sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
nani anaependa kukaripiwa?
nanj anaependa kupigwa?
nani anapenda kugombezwa?
nani anapenda kupigwa?
nani anapenda kunyanyaswa?
HAKUNA!!!!
Inanishangaza sana kuona kuna baadhi ya wazazi hawaheshimu kabisa mahouse girl wanaobaki na watoto wao, huwaona kama wanadamu wa toleo la pili.
House girl anaweza kuyaficha mengi sana moyoni, wewe ukaona kwamba hajaumia lakini ana vitu vingi sana kakuvumilia ni vile tu hajaamua kubrespond wazi wazi, ndio hapo sasa humuona mtoto wako kama balozi wako, atakachokifanya kwa mtoto wako huendana na unavyoishi nae.
kama unaishi nae vizuri basi kwa kiasi kikubwa nae ataishi na mtoto wako vizuri ila kama unamnyanyasa nakwambia atakuwa anakuchekea usoni ama kujifanya kuchukulia poa unachomfanyia ila unapoondoka asubuhi kwenda kwenye shughuli zako, hapo mtoto wako ndio atatumiwa kulipizia kisasi, nadhani wengi sio wageni wa zile video za siri zinazorekodiwa ma house girl wakiwa peke yao na watoto, huwafanyia watoto unyama ambao unatisha sana.
Ishi vizuri na house girl wako anaekulelea watoto, kumnyanyasa, kumtukana, kumgombeza, kumpiga, n.k ni sawa na kutukana mamba kabla hujavuka mto.....Kisasi humwendea mtoto wako ambae hawezi kulalamika.
House girl wako anaekulelea mtoto hakikisha yupo kwenye mood nzuri, akiwa na mood mbaya inakuwa hatari sana kwa mtoto, kama ni mshahara mlipe kwa wakati, kama ni nguo mnunulie, kama ni kazi basi muwe mnasaidiana sio mambo ya kuamshana saa 11 asubuhi kila siku huku wewe unachapa usingizi, kama mnaenda out muwe mnaenda wote, msimtenge, n.k. akianza kujihisi tu kwamba mnamchukulia kama mwamadamu wa daraja la mwisho hii huwa inamjengea stress, hata kama hamumpigi ama kumtukana ama kumnyanyasa bado inampa stresa kuona anadharauliwa na hana thamani, kwa hizi stress zinamuondolea umakini kwenye kuwalelea mtoto wenu.
JIONGEZEEE!!