Jipatie Nakala yako: Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania by Nyerere

Jipatie Nakala yako: Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania by Nyerere

- Haya mkuu ngaoja niwaachie huu mjadala maana naona inatakiwa uniform kihitaji the otherside nipo anytime, huu mjadala ni mzuri ila matusi sio sawa maan wengi tunamheshimu sana Mwalimu, naomba kujitoa sasa.

FMEs!

Aaah bwana wewe, usiwe na hasira za hivyo...ni heshima hiyo hiyo kwa Mwalimu inayotufanya wengine tuwe wakali mno mwalimu akitukanwa!....pole sana.
 
huu ndio umuhimu wa kuwepo mtandao. ingekuwa kiandikwe sasa hivi hata kama kingekosekana madukani lazima mtandaoni kingekuwepo.
 
Heshima kwako Mlenge,

Naomba kukupa shukrani zangu za dhati kwani jambo ulilolifanya ni jema kwa Tanzania ya sasa na vizazi vijavyo.

Nimesoma kitabu chote nimebaini mambo matatu makubwa.

[1] Mzee Ruksa hakustahili kuwa rais wa Tanzania kwasababu si mtu wa kuchukua maamuzi magumu kama ilivyo kwa Muungwana leo.Nina hakika Mwl Nyerere angekuwa hai leo angemwambia Kikwete awaondoe kwenye chama kundi la mafisadi akiaanza na E Lowassa,A Chenge,R Azziz na wengine wote waliohusika kwa njia moja au nyingine kufilisi hazina ya taifa letu kwa njia za kitapeli.Nina hakika Mwl angekuwa hai leo asingekubali kazi ya kupatanisha makundi yanayokinzana [Sitta Dhidi ya Rostam & E Lowassa] ndani ya CCM,angemshauri Muungwana kuwaburuza mahakamani wezi badala ya kuwakumbatia.

[2] Ndoto za kutaka kuwa rais wa Tanzania zilisababisha Mzee J S C Malecela ashindwe kukemea,kupinga na kutetea maslahi ya taifa ndani ya bunge na ndani ya vikao vya chama.Mzee J C Malecela kwa namana ya ajabu alishindwa kusimamia hata mambo ambayo ni rahisi kuyasimamia akiwa na wadhifa wa waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais,kwakushindwa kufanya hivyo nadhani haikuwa busara kuachiwa kugombea wadhifa wa urais wa Tanzania.Nadhani Mwl alikuwa sahihi kumtupa nje katika kindumbwe ndumbwe cha kugombea urais wa Tanzania.

[3] Mwl Nyerere alikuwa ni kiongozi mwenye maono ya mbali na alikuwa na uwezo wa kutetea,kusimamia na kulinda jambo analoliamini.Mwl Nyerere atabaki na kosa moja kubwa ambalo mpaka leo bado linanipa shida sana hasa tunapomjadili ni kuwaaminisha waTanzania kwamba B W Mkapa ni kiongozi safiiiii [Mr clean].Hii dhambi Mwl hawezi kuepuka sijui ulemchakato wa kumfanya mtakatifu umeishia wapi labda watu wamestuka.
 
Ahsante Ngongo kwa analysis nzuri. Japo sijakisoma kitabu naomba kuongeza hapo kwenye no 3. Nachelea kuita kosa au sijuwi niiteje. Anyway niite kosa tu. Kwangu mm kosa kubwa kuliko yote ambalo Mwalim alilifanya na ndilo linalotutesa na litakaloendelea kututesa endapo halitafanyiwa kazi ni katiba ya nchi. Mzee ulimwengu aliliweka vizuri sana siku moja. Alisema kuna watu wanadhani Mwalimu alikuwa ni sehemu ya katiba lakini yeye anaamini katiba yetu ni sehemu ya Mwalimu.Nakubaliana 100% na Mzee Ulimwengu. Mwalimu alifanya makosa makubwa sana kutokubalisha katiba kabla ya kuondoka madarakani. I know alijuwa angeelekewa vibaya lakini hiyo ilikuwa bora kuliko huu upuuzi unaoendelea sasa.

