Jirani anaweza kukufanya uchukie nyumba yako

Jirani anaweza kukufanya uchukie nyumba yako

Kama kichwa cha habari kinavyoeleza z, unaweza kumpata jirani anafuga, inawezekana ikawa kuku, ng’ombe, bata nk.

Mifugo inatoa harufu inayoambatana na inzi, harufu inaweza kukukatisha hamu ya kula na unashindwa kupunga upepo nje ya nyumba yako kwa kero ya inzi pamoja na harufu.

Unapolalamika jirani hakuelewi kwakua ng’ombe wanampatia maziwa na yeye ndiye muuzaji wa maziwa mtaa..

Ukizingatia viwanja vyetu vya uswahilini hivi vya 20x20. Unawaza ningejua nitakutana na haya nisingenunua kiwanja hapa.

Kuku kwanza jogoo anakuamsha ile saa ya usingizi mzito na wala huna safari, kama unashighuli za kufanya unaweza kusema hii ndiyo alarm yako asubuhi.

Kuna jirani alikua anapika mama ntilie, mchana moshi wote unaingia sebuleni kwangu. Nilipomwbia masikitiko yangu alianza kuniimbia nyimbo za vijembe. Ilibidi nipeleke malalamiko yangu kwa kiongozi wa mtaa. Baada ya kupata ujumbe kutoka serikali ya mtaa, amehamisha sehemu ya kupikia lakini sikuhizi hatusalimiani. Nimepata adui mpya.

Hivi ni vituko uswahilini, eh bwana wee (kiitikio). Uswahilini kuna vituko!
By Suma Lee
 
Kuna sehemu nimejenga kuna kanisa,mwanzo halikua na kelele coz walikua bado hawajaingiza umeme,ila toka juzi wameingiza umeme nimeona dalili za kelele...nimepanga kuwambia wakigoma,taenda serikali za mtaa,nisiposaidiwa taenda NEMC kushitaki,napo nisipofanikiwa taenda mahakamani kuomba tafsiri ya kisheria,maana siwezi vumilia upuuzi wa makelele.

Kuna wenzao wa masjid. Walikuwa wakipiga ile swalaa swalaa. Kama fk 40 hivi, kuanzia saa 11 dot mpaka 12 kasoro. Nikaona isiwe shida. Nikauza ile nyumba iliyoko Mfaranyaki. Nikaona isiwe tabu.
Sikuwqpeleka popote kama wewe unavyopanga kufanya. Nikaogopa wasije wakaniloga bure na takibili yao. Maana nasikia somo la kuloga watu wanalipenda sana. Siju hiyo hawakosi masjid
😛
 
Mimi jirani yangu aliniomba tuache sehemu ya njia kati ya plot yangu na yake ili watu wapite, yaani tusizibe njia iliyokuwepo. Yani mimi niache sehemu na yeye aache kwa upande wake kisha papatikane njia.

Basi nikakubali na wakati ninajenga fensi nikaacha eneo kidogo kwa ajili ya njia kama tulivyokubaliana na jirani yangu. Na yeye kwake ilikuwa afanye hivyo hivyo, ila sasa cha kushangaza akajenga fensi yake moja kwa moja mpaka akaunganisha na plot yangu yaani kile kipande changu cha ardhi nilichokiacha kama njia akakifanya ni part ya plot yake.. kikawa kipo ndani ya fensi yake.

nilimuwakia hajaamini nikamwambia vunja ukuta wako uishie kwenye mpaka wako, yaani kila mtu abaki kwenye eneo lake. Nikasema nitaweka bustani kwenye fensi kwa nje kwenye eneo langu alilochukua.. Hii siku nilikasirika sana

Akaitisha kikao akaomba msamaha nikaamua kupotelezea tu, hawa wenzetu wachaga ukiwa nae jirani chukua tahadhari ya eneo lako mapema

sasa hivi sitaki mazoea naye kabisa zaidi ya salamu tu, infact ni kama mwizi aliyeiba eneo langu kisha baadae akajidai kuomba msamaha

Kwa akina meku ni kawaida sana. Kukuibia mpaka.
 
Naona mnawasahau walokole wa kugeuza nyumba kuwa kanisa,...waumini watatu,.spika zakutosha,...🙄🙄🤔🤒🤒
 
Kama kichwa cha habari kinavyoeleza z, unaweza kumpata jirani anafuga, inawezekana ikawa kuku, ng’ombe, bata nk.

Mifugo inatoa harufu inayoambatana na inzi, harufu inaweza kukukatisha hamu ya kula na unashindwa kupunga upepo nje ya nyumba yako kwa kero ya inzi pamoja na harufu.

Unapolalamika jirani hakuelewi kwakua ng’ombe wanampatia maziwa na yeye ndiye muuzaji wa maziwa mtaa..

Ukizingatia viwanja vyetu vya uswahilini hivi vya 20x20. Unawaza ningejua nitakutana na haya nisingenunua kiwanja hapa.

Kuku kwanza jogoo anakuamsha ile saa ya usingizi mzito na wala huna safari, kama unashighuli za kufanya unaweza kusema hii ndiyo alarm yako asubuhi.

Kuna jirani alikua anapika mama ntilie, mchana moshi wote unaingia sebuleni kwangu. Nilipomwbia masikitiko yangu alianza kuniimbia nyimbo za vijembe. Ilibidi nipeleke malalamiko yangu kwa kiongozi wa mtaa. Baada ya kupata ujumbe kutoka serikali ya mtaa, amehamisha sehemu ya kupikia lakini sikuhizi hatusalimiani. Nimepata adui mpya.
Mifugo inafaa kuwekwa nje ya makazi,shida ni ujuaji wa miji, unakuta umeanzisha eneo,baada ya muda eneo Hilo linajaa na Wewe ndio hapo pakufugia.
 
Ukienda kujenga lazima ufanye uchunguzi kama msikiti au kanisa lipo sehem gani,mfugaji wa kama yupo karibu yani inshort zunguma mit 200 tokea apo
 
Back
Top Bottom