Jioni moja miaka mingi iliyopita na Subhash Patel

Jioni moja miaka mingi iliyopita na Subhash Patel

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
subhash_patel_CMD.jpg

Subash Patel nilimjua katika miaka ya mwishoni 1970 au mwanzoni 1980 kupitia rafiki yake Said Ibrahim ambaye mimi pia ni rafiki ndugu.

Said ndiye alinipeleka nyumbani kwake.

Miaka hiyo alikuwa anaishi nyuma ya Zanzibar Guest House Mtaa wa Zanaki na Libya Street sehemu za Kisutu. Siku hizo Subash hakuwa tajiri lakini mfanyabiashara kijana anaeinukia. Ninachokumbuka kila nilipokuwa nasoma jina la Subash katika magazeti au kumuona katika TV ni kuwa ilikuwa nyumbani kwake ndipo nilipoiona movie mashuhuri, "The Message," kwa mara ya kwanza.

Hii ilikuwa sinema maarufu sana kuhusu maisha ya Mtume Muhammad (SAW). Sinema hii tukiisoma sifa na "reviews," zake kwenye magazeti tu kwani enzi hizo Tanzania ilikuwa hoi na taaban kwa kila kitu.

Sinema za Hollywood zilikuwa haziingii nchini. Waagizaji wa filamu Tanzania Film Company (TFC) kazi iliwashinda kabla hata hawajaianza. Kwangu Mimi kupata nafasi ya kuangalia sInema hii halikuwa jambo dogo.

Iko siku Subhash alikuja ofisini kwetu alikuwa na miadi na Mkurugenzi wa Idara tukaonana na kusalimiana lakini hakunikumbuka. Ilikuwa miaka mingi imepita na ilikuwa tumeonana mara moja tu.
 
Umri nao unachangia, huyu mzee smartpone kajifunza juzi tu unataka aandike ese?
Einstein1...
Mie mtaalamu bwana usinifedheheshe vijana wakanishambulia, "Oh huyu mzee mshamba."

Nimeanza kusoma word processing "Word Perfect" na DOS Command Uingereza bado kijana.

Hakuna Windows enzi hizo.

Command zote unahifadhi kichwani!
 
1gb

Wewe ni mtu wa pili kunilaumu.
Kipi hakijakaa sawa?
Mzee, Nafikiri hawajaelewa kwamba, Subhashi hakuwa mtu wako wa karibu ila kwa kuwa ni figure kwenye taifa basi si vibaya ukaandika jambo ukumbukalo kumhusu. Walitaka ulete ubuyu hapa kama vile ulikuwepo wakati anakufa. All in all namtakia heri katika hatua yake ya maisha inayofuata.
 
Mzee,Nafikiri hawajaelewa kwamba,Subhashi hakuwa mtu wako wa karibu ila kwa kuwa ni figure kwenye taifa basi si vibaya ukaandika jambo ukumbukalo kumhusu.Walitaka ulete ubuyu hapa kama vile ulikuwepo wakati anakufa.All in all namtakia heri katika hatua yake ya maisha inayofuata.
Andoza,
Ahsante sana.
 
Back
Top Bottom