Katiba yetu imemfanya rais kuwa mungu mtu yaani ni zaidi ya kuwa executive president which is very dangerous kama mkipata mtu asiye mtendaji kama ilivyo sasa. Unajuwa kuna kipindi namwangalia rais wetu wa sasa then ninamreflect na Mwalimu akili yangu inagoma kwamba watu hawa wawili hawawezi wote kuwa marais wa Tanzania kwa katiba ile ile no way lazima itakuwepo shida kubwa tu na ndio yanayotokea.Hope nimeeleweka.
 
Bien recu.

Well received

Thanks

Natafuta kitabu kilichoandikwa na J.K. Nyerere, "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania" kwa Kiswahili au Kiingereza.

Jitihada za kukipata mitaa ya Dar zilishindikana baada ya kuambiwa 'udaku' kwamba kimepigwa marufuku kinamna. Madukani mwa vitabu mwote nilimopita kukiulizia waliniona juha, kana kwamba 'kila mtu anajua' kitabu kilipigwa marufuku.

Madai hayo ni ya kweli au uzushi tu wa uchaguzi?

Shida yangu ni nakala moja tu ya kitabu hicho kwa ajili ya rejea ya kitaaluma.

Natanguliza shukrani.

Mlenge

=============
UPDATE by JF Admin:

Kwa msaada wa mkuu SubiriJibu kitabu kimepatikana, nakala inaweza kupatikana chini hapa
 
Ahsante Ngongo kwa analysis nzuri. Japo sijakisoma kitabu naomba kuongeza hapo kwenye no 3. Nachelea kuita kosa au sijuwi niiteje. Anyway niite kosa tu. Kwangu mm kosa kubwa kuliko yote ambalo Mwalim alilifanya na ndilo linalotutesa na litakaloendelea kututesa endapo halitafanyiwa kazi ni katiba ya nchi. Mzee ulimwengu aliliweka vizuri sana siku moja. Alisema kuna watu wanadhani Mwalimu alikuwa ni sehemu ya katiba lakini yeye anaamini katiba yetu ni sehemu ya Mwalimu.Nakubaliana 100% na Mzee Ulimwengu. Mwalimu alifanya makosa makubwa sana kutokubalisha katiba kabla ya kuondoka madarakani. I know alijuwa angeelekewa vibaya lakini hiyo ilikuwa bora kuliko huu upuuzi unaoendelea sasa.

Katiba yetu imemfanya rais kuwa mungu mtu yaani ni zaidi ya kuwa executive president which is very dangerous kama mkipata mtu asiye mtendaji kama ilivyo sasa. Unajuwa kuna kipindi namwangalia rais wetu wa sasa then ninamreflect na Mwalimu akili yangu inagoma kwamba watu hawa wawili hawawezi wote kuwa marais wa Tanzania kwa katiba ile ile no way lazima itakuwepo shida kubwa tu na ndio yanayotokea.Hope nimeeleweka.

Heshima kwako Bobby,

Upo sahihi kabisa mkuu wangu.
Nadhani hata Mwenyezi Mungu akituangalia anatushangaa jinsi tulivyomfanya mwanandamu mwenzeti afananefanane na yeye.
 
- Jasusi with all due repsect, the ishu hapa ni kwa nini walitaka kumpindua sio kwa nini walishindwa!

FMEs!
FMES,
They are all related. Nkrumah alipinduliwa. Lumumba aliuawa. Ben Bella alipinduliwa
na close associates wake. Sylvanus Olimpio alipinduliwa. Milton Obote alipinduliwa. All this in the 60-70's Kwa nini Nyerere alisurvive? That is the issue. And in fact I asked it as a rhetorical question. Kama hauna jibu mimi nitarudi na jibu lake.They are all related!
 
Aaah bwana wewe, usiwe na hasira za hivyo...ni heshima hiyo hiyo kwa Mwalimu inayotufanya wengine tuwe wakali mno mwalimu akitukanwa!....pole sana.

