Jinsi ya mzazi kumchukulia cheti cha sekondari mtoto wake aliye nje ya nchi

Jinsi ya mzazi kumchukulia cheti cha sekondari mtoto wake aliye nje ya nchi

Mimi nilishamchukulia ..... cheti chake.

Aliandika barua ya mimi kuomba kumchukulia cheti chake. Nilitoa copy vitambulisho vyangu wakanikubalia.
Ulimchukulia your my wife wako?
 
Kichwa kinauma, siwezi elezea hali halisi hapa ila mwanafunzi hawezi kukichukua mwenyewe kwa sasa.Kama kuna mtu wa wizara ya elimu jamani anisaidie nifanyeje
 
Wewe ulikuwa kama mzazi au.Nimemwambia mwalimu mkuu wa shule kama mwenyewe kupitia mwanasheria anaweza kuandika barua wanasema mwongozo unakataza.Nimejichokea na hiyo miongozo kwa kweli kwani Ada nilipe then cheti siruhusiwi
Kauli...namna unavyojieleza...mtu uliyekutana naye. Siwezi nikatoka Arusha kufuata cheti nikafika Dar ukaniambia habari za wizara.

Yes kama mzazi mlezi.
 
Jamani naomba kupata maelekezo kuna uwezekano kwa mzazi kumchukulia mtoto wako cheti chake cha form four au six kama yeye mwenyewe hayupo nchini na nina documents zote zinazoonyesha hayupo.

Cheti original kinahitajika chuoni alipo. Je, kuna uwezekano wa mzazi kukichukuwa? Na je, utaratibu upoje?

Kama nimeweza kumlipia karo miaka yote hata cheti siwezi kupewa? Jamani naomba mwenye kuelewa utaratibu anisaidie.
Tuambie MATOKEO yake Kwanza
 
Mimi wakati nasoma nchi za watu nilimtuma mtoto wa ndugu yangu.

Mwambie mwanao aandike barua kukupa ruhusa ya kuchukua cheti chake.

Ila wasiliana na shule aliyomaliza wanataratibu gani?
 
Mimi wakati nasoma nchi za watu nilimtuma mtoto wa ndugu yangu.

Mwambie mwanao aandike barua kukupa ruhusa ya kuchukua cheti chake.

Ila wasiliana na shule aliyomaliza wanataratibu gani?
Asante ngoja nijaribu hii option
 
Nimeenda ndugu ,wamenikatalia na hawatoi na wanasema hakuna alternative. Sasa nikajiuliza kama motto akinipa power of attorney bado wamesema haiwezekani.Sasa mwenye kujua unafanyaje.Mimi naming kuna alternative
Hiyo shule washamba tu. Kuna uwezekano wa mtoto wako kuandika formal letter akiomba umchukulie cheti chake. Hicho kinafanyika sana. Hao labda wanataka hongo, ongea nao vzr. Bongo ukiona mtu ana complicate jambo ujue anatengeneza mazingira ya rushwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo ni suala la busara na uelewa wa mkuu wa shule, ofisini mpo wawili tu mkuu wa shule na wewe, technolojia imekuwa siku hizi mkuu anaweza kuambia nenda na document kuonyesha wewe ni mzazi wake, pili andika barua ya kujicomir unachukua cheti tatu, kuna whatsap video call fika kwa mkuu mpigie kijana aongee na wewe live mkiwa na mkuu kisha atume video fupi akisema cheti mpatie mzazi mkuu atoe cheti

Lengo ni ushahidi siku mtahiniwa akirudi dai cheti akute hakipo hofu ya nini hapo ni kuyajenga tu mkuu wa shule na wewe
 
Jamani sema sisi tunataka mambo kirahisirahisi....
Cheti ni cha aliyefanya mtihani na kutunukiwa...hivo anayeruhusiwa kukabidhiwa ni mwenye cheti na sio mzazi ati kisa kalipa ada etc. Thamani ya cheti haipimwi na hela.
Mtoto akishachukua cheti chake ndo yupo free kumwachia mzaz wake.

Incase mzazi kachukua cheti na mtoto kaamua kumkomoa mwlm...basi mwlimu 20yrs itamuhusu.

Kuna kesi mbili mi ninazifahamu...
1. Mzazi (baba) waliparangana na mkewe...mtoto akawa anaishi na mama....baba akaamua kwenda kuchukua cheti....mtoto anafata chet akakosa...akatishia kwenda polisi..ilibd mkuu ampigie babake na kumbembeleza....ana kumweleza yeye atafungwa...baba akaachia chet...

2. Kuna baba alichukya cheti for good.
Mtoto kwenda kuchukua akakikosa...akaenda polisi mojakwamoja....wakaja wakamsweka mwlm alikaa ndan 2days...later baba akasema chet akukichukua yeye....mwlm aliachiwa na kukabidhi ofic

Sasa mwongozo uliopo ni mwanafunz ndo anakabidhiwa cheti...
Tusirahisishe mambo jamani.... 20yrs sio kitu kidogo
 
Back
Top Bottom