Jipatie Nakala yako: Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania by Nyerere

Jipatie Nakala yako: Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania by Nyerere

Saafi saana, jamani na mi naomba kama twaweza kupatiwa soft ya report ya tume ya Jaji Kisanga na Nyarali,MM au moderator mwaweza kunisaidia au kutusaidia na kwa wengine ambao wako interested nimejaribu ku google but nimekosa please amd please au mwa forum yeyote alie nazo
 
Mimi sishangai kwa kitabu hicho kupigwa marufuku, hili linawezekana kabisa kwa viongozi tuliona katika serikali ya sasa, haswa pale inapoonekana kwamba inakosoa, inafichua au kuumbua utendaji kazi wa viongozi walioko madarakani. Mbaya zaidi ni pale inapoonekana kwa kilichopo ndani ya kaitabu hicho kinaweka wazi uchafu uliogeuka kuwa madoa au kutu ndani ya serikali ya CCM. Kwani marufuku maana yake nini? Hata kumzuia kiongozi wa serikali/mbunge kuzungumzia Dowans hiyo pia ni marufuku tosha. Hapa cha kufanya ni kumuomba Mzee Mwanakijiji atutafutie hicho kitabu ili tukisome na kuweka wazi maono ya Mwl. Nyerere. Kama watanuna shauri yao.
 
mbona document aliyoweka mdau mlenge ina makosa mengi (grammatical errors)?
 
sikutegemea kusikia kimepigwa marufuku, lini jamani? kweli tunaelekea kubaya, hicho kaandika mwenye nchi,sie akina fulani si tutachapwa viboko hadharani? akili mkichwa nchi isha uzwa ajamani
 
mbona document aliyoweka mdau mlenge ina makosa mengi (grammatical errors)?
Sijaweka nakala ya kitabu chochote hapa! Nakala hiyo imewekwa na mmiliki / modereta wa Jamiiforums.
 
Nakumbuka hicho kitabu kilitoka mwaka 1994 enzi ya mzee ruhsa. Kilikuwa kinakosoa mambo mengi ya serikali ya awamu ya pili. Kulikuwa na malumbano makali kati ya serikali na nyerere. Huwezi amini ungesima magazeti ya kama uhuru na mzalendo yalimponda sana baba wa taifa kama kwamba si mwenzao.
Ikawa kama jamii ilitaka kugawanyika pande mbili, ndipo serikali ilipoamua kuzinunua copy zote mitaani. Nakumbuka kilikuwa kinauzwa kama vitabu vingine tu mitaa ya samora dar, na bei yake ilikuwa ni tshs 1,000/- tu.
Sina shaka kitabu hiki kimefichwa kwenye kabati moja na KATIBA.
 
Natafuta kitabu kilichoandikwa na J.K. Nyerere, "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania" kwa Kiswahili au Kiingereza.

Jitihada za kukipata mitaa ya Dar zilishindikana baada ya kuambiwa 'udaku' kwamba kimepigwa marufuku kinamna. Madukani mwa vitabu mwote nilimopita kukiulizia waliniona juha, kana kwamba 'kila mtu anajua' kitabu kilipigwa marufuku.

Madai hayo ni ya kweli au uzushi tu wa uchaguzi?

Shida yangu ni nakala moja tu ya kitabu hicho kwa ajili ya rejea ya kitaaluma.

Natanguliza shukrani.

Amazon.com: Mlenge Fanuel Mgendi: Books, Biography, Blog, Audiobooks, Kindle

=============
UPDATE by JF Admin:

Kwa msaada wa mkuu SubiriJibu kitabu kimepatikana, nakala inaweza kupatikana chini hapa
Mkuu jaribu Tanzania Publishing House (TPH) mtaa wa Independence Avenue ( Samora siku hizi, I like old names they had good meanings). Pana vitabu vingi vya wabongo pale.
 
Back
Top Bottom