- Mkuu nimekusikia sana, mimi sijamtukana wala kumkashifu Mwalimu, kwanza ni against mafundisho ya dini yangu, ninachofanya ni kujaribu kuweka the otherside with a Critical Analysis, Mwalimu amenisomesha bure, amenipa ID yaani utaifa, Shuleni nimelima mashamba ndio maana leo ninaweza kufanya kazi yangu binafsi kwa masaa 13 mpaka 15 kwa siku, JKT nimejifunza uvumilivu na ukakamavu, kukosa vitu vya anasa kumenifanya niwe na self restraint katika kupursue anasa au kuweza kuishi bila kua navyo, Mwalimu pia amenipa anwani kule kijijini, akanipa heshima na kupendana na wananchi wenzangu bila kujali uwezo wao wala nafasi zao katika jamii, Mwalimu alikuwa ana command a great repsect kwa viongozi wenziwe, na mengine mengi ambayo simply binafsi ninaamini he was the greatest, watoto wake wote ni marafiki zangu wa karibu sana, ninawaheshimu sana maana huenda hawana mali za ajabu lakini wana heshima kama wananchi wengine na ni watu wa kawaida sana,

- Tatizo langu na hiki kitabu ambacho ninakijua kwa kurasa tena nje ndani, ni simply a misleading book, kwa sababu nia ilikuwa kumzuia Malecela asiwe Rais kwa sababu zao wawili za kibinafsi ambazo hazina anything to do na taifa. Kwa mfano kitabu in general kinasema tatizo letu Tanzania ni Muungano, I mean what the hell is Muungano katika maisha yangu ya kila siku na ya wengine wote wananchi wa Tanzania? To me Muungano ni tatizo la viongozi wa juu wa taifa ambao wanajaribu kuutumia kutafuta power, kuna wa-Zanzibari wengi wanaotaka kuwa marais wa Jamhuri sasa wakishindwa kwenye ndoto zao hizo ndio wanaleta kelele kuhusu Muungano.

- Again, Mwalimu anatatizwa na viongozi wanaotaka power, lakini anasahau kwamba na yeye did the same thing kwa nini hakuridhika na Uwazriri mkuu tu na ni sheria gani alivunja kwa kuwa na hizo ambitions? Halafu anasema Malecela alivuruga serikali kwa kutaka power, lakini anasahau kwamba ni yeye mwenyewe ndiye aliyemtumia Salmin kuiba uchaguzi wa Zanzibar 1995 sasa kweli hiki kitendo hakikuwa cha kuharibu serikali, unafikiri kwa nini mpaka leo tunaibiana kura za uchaguzi ni kwa sababu ya matendo kama haya ya Salmin yaliyopewa baraka na Mwalimu, kuna viongozi waliyoyaona kama kina Almeir, ambao mpaka leo wanaendeleza yale yale ya kuiba kura.

- I can go on and on na hiki kitabu na mazingaombwe yake, kama vile Mwalimu anamlaumu Mwinyi kwamba ni weak, sasa amesahau kwamba ni yeye mwenyewe aliyetupa huyu Rais, sasa kama amegundua kwamba hayuko kama alivyotegemea ustaarabu alitakiwa kutuomba msamaha wananchi kwamba samahani sana kwa kuwachagulia kiongozi asiyefaa, na kwamba sitarudia kuwachagulia Rais tena, no bado akatuchagulia Mkapa, tizama tulipo sasa ndugu yangu tumekwama sisemi kwamba matatizo yote tuliyonayo ni ya Mwalimu, lakini wapi his responsibility?

- Kumtukana Mwalimu no way siwezi, ila ninajaribu tu kuangalia solution ya matatizo ya nchi yangu sikuona yaklijadiliwa kwa kina na mapana, badala ni beef za personal tu zilizojaribiwa kugeuzwa kuwa a national ishu kwa maoni yangu!

Respect.

FMEs!
 
Heshima kwako Mlenge,

Naomba kukupa shukrani zangu za dhati kwani jambo ulilolifanya ni jema kwa Tanzania ya sasa na vizazi vijavyo.

Nimesoma kitabu chote nimebaini mambo matatu makubwa.

[1] Mzee Ruksa hakustahili kuwa rais wa Tanzania kwasababu si mtu wa kuchukua maamuzi magumu kama ilivyo kwa Muungwana leo.Nina hakika Mwl Nyerere angekuwa hai leo angemwambia Kikwete awaondoe kwenye chama kundi la mafisadi akiaanza na E Lowassa,A Chenge,R Azziz na wengine wote waliohusika kwa njia moja au nyingine kufilisi hazina ya taifa letu kwa njia za kitapeli.Nina hakika Mwl angekuwa hai leo asingekubali kazi ya kupatanisha makundi yanayokinzana [Sitta Dhidi ya Rostam & E Lowassa] ndani ya CCM,angemshauri Muungwana kuwaburuza mahakamani wezi badala ya kuwakumbatia.

