwa kupitia uwekezaji kwenye viwanja na nyumba.

Si zaidi ya asilimia kumi ya wawekezaji wote waliojenga mafanikio makubwa sana kupitia uwekezaji kwenye ardhi na majengo.

Sababu kuu ya wengi kushindwa kujenga utajiri mkubwa ni kutojifunza. Haiwezekani kuwa na mafanikio kuliko uwezo wa kiakili na kimaamuzi ulionao.

Sina maana akili za kufaulu darasani, nina maana uwe na maarifa sahihi na taarifa sahihi ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo.

Kisha kutumia maarifa sahihi na taarifa sahihi ulinazo. Wengi wa wamiliki wa viwanja na nyumba huamini kuwa uwekezaji huu ni rahisi kujenga utajiri mkubwa bila hata kujishughulisha sana.

Wengi huamini kuwa unanunua, unasubiri na kuwa tajiri. Hii inaweza kuwa ndiyo au ikawa hapana.

Kama uwekezaji kwenye viwanja na nyumba ingekuwa rahisi hivyo, isingekuwa tena ni njia ya kujenga utajiri mkubwa.

Ni kweli uwekezaji huu ni moja ya sekta iliyowafanya mamilionea na mabilionea wengi kufikia uhuru wa kifedha ndani ya miaka mitatu, mitano hata kumi.

Lakini matajiri hawa walikuwa na kitu cha ziada cha kuweza kuwekeza kwa kujitofautisha na wawekezaji wengine.

Kitu ninachokushirikisha leo ni hiki hapa;

Jifunze kwa bidii.

Jifunze kuhusu uwekezaji kwenye ardhi na majengo.

Rafiki yangu, jambo la kujifunza lipo ndani ya uwezo wako. Hata kama hauna muda, unaweza kuwa na kiasi kidogo cha fedha cha kuwalipa watu ambao tayari wana maarifa sahihi na taarifa sahihi za uwekezaji huu.

Wapo wengi ambao walitumia mbinu bora kutoka kwa washauri/menta/kocha wao kiasi kwamba hawakuhitaji kutenga muda wa kujifunza.

Walitumia mbinu ambayo huelekezwa na kocha au menta wao. Kwa jinsi hii timu yote ya mwekezaji husika huwa inafanya kazi kwa kutumia mbinu ya kocha au menta ambayo inafaa kwa mwekezaji husika.

Pia, unaweza kujifunza wewe mwenyewe moja kwa moja kutoka kwenye vyanzo tofauti tofauti vya maarifa sahihi na taarifa sahihi.

Njia Za Kupata Maarifa Sahihi Na Taarifa Sahihi.

Menta/Kocha Wako.

Hii ni njia bora kabisa ya kubaki kwenye njia kuu. Michepuko inakuwa mingi kwenye safari ya kufikia mafanikio makubwa sana.

Ili ubaki njia kuu ni muhimu sana kuwa na kocha au menta au rafiki wa kukuwajibisha (accountability partner).

Haijalishi una taaluma, kipaji, na uwezo wa juu kiasi gani, kama hauna mtu huyu njia yako ya kufikia uhuru wa kifedha itakuwa ya tabu mno na utachoka sana.

Kocha ni kama mtalimbo wa kusukumia jiwe kubwa sana ambalo hamuwezi kuliinua watu kumi. Kocha atakufanya ufanikiwe mapema na kwa kutumia nguvu kidogo.

Huyu ndiye atakuwa mtu wa kulaumiwa pale unaposhindwa jambo. Kocha au menta wako atakuwa na wewe hatua kwa hatua kutoka mwanzo wa safari yako hadi kufikia uhuru wa kifedha.

Vitabu Vya Viwanja Na Nyumba.

Vitabu ni hazina nyingine ambayo hutakiwi kuikosa. Mimi nimeandika vitabu vitatu (3) vilivyoandikwa kwa lugha ya kiswahili.

Vitabu vingine vingi vya lugha ya kiingereza ninaweza kukupatia kama zawadi bure kabisa kila unapohitaji kutoka kwangu.

Mwanzoni unaweza kutumia mbinu bora za kocha au menta wako endapo hauna muda wa kutosha kujifunza wewe mwenyewe kutokana na ajira au biashara uliyonayo.

Lakini kwa baadaye utalazimika kuanza kujifunza wewe mwenyewe moja kwa moja kwa sababu utakuwa umepata kipato kinachokuongezea uhuru wako.

Semina Za Uwekezaji Kwenye Viwanja Na Nyumba.

Hizi ni zile za njia ya mitandao au semina za ana kwa ana. Semina za ana kwa ana zina nguvu zaidi kuliko semina za njia ya mtandao.

Kwenye semina za moja kwa moja unakuwa na umakini mkubwa kwenye masomo husika. Pia, unaweza kutumia lugha ya picha ya mwili kujifunza kutoka kwa mwezeshaji.

Unashauriwa uhudhurie angalau semina moja kila mwaka kuhusu uwekezaji kwenye ardhi na majengo.

Tafakari.

Njia nyingine ya kujifunza ni kusikiliza sauti yako ya ndani inavyoongea. Njia hii ni njia ngumu na njia ya kibunifu sana.

Ukiweza kuitumia vyema wengi hawatakuelewa wakati wa mchakato, lakini watakuelewa baada ya kukamilisha jambo unalofanya.

Kwa kutumia njia hii, unaweza kufanya mambo makubwa sana kama matokeo maarifa sahihi na taarifa sahihi ulizopata kupitia njia za hapo juu.

Kwa kutumia njia hii, unaiamrisha akili isiyofikiri (subconscious mind) kukupa majibu bora ya changamoto za uwekezaji kwenye viwanja na nyumba.

Kwa kupata suluhisho za chanagamoto za uwekezaji kwenye ardhi na majengo utajiweka kileleni kabisa juu ya washindani wengine.

Utakuwa mwekezaji wa kuleta suluhisho sio kuleta chanagamoto nyinginezo. Utakuwa unanunua chanagamoto, na kuuza suluhisho.

Mwaliko Wa Kuwa Mwanatimu Wako.

Naitwa Aliko Musa. Mimi ni mwandishi na mshauri mbobezi wa uwekezaji kwenye viwanja na nyumba.

Mimi nimejitoa kwa kusaidia wawekezaji kwenye viwanja na nyumba ili wajenge mafanikio makubwa.

Kwa kipindi cha miezi sita (6) utafahamu thamani halisi ya huduma ninazotoa. Kila hatua nitashirikiana na wewe ili uwekeze kwa mafanikio makubwa sana.

Kwa kipindi cha hiyo miezi sita (6) utakuwa na wanachama wengine ambao utajifunza nao kila siku kwa miezi sita (6) mfululizo.

Kwa kipindi cha miezi sita (6) utaruhusiwa kunipigia simu, kutumia ujumbe wa kuomba ushauri na kunishirikisha chochote kuhusu uwekezaji wa ardhi na majengo.

Hutajuta kunichagua mimi kuwa rafiki yako na mmoja wa wanatimu wako wa kuwekeza kwenye viwanja na nyumba.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Namba ya WhatsApp; +255 752 413 711
 
Back
Top Bottom