Jinsi ya kuzuia tatizo la kuharisha safarini

Jinsi ya kuzuia tatizo la kuharisha safarini

Safarini tembea na kamba kavu ya magome ya mgomba. Funga kidole cha mwisho cha mguu wa kushoto.

Huwezi kujisaidia haja kubwa NG'OO hadi ufungue kamba hiyo.

TEST IT
Dah.... Au chukua njiti 2 za kiberiti...zifunge pamoja kwa Uzi wa kaniki....weka juu ya sikio.....haja size zote utazisikia kwa wengine hadi utoe njiti sikioni 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Tatizo la kuharisha safarini linatatiza sana na pia huabisha. Shida hii husababishwa na sumu zilizotengenezwa na bakteria au virusi uliowameza kwenye msosi. Ni jinsi gani ya kujizuia.

1. Usile vyakula vichafu hasa usiku kabla ya safari. Wengi wanaopata shida ya kuharisha safarini si sababu ya vyakula wanavyokula safarini, ni sababu ya vyakula walivyokula jana usiku. Kawaida sumu hizi huchukua kuanzia masaa nane kuanza kusababisha kuharisha toka mtu ale sumu hizo. Sasa unaamka vizuri, unashanga umekula tu kidogo tumbo linachafuka. Sumu ile ya jana inakuwa imeanza kufanya kazi. Vyakula hatari kwa kusababisha mambo haya ni chachandu, kachumbari na jamii ya nyama isiyoandaliwa vizuri. Unakuta mtu amsechamba, na bila hata kujisafisha vya kutosha anaenda kuandaa kachumbari au chachandu. Ni rahisi sana kupata wadudu na hizo toxins.

2. Flajili haifungi kuharisha. Ukianza kuharisha usitegemee flajili itafunga. Dawa za kufunga kuharisha zipo, moja wapo inaitwa Loperamide. Na ni vema sana hii dawa ikawekwa kwenye mabox ya huduma ya kwanza kwenye mabasi. Hii inatuliza misuli ya tumbo haraka sana hivyo inakata kuharisha fasta. Fajili ni dawa ya kuua bakteria, inachukua muda mrefu kufanya kazi. Siyo dawa ya emergency.

3. Epuka vyakula vya vinavyoweza sababisha uharishe. Kama unajijua mbovu wa vyakula fulani, basi usitumie wakati wa safari au masaa kadhaa kabla ya safari kama usiku wa safari. Kuna vyakula kama Juisi ya ukwaju. Ukwaju huwa unatabia ya kulainisha choo na kuongeza msukumo. Epuka juisi hiyo safarini.
Tumia kitunguj saumu
 
Safarini tembea na kamba kavu ya magome ya mgomba. Funga kidole cha mwisho cha mguu wa kushoto.

Huwezi kujisaidia haja kubwa NG'OO hadi ufungue kamba hiyo.

TEST IT

Ukikaa na mchawi na yeye akishika hilo gome la mgomba akilitoboa kuharisha ni dakika sifuri

Hata ww unaweza mchezea mtu mchezo ukiwa nae karibu toboa gome la mgomba chap anaenda kuharisha imeisha hiyo
 
Kama unaona viashiria vya tumbo mgogoro ysiku wa kuamkia safari kunywa LOPERAMIDE (vinauzwa elfu moja tu)..
 
dawa ya kuharisha safarini ni kuacha ulaku tu. utakuta umekaa na jibu kwenye basi kila basi likisimama ananunua chochote na anakula, hajanawa mikono na hajui vyakula hivyo vimekaa siku ngapi hadi yeye aje kuuziwa. kuna mmoja tulikuwa tunaelekea mkoa fulani ikabidi ashukie njiani akapange guest safari itaendelea kesho yake, kwasababu alishajinyea tayari na watu washaanza kulalamika harufu, tena dume zima.
 
Back
Top Bottom