[2] Ndoto za kutaka kuwa rais wa Tanzania zilisababisha Mzee J S C Malecela ashindwe kukemea,kupinga na kutetea maslahi ya taifa ndani ya bunge na ndani ya vikao vya chama.Mzee J C Malecela kwa namana ya ajabu alishindwa kusimamia hata mambo ambayo ni rahisi kuyasimamia akiwa na wadhifa wa waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais,kwakushindwa kufanya hivyo nadhani haikuwa busara kuachiwa kugombea wadhifa wa urais wa Tanzania.Nadhani Mwl alikuwa sahihi kumtupa nje katika kindumbwe ndumbwe cha kugombea urais wa Tanzania.

[3] Mwl Nyerere alikuwa ni kiongozi mwenye maono ya mbali na alikuwa na uwezo wa kutetea,kusimamia na kulinda jambo analoliamini.Mwl Nyerere atabaki na kosa moja kubwa ambalo mpaka leo bado linanipa shida sana hasa tunapomjadili ni kuwaaminisha waTanzania kwamba B W Mkapa ni kiongozi safiiiii [Mr clean].Hii dhambi Mwl hawezi kuepuka sijui ulemchakato wa kumfanya mtakatifu umeishia wapi labda watu wamestuka.

- Mwalimu alikua sahihi kumtupa nje, sasa kwa nini hawa viognozi wa sasa hawako sahihi kuivuruga Demokrasia yetu kama wanavyofanya, ndiko tulikoiga hapo mkuu uliposema Mwalimu alikuwa sahihi in the process alikuwa anaipindisha Demokrasia na ndio tatizo tulilo nalo mpaka leo, now you can see ni kwa nini hatutakuja kutoka hapa tulipo!

FMEs!
 
FMES,
They are all related. Nkrumah alipinduliwa. Lumumba aliuawa. Ben Bella alipinduliwa
na close associates wake. Sylvanus Olimpio alipinduliwa. Milton Obote alipinduliwa. All this in the 60-70's Kwa nini Nyerere alisurvive? That is the issue. And in fact I asked it as a rhetorical question. Kama hauna jibu mimi nitarudi na jibu lake.They are all related!

- Mkuu wangu kama ninaelewa niligusa ishu ya kupendwa na kutopendwa na wananchi ambayo Mwalimu ameisema sana kwenye hiki kitabu, kwa nini Mwalimu hakupinduliwa ni Topic byitself, fungua thread on that hapa tujadili kitabu na mistari yake, nilichokuwa ninakisema ni kwamba hata Mwalimu kuna waliokuwa hawamtaki na walionyesha kwa vitendo ndio hasa historia tuliyonayo, historia haindikwi na Rais au Mfalme, Yesu hakuandika historia, wala Nabii musa historia huandikwa na wananchi watawaliwa, sio watawala maana hakuna Mfalme anayeweza kukubali makosa yake siku zote yatakuwa ya wengine tu!

- Hivi Hitler angeandika kitabu kingekua ni cha namna gani?

Respect.

FMEs!
 
Hitler alishaandika kitabu. Tena kilikuwa bestseller. Kinaitwa Mein Kampf!

- Mkuu wangu si umekiona je kinaweza kuwa muongozo wa historia, maana kilikuwa kimejaa ideas za yule mwalimu aliyekwua mshauri wake na mentor wake, ubaguzi mtupu sasa kinawezaje kua history! Otherwise, ahsante kwa kumbu kumbu mkuu tupo pamoja sana.

FMEs!
 
Sasa hali ya Zimbabwe imeharibika zaidi, na hata kama kuna demand ya hicho kitabu, Mchapishaji wake hawezi kukichapisha.Labda Mzee MwanaKijiji angefanya mpango akaomba kichapishwe hapa Tanzania, basi hao wanaotaka kukisoma wangepata "new edition".

Mzee mara mwisho umeenda lini Zimbabwe? Una uhakika kuwa mchapishaji huyo hawezi kukichapisha? Au ni hisia tu za Ki-BBC?

