Jirani anaweza kukufanya uchukie nyumba yako

Jirani anaweza kukufanya uchukie nyumba yako

Jirani yangu kachukua mchanga nilinunua kajenga banda la kuku..., hapo bado sijamaliza ujenzi..., inatia hasira sana
 
Mi jirani yangu amejenga choo mpakani kabisa na kamaliza,ubaya unakuja pale maji ya kuoga na na mikojo inatiririkia kwangu na nimemwambia ila kilichotokea sio kurekebisha ila ni kununiana na huu ni mwaka wa nne.

huyo mchukulie hatua serikali za mtaa, kila mtu ajitosheleze kwenye eneo lake bila kuingilina. Hiko choo ama atatafuta pa kupeleka maji au atakivunja, its none of your business

Kiutaratibu unapojenga nyumba unatakiwa uwe makini kiasi kwamba hata maji ya kwenye bati lako yasimwagikie kwenye kiwanja cha jirani yako..
 
Jirani yangu kachukua mchanga nilinunua kajenga banda la kuku..., hapo bado sijamaliza ujenzi..., inatia hasira sana

Alikuomba? kama hajakuomba mwambie alipie anachukuaje bila kuomba?
 
Mimi jirani yangu aliniomba tuache sehemu ya njia kati ya plot yangu na yake ili watu wapite, yaani tusizibe njia iliyokuwepo. Yani mimi niache sehemu na yeye aache kwa upande wake kisha papatikane njia.

Basi nikakubali na wakati ninajenga fensi nikaacha eneo kidogo kwa ajili ya njia kama tulivyokubaliana na jirani yangu. Na yeye kwake ilikuwa afanye hivyo hivyo, ila sasa cha kushangaza akajenga fensi yake moja kwa moja mpaka akaunganisha na plot yangu yaani kile kipande changu cha ardhi nilichokiacha kama njia akakifanya ni part ya plot yake.. kikawa kipo ndani ya fensi yake.

nilimuwakia hajaamini nikamwambia vunja ukuta wako uishie kwenye mpaka wako, yaani kila mtu abaki kwenye eneo lake. Nikasema nitaweka bustani kwenye fensi kwa nje kwenye eneo langu alilochukua.. Hii siku nilikasirika sana

Akaitisha kikao akaomba msamaha nikaamua kupotelezea tu, hawa wenzetu wachaga ukiwa nae jirani chukua tahadhari ya eneo lako mapema

sasa hivi sitaki mazoea naye kabisa zaidi ya salamu tu, infact ni kama mwizi aliyeiba eneo langu kisha baadae akajidai kuomba msamaha
 
Hivi kufuga kuku nayo ni kitu hatari kiasi hicho ?

kwanza ufugaji wa kuku hasa wa mayai unaleta sana nyoka, nyoka wanafata mayai ya kuku. dada yangu alikuwa anafuga kuku wengi wa biashara na karibu kila wiki alikuwa anaua nyoka bandani kwake, yani kila mara nyoka wanaingia kula mayai.

kwa hivyo ukiwa jirani na mfuga kuku jiandae na wewe kutembelewa na nyoka nyumbani kwako.
 
Akitoa hao mifugo--anamkodishia mtu wa kanisa.
Kanisa la mabati na spika mbili kubwa.
Utahama mwenyewe!

hahaha wakati natafuta plot nilipata kiwanja sehemu nzuri sana ila baada ya nyumba 2 kuna kanisa kuubwa la kilokole ikifika saa 10 jioni tu waanza kuimba, nikapiga hesabu nikaona hapa hapana sitainjoi nyumba yangu nikaacha kununua ile plot
 
kwanza ufugaji wa kuku hasa wa mayai unaleta sana nyoka, nyoka wanafata mayai ya kuku. dada yangu alikuwa anafuga kuku wengi wa biashara na karibu kila wiki alikuwa anaua nyoka bandani kwake, yani kila mara nyoka wanaingia kula mayai.

kwa hivyo ukiwa jirani na mfuga kuku jiandae na wewe kutembelewa na nyoka nyumbani kwako.
Hii naisikia kwako chief
 
Alikuomba? kama hajakuomba mwambie alipie anachukuaje bila kuomba?
Kwa kweli hakuomba.., mbaya zaidi ni kuwa yeye alimaliza ujenzi wa nyumba mimi bado najitafuta kumaliza.., Jirani mwingine nae alichukuwa matofali yangu akajengea choo kisa alikuwa na sherehe kwaio akapita na tofali zangu ili wageni wake wasipate shida kujisaidia
 
Ha ha ha haaaa hivi na tulio kwenye nyumba za kupanga nao tuna majirani? Any way mimi mpangaji mwenzangu alikuwa kero kwangu kama ndio jiran basi ndiye huyo huyo.
Picha linaanza ana miaka 31 na ana watoto watano. Kinachotokea huduma muhim kwa familia hatoi chai ikipikwa sukari inawekwa kiasi kwamba chai ikiwa inaingia tumboni ndio unajua kuwa ilikuwa na sukari.
Uji ukikorogwa ni marufuk kuweka sukari anatia chumvi.
Samaki akinunua bichwa lote lake pekee yake watoto watajua wenyewe na kwa kuwa ni msabato anapitia humo humo kuwanyima familia baadhi ya huduma.
Shughuli kwa majirani watot wake wte wanajua ratiba ya majirani kula ha ha haaa ukitenga tