SoC01 Jiongeze zaidi

SoC01 Jiongeze zaidi

Stories of Change - 2021 Competition

smartdunia

Member
Joined
Jul 29, 2021
Posts
12
Reaction score
9
"Mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake",msemo huu uliobeba maana,yamkini unatumiwa na waswahili kufikisha ujumbe kwa watu kua watu wanatakiwa kuishi kulingana na uwezo wao wa kimaisha ulipoishia,lakini kwa upande mwingine tunapaswa kukubaliana kua matumizi ya msemo huu ni sahihi kwa asilimia zote ukitumika kwa huyo mnyama aliyetajwa hapo asiyekua na utashi,na sio kwa binadamu aliyejaaliwa akili na utashi.

Mbuzi anakula majani yaliyokaribu na mahali alipofungiwa kwasababu hana uwezo wa kuirefusha kamba yake, ujanja wake upo mikononi mwa binadamu aliyemfunga,anachotakiwa kukifanya ni kutulia na kuhakikisha anatosheka na chakula kilichopo karibu naye.

Lakini wewe kiumbe wa pekee,uliyependelewa utashi na akili zaidi ya mnyama yeyote chini ya jua,Tena ukapewa mamlaka ya kumiliki viumbe wanzako wasio na utashi unapaswa kufahamu kua huna hata chembe ya sababu ya kujifananisha na mnyama yeyote.

Tofauti na mbuzi,unaweza kula kwa urefu wa kamba yako huku ukifikiria ni jinsi gani ya kuongeza urefu wa hiyo kamba hata mara kumi zaidi kwani uwezo unao.

Hoja yangu ya msingi iko wapi?

Hili ndilo swala muhimu zaidi katika makala hii.

Tunatakiwa kushughulisha akili zetu kila siku, kila mara unapofanikiwa, unatakiwa kushukuru, kufurahia kidogo ulichokipata Kisha fikiria njia ya kujiongeza zaidi kwani ni dhambi kubwa kubaki hapo ulipo wakati muda unazidi kusonga mbele.

Kumbuka, maisha ni kama safari ambayo unasafiri huku umebeba mzigo,mzigo wa maisha ukichoka kuubeba kichwani, unauhamishia begani, Kisha unaurudisha kichwani huku safari inaendelea,ukithubutu kuushusha chini umekwisha kwani hiyo itakua ndio maana halisi ya kukata tamaa.

Ni ajabu kuona unatumia njia zilezile, kufanya kitu kile kile alafu utategemea mabadiliko katika safari yako,unapoona mabadiliko yanaleta ugumu, tunapaswa kua wepesi kujifunza vitu vipya na kubuni mbinu mpya ili kuleta matokeo mengine,ili mradi tusonge mbele,tusiwe kama mbuzi anayekula kwa urefu wa kamba yake na kuishia hapo hapo,yeye hana makosa kwani upeo, hakupewa.

Mwisho nipende kunukuu kutoka kwa mwandishi mmoja maarufu aitwaye Vincent Van Gogh aliyeandika.

"Great things are not done by impulse, but by a series of small things brought together" .

Maana halisi yenye kueleweka ni kwamba, mambo makubwa hayafanyiki ghafla tu,ni matokeo ya vitu vidogo vidogo ambavyo vimeungana na kutengeneza hicho kitu kikubwa.

Bila shaka hata swala la muda linahusika,hivyo fanya jambo dogo leo,usiishie hapo,kesho ongeza zaidi kwa mbinu na maarifa kisha ipo siku utahisi umebadili dunia yako kua kama pepo.


Nikutakie mabadiliko mema.
 
Upvote 1
Samahani Mleta uzi hivi huyu mwandishi vicent van go ndio aliyeandika kitabu cha satanic verse kilichomletea shida kutoka kwa jamii ya waislamu?[emoji15]
Hicho kitabu cha satanic verse wanadai kilileta mushkeli sana haswa kwenye ulimwengu wa waislamu wakidai kinamkashifu mtume wao SAW
 
Vincent van Gogh kwa mujibu wa Wikipedia [emoji116]

Vincent Willem van Gogh was a Dutch post-impressionist painter who posthumously became one of the most famous and influential figures in the history of Western art. In a decade, he created about 2,100 artworks, including around 860 oil paintings, most of which date from the last two years of his life. Wikipedia
 
Back
Top Bottom