Pamoja na maswali yangu hayo ni wazo zuri kumuomba tuchapishe Tanzania au tuchapishe pamoja naye. Inawezekana pia hakimiliki ya kitabu hicho ni ya familia ya Mwalimu. Tuiombe pia.
 
mengi yameandikwa kwa sifa na kebehi lakini ukweli utabakia kwamba mwalimu katuachia mtihani mkubwa sana. Huu mtihani upo ndani ya maelezo yake na yale aloyafanya kwani katika kumsoma vizuri mwalimu tukubaliane kwamba mwalimu Nyerere hakuwa mtu mwenye maamuzi mazuri ktk MIRATHI..iwe familia yake ama Kitaifa kwani kosa kubwa la mwalimu pamoja na upendo wake kwa nchi yetu na wananchi wake ni ktk kukabidhi madaraka ya Uongozi.
Hivyo kuwadharau watu wengine na kuwaita wahuni hali chaguo lako ndilo linaonyesha uhuni zaidi nadhani bila shaka mwalimu alikuwa mhuni pia. Mimi siku zote nitalia na mwalimu ktk kuomboleza kwani ndiye aliyekabidhi madaraka ya nchi yetu kwa WAHUNI tunaowajua sisi. He meaned good hilo halina Ubishi lakini maadam tunakwenda chini, hayo namwachia Mungu..
Kawaita hao kina Malecela wahuni, Lowassa, Sitta na wengineo wengi tu kama wahuni, lakini alishindwa kuuona Uhuni wa wanae mwenyewe hao kina Mwinyi na Mkapa na kundi zima la mawaziri waliofuata walikuwa wahuni kupita kipimo chochote cha uhuni, hasa walipopata barehe ya uchaguzi wa mwaka 2000.
Hivyo sisi wananchi tumewaona wahuni wote ktk makundi tofauti na nadhani sisi wananchi ndio tyunaotakiwa kuandika vitabu kama hivi.
Na kama alivyosema FMES, ni kutokana na maamuzi yake ndio maana tupo hapa leo hii. Tanzania imekuwa nchi ya USANII, iuliyojaa madalali wauza nchi kama nyumba za Kariakoo. nchi yetu inanadiwa kama nyumba za Kariakoo na kama mtakumbuka niliwahi sema kila mageuzi ndani ya Kariakoo, hu refrect mikakati ya nchi nzima kiutawala. hapa ndipo tuliposimama leo hii ya kesho anayajua Mungu.

Binafsi nimechoka na hizi hadithi za Mwalimu, Mwinyi, Mkapa na sijui JK...kwani nguvu ya taifa letu ni sisi wananchi wenyewe.. tulikubali hali hizo wakati ule na tunaendelea kukubali imani potovu ya kuabudu viongozi wetu kiasi kwamba wao wamefikia kuwa kama MIUNGU wetu..Haswa viongozi wanaelewa fika kwamba sisi wananchi tunawaogopa na sii kuwaheshimu, sisi ni watumwa ndani ya Uhuru kiasi kwamba hakuna tofauti ya kimaisha baina ya kuwa uhuru ama kutawaliwa kwa sababu ukiitazama tanzania kiuchumi ipo kwa maslahi ya watu wachache tu..Hivyo watawala wetu - iwe wazungu, waarabu ama waafrika weusi, haiwezi kuondoa maana halisi ya Utumwa wa mwananchi.
Hatma ya Tanzania haiwezi kutazamwa kwa kufuata hulka na tabia za viongozi kwa sababu Tanzania imejaa wasanii, wacheza sinema ambao wanasubiri tu role watakayo pangiwa kucheza..Ni muhimu sana kwa wananchi kuanza kujipanga Upya, kutazama watu na mazingira kulingana na wakati. Ya mwalimu yameisha pita, aloandika sii elimu bali matukio na fikra zake yeye..Na sii lazima iwe ndio ukweli wenyewe kwani tumeyaona kwa macho yetu wenyewe wahuni ni kina nani - Hao alowapa uongozi wa nchi yetu kwa jumla yao ndio wahuni wa kweli kwani wote hawa hula toka sahani moja..
 
- Mkuu wangu si umekiona je kinaweza kuwa muongozo wa historia, maana kilikuwa kimejaa ideas za yule mwalimu aliyekwua mshauri wake na mentor wake, ubaguzi mtupu sasa kinawezaje kua history! Otherwise, ahsante kwa kumbu kumbu mkuu tupo pamoja sana.

FMEs!

Umekisoma? Kwani historia ni nini? Zifuatazo ndizo sura zake - Je, sio Historia hiyo au Propaganda sio Historia au sehemu ya Historia?

Chapter 3: Subjects and Citizens
Chapter 4: Personality and the Conception of the Völkisch State
Chapter 5: Philosophy and Organisation
Chapter 6: The Struggle of the Early Period – the Significance of the Spoken Word
Chapter 7: The Struggle with the Red Front
Chapter 8: The Strong Man Is Mightiest Alone
Chapter 9: Basic Ideas Regarding the Meaning and Organization of the [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Sturmabteilung"]Sturmabteilung[/ame]
Chapter 10: [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Federalism"]Federalism[/ame] as a Mask
Chapter 11: [ame="http://en.wikipedia.org/wiki/Propaganda"]Propaganda[/ame] and Organization
Chapter 12: The Trade-Union Question
Chapter 13: German Alliance Policy After the War
Chapter 14: Eastern Orientation or Eastern Policy
Chapter 15: The Right of Emergency Defense

Source: [ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Mein_Kampf[/ame]
 
Mzee mara mwisho umeenda lini Zimbabwe? Una uhakika kuwa mchapishaji huyo hawezi kukichapisha? Au ni hisia tu za Ki-BBC?

Pamoja na maswali yangu hayo ni wazo zuri kumuomba tuchapishe Tanzania au tuchapishe pamoja naye. Inawezekana pia hakimiliki ya kitabu hicho ni ya familia ya Mwalimu. Tuiombe pia.

Una maana gani?
 
..hii ni mara ya pili kukisoma kitabu cha Mwalimu Nyerere.

..nadhani kilichotokea kwa Mzee Malecela ni kosa la kiufundi tu, au tactical error, ktk kuhakikisha hoja ya Tanganyika inashindwa.

..Mwalimu angekuwa wa msaada mkubwa zaidi kama angekwenda kwenye chanzo cha matatizo ya huu Muungano wetu.

NB:

..kwa upande wangu nadhani wabunge 55 walikuwa wamekerwa na vitendo vya rushwa vilivyokuwa vikiendekezwa na utawala wa Raisi Mwinyi. rushwa na hujuma zile wakati mwingine zilionekana kama ni za Wazanzibari dhidi ya Tanganyika.

..baada ya hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika, kulifuatia hoja nyingine binafsi ya Jenerali Ulimwengu, na Patrick Qorro na zote zilikuwa zimejielekeza ktk masuala ya rushwa na kukosekana kwa maadili ktk utawala wa Raisi Mwinyi.
 
FMES kumbuka hata Historia, kwa mujibu wa Nyerere, inasema kuwa jamii zetu za asili ziliishi kwa misingi ya Kijamaa. Mpaka kesho watu wengi wanasema hiyo siyo kweli. Historia daima inakuwa na mgongano wa tafsiri ndugu yangu, kila mwamba ngoma huvutia kwake ndio maana kuna propaganda sana!
 
Umekisoma? Kwani historia ni nini? Zifuatazo ndizo sura zake - Je, sio Historia hiyo au Propaganda sio Historia au sehemu ya Historia?

Chapter 3: Subjects and Citizens
Chapter 4: Personality and the Conception of the Völkisch State
Chapter 5: Philosophy and Organisation
Chapter 6: The Struggle of the Early Period – the Significance of the Spoken Word
Chapter 7: The Struggle with the Red Front
Chapter 8: The Strong Man Is Mightiest Alone
Chapter 9: Basic Ideas Regarding the Meaning and Organization of the Sturmabteilung
Chapter 10: Federalism as a Mask
Chapter 11: Propaganda and Organization
Chapter 12: The Trade-Union Question
Chapter 13: German Alliance Policy After the War
Chapter 14: Eastern Orientation or Eastern Policy
Chapter 15: The Right of Emergency Defense

Source: http://en.wikipedia.org/wiki/Mein_Kampf
Pia chaweza somwa hapa: http://www.crusader.net/texts/mk/
 
Back
Top Bottom