Jioni ya 4/11/2019 safarini Uganda kibiashara

Hv hamnaga zile temporary permit pale mpkani,maana naona ishu ya passport imekuwa ngumu sana sshv.
 
Huo ndo ukweli. Maisha ni Magumu sana Uganda na kuna ukienda ndanindani huko kina umasikini wa kutisha
 
Kamanda mpambanaji uko njema ila tujulishe kila hatua [emoji16][emoji16][emoji16]
 
hongera sana samahani hv nikiwa na mtaji wa laki 6 ya tz nikiingia Ug si mtaji tosha huko
Thanks mkuu mtaji wowote unatosha lakini lazima uzingatie wapi Unatoka (Mkoa) na mzigo wako unaokwenda kuchukua ni upi
 
duh asee hataree
 
Wenyeji wanashauri uwe na mtu Kampala ukifika Mtukula unauliza rate ya kule town ni ngapi mfano mimi border rate ilikua 1.58 wakati town ilikua 1.56
Cjawah kuchange rate hiyo 1.57,56,58 ukichange mpakan ndo majanga yenyewe hayoo
 
Nataka nikafunge mizigo miwili
1:sandals za mtumba za kiume kutoka Italy
2:Nguo za watoto za mtumba
Mizigo hii yote iwe grade1
Je mil3 nitarudi na mzigo wa maana kweli na ukanilipa?
Msaada wenu wa mawazo ndg zetu
mlioenda huko.
Kwa Mimi hapo kwenye mtumba nitakudanganya ila Zingatia sehemu unayotoka mfano watu wa Dar to Kampala Nauli ni 110,000/= ukikata moja kwa moja lakini ukiunga ni around 75-80 mpka Kampala
 
Kamanda mpambanaji uko njema ila tujulishe kila hatua [emoji16][emoji16][emoji16]
Muhimu sana ukifika Uganda Jitahidi kupata hotel yenye Wi-Fi kidogo utarahisisha mambo yako na kuna hotel bei ni 25,000/= ya kibongo ya kiganda ni 40,000/= pale unapata Wi-Fi na breakfast asubuhi .so ukienda mizunguko cm inakua ya kupigia Picha tu au kuangalia muda au calculator
 
Kwani mitandao yao haina Data?
Mbona mleta mada hujatueleza vizuri kuhusu hiyo Kampala?
 
Reactions: rr4
Ulifanikisha kilichokupeleka?

Kuna utofauti gani na hapa Dar?

Ushuru ulilipa kiasi gani?

Gharama za kusafirisha huo mzigo ulilipa kiasi gani?
 
Kwani mitandao yao haina Data?
Mbona mleta mada hujatueleza vizuri kuhusu hiyo Kampala?
Fuatilia comments hapa au ukiuliza swali nitakujibu

OK kuhusu mitandao ni kama unatumia line za Tz ukivuka mtukula zote zinakua hazifanyi kazi isipokua Voda iko hewani mtu wa Tz akikutumia Ujumbe unaupata ila huwezi kumjibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…