Jinsi ya kuzuia figo zako kuwa na mawe

Jinsi ya kuzuia figo zako kuwa na mawe

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
20210311_122752_0000.png

Kunywa maji mengi ni jambo muhimu sana katika kuzuia mawe kwenye figo. Kunywa kati ya glasi 12-14 (zaidi ya lita tatu) kila siku

Usile chumvi nyingi, chumvi nyingi katika chakula inaweza kufanya kalsiumu zaidi itoke mwilini kwa njia ya mkojo na hivyo kuongeza hatari ya mawe kutokea

Punguza vyakula kama nyama ya mbuzi, kuku, samaki, ng’ombe na hata mayai. Hivi huwa na asidi nyingi ya aina ya yurik ambayo huleta mawe

Kula mboga mboga na matunda mengi ambayo hupunguza asidi kwa ujumla na kwenye mkojo
 
Sisi wanywa bia.. hayo mawe tunayaondoa kwa masanga.. maana ni kimiminika pia
 
Kwa mujibu wa maelezo aliuoyatoa Daktari kwenye kipindi cha Meza Huru - ITV, gharama ya upandikizaji tu ni sh. 30,000,000/=.
Figo ni zako [namaanisha amezitafuta mgonjwa kutoka kwa nduguze/jamaa zake].
Duuuh!!
 
Hapo mgonjwa hana figo sasa inabidi apewe za kununua,gharama ipoje?
 
Yani nisile Mbuzi,Kuku Samaki Mayai nk.....
raha ya kuishi unaitoa wp hapo usipokula hivyo vitu!!!??
mwingine ataongezea usinywe na pombe....
 
Nilisikia dawa ya mawe kwenye figo ni kunywa maji mengi.
Ukinywa maji mengi sana mawe yanayeyuka na kupona.
Je ni kwel?

Maji mimi yalinikataa miaka zaidi ya 40 yaani ni chai, kahawa, juice basi ila maji kama maji huwa sinywi ila nadunda namshukuru Mungu
Niko tofauti kwani binadamu wote sio sawa na Kiu siijui hata liwe joto kiasi gani
Kweli wanasema kuwa uyaone [emoji1787]
 
Kwa mujibu wa maelezo aliuoyatoa Daktari kwenye kipindi cha Meza Huru - ITV, gharama ya upandikizaji tu ni sh. 30,000,000/=.
Figo ni zako [namaanisha amezitafuta mgonjwa kutoka kwa nduguze/jamaa zake].
Duuh....
 
Maji mimi yalinikataa miaka zaidi ya 40 yaani ni chai, kahawa, juice basi ila maji kama maji huwa sinywi ila nadunda namshukuru Mungu
Niko tofauti kwani binadamu wote sio sawa na Kiu siijui hata liwe joto kiasi gani
Kweli wanasema kuwa uyaone [emoji1787]
Siku hizi ukifuatilia sana maelekezo ya hawa wanaojiita WATAALAMU unaweza ukafa kwa presha na mawazo.......maana lila mtu anasema la kwake......
 
Maji unakunywa sema kwa mfumo mwingine kupitia hayo uliyosema
 
Siku hizi ukifuatilia sana maelekezo ya hawa wanaojiita WATAALAMU unaweza ukafa kwa presha na mawazo.......maana lila mtu anasema la kwake......

Yaani ni shida Mkuu
Hata kunywa maji mengi kupita kiasi ni kujitafutia matatizo tu
Ila siamini wanayosema wataalamu kwani kila mmoja ana mfumo wake mwilini
Mimi kwenye chakula lazima niongeze chumvi na kwenye chai sukari lazima
Sio mimi bali mwili ndio unataka na vingine hautaki
 
Lita tatu za maji ya Kilimanjaro ni 3000 x siku 30 jumla ni 90,000

Hapo bado king'amuzi, Kodi , Hela ya usafi , vicoba, Vocha , bado mizinga, saidia, ndugu, hujala asubuhi - usiku.

Kweli ni mitano Tena a.k.a Again
Tumia ya kuchemsha nyumbani. Unabeba container ya lita tatu kwenye begi fresh kabisa. Mimi huwa natembea na gallon ya lita tano ya maji ya kuchemsha ya nyumbani linakuwa na barafu kabisa limegandishwa.....

Nikiliacha kwenye boot mule na hili joto la Dar inayeyuka taratibu nakwenda kumimina lita moja na nusu kila mara baada ya gallon kukauka hadi yanaisha.....

Na nikitembea siwashi AC inanisaidia sana kunywa maji maana lile joto linanifanya nisweat na kutoka jasho nyingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom