Hapo haiwezekani , hata kama utabadilisha date format sio kwamba hizo tarehe zitajibadilisha zenyewe kwenda kwenye miezi na miezi kwenda kwenye tarehe,kuset format ilibidi uifanye kabla ya kuanza.
Suluhisho ni kuweka column tatu ambazo zitakuwa na heading ya date,month,year then kwenye column ya Age utaandika hii formula
=DATEDIF(DATE(D4,E4,F4),TODAY(),"y") ambapo column D itakuwa ni date,column E ni month na column F ni year
Baada ya hapo sasa, ivunje hiyo column ya birth date kwa kutumia text to column ili tarehe,mwezi na mwaka vijitenge na kuingia kwenye hizo column tatu ulizoziinsert. Hapo sasa ndo ufanye evaluation japo haitowezekana kuzirekebisha zote kwa sababu hutoweza kutrack error kama tarehe iliyojazwa kimakosa ipo kwenye mwezi na ni chini ya 12. Mfano unaweza ukaandika kwenye column ya pembeni, =IF(E4>12,"error","") then ukadrag mpaka chini,ambapo column E ni column za miezi so ikileta hilo neno la error unafanya exchange ya date na month.
Pia tumia input message ambayo ipo kwenye data validation kama user instruction( mtu akiclick cell, text box inadisplay ambayo inampa maelekezo) vinginevyo tumia freeze pane ili mtu anaposcroll down,heading za column ziendelee kuonekana. Nimeelezea juu juu lakini nina imani utakuwa umeelewa