Mambo ya Mungu siku zote yameonekana ya kipuuzi na ya wehu, lakini ndio huwa ndio msingi mkuu wa maisha. thread inaongelea wahindi maskini. mimi nilichangia kuwa ukikutana na mtu maskini, na una uwezo kumsaidia, umpe, kwasababu ndio maagizo ya Yesu, tuwape wahitaji, huo ndo upendo, hatuwezi sisi sote tukawa matajiri, wapi matajiri na maskini, wahitaji na wenye navyo. kwahiyo, kama wewe umeamua publicly kumkana Yesu kwamba hana uwezo kuusaidia uchumi wako, basi unaye mwingine wa kukusaidia. ila sisi wenzako tunamhitaji Yesu mno hata katika mambo ya uchumi.
na kwa taarifa tu, hatuandiki hivi kwasababu tunalala njaa, au kwasababu tuna umaskini, hapana, tulishawahi kupambana sana kutafuta maisha kwa kutumia elimu, kwa kutumia ujuzi, kwa connections za watu waliofanikiwa nakadhalika, hatukufanikiwa, hadi tulipofunguliwa mlango wa baraka rohoni na Yesu mwenyewe, ndio huku mwilini degree zetu zikaanza kufanya kazi. unaweza kuwa na kila kitu ukatoa jasho lote, usifanikiwe, ila mtu mwingine hana kile ulicho nacho, hajatoa jasho sana amefanikiwa, kwasababu katika ulimwengu wa roho kuna mpenyo, Yesu aweza kukusaidia hata kwenye mambo yako ya kiuchumi. usimdharau kwamba hawezi kukusaidia, unamhitaji.
Namshukuru Mungu nimekuwa ushuhuda unaotembea, kwamba kabla ya kufunguliwa uchumi wangu rohoni, nilitegemea sana akili zangu na jitihada zangu sikufanikiwa, ila nilipokabidhi degree zangu kwa Yesu anisaidie kuzitumia (tena sio moja), nimeshuhudia kufanikiwa sana katika dunia hii hii.
Mimi namhitaji Yesu katika uchumi wangu, Eeh Yesu endelea kunisaidia kadiri pale unapotaka nifikie, wewe ndiwe wa kunipa uhai na nguvu za kufanya kazi, pia unamzuia yeye anipingaye katika uchumi na maisha yangu, bila wewe shetani angeshakula uchumi wangu na angeshafunga milango yangu ya baraka, NAKUHITAJI YESU, NAKUHITAJI YESU, VIVYO KILA SAA, KILA DAKIKA NA KILA SEKUNDE. WEWE NDIWE MWANAUCHUMI WANGU. Kwa Jina lako takatifu ninaomba, Amen.
nawaasa mnaosoma hapa, msimsikilize huyu jamaa, anaposema Yesu hakuwa mwanauchumi hivyo hamhitaji Yesu katika kumsaidia uchumi wake. Yesu ni zaidi ya Mwanauchumi, yeye ni Mungu, anaweza kukusaidia uchumi wako ukafanikiwa. wala msimdharau.