INAUZWA Jipatie Excel Template ya kuchakata matokeo ya wanafunzi (O-level) kwa sh 35,000/=

Shukran mkuu ngoja nianze nazo..
Ila ni zipi function zinatumika saana katika project kama hii ya kwako...

Yaani uwezo wa kuliko data ya sheet moja na sheet nyingine...

!?

Unaanza na sheet name kabla ya jina la cell, baada ya sheet name unaweka alama ya ! Mfano =A5+'setting'!B7
Njia rahisi ni ya kuselect sheet kwenye sheet tab (ukishaandika =A5+ unaselect sheet unayotaka then unaselect cell)
Pia unaweza ukalink data ambazo zipo kwenye workbook tofauti tofauti
 
Shukran mkuu... Kwa iyo nkitaka kuisoma mitandaon hii condition sijui function huwa inaitwaje kitaalamu mkuu?
 
Kuhusu penati mkuu huo mfumo bado unatumika ? maana mwaka huu kuna madogo wana F math na division imebaki vile vile na hata ukihesabu point sawa
 
Kuhusu penati mkuu huo mfumo bado unatumika ? maana mwaka huu kuna madogo wana F math na division imebaki vile vile na hata ukihesabu point sawa
Miaka ya nyuma ulikuwa unatumika lakini kwa sasa sifahamu (Mimi sio mwalimu). Nimeweka kama optional ili mtu aamue mwenyewe, angalia kwenye picha za report hapo juu
 
Kiongozi unitengezea sheet template ya kurekodi mauzo na manunuzi ya kiduka changu?
 
Select header ya column husika, then right click kisha chagua format cells. Kwenye data type badili hiyo general, chagua date kisha tafuta date format ambayo utakuwa unatumia kujaza birthday date zako
Nimekusoma saana mkuu... Iyo nilishafanya ila bado tatizo likawa lipo...

Alafu kilichopo ni kwamba data tayari zipo na ni nyingi km majina elfu 5 hivi... Na walioingiza data kila mtu aliingiza ajuavyo.. Kuna mwengine alianza mwez then date.. Mwingine alianza date then month.. Si unajua tareh ikiwa chini ya 12 inatambulika km mwez sometime..

Kwa iyo ni data nyingi ambazo zimetiwa katika mifumo tofaut.... Nikataka niichange zoote kwenye format moja then niitie iyo formula.. Sasa nilijaribu stil nikaona error sasa sijuh hata nafeli wapi aisee
 
Okoa muda, rahisisha mambo,kuwa tofauti na wengine. Hii sio software, ni Ms excel, haina malipo ya ziada utaitumia Maisha yako yote
Nikihitaji ya A level kupanga matokeo ya shule zaidi ya moja bei gani?
Iwe na vitu vifuatavyo
Matokeo kwa division (reg namba na majina)
Best ten kwa kila somo
Best ten overall na kwa jinsia
Results summary
....
 
Nashukuru saana mkuu nimeeelewa vizuur saana nkienda job weekend au j3 nitaifanyia kazi mkuu... Shukran saana ubarikiwe... Ngoja nikikamilisha hili ntakuungisha templates zile mkuu
 
Naona hapo class timetable. Nadhani tengeneza yenye uwezo wa school timetable, inayo involve madarasa, vyumba , masomo ya madarasa tofaut na walimu wa masomo husika yan inakuwa overall timetable ya mikondo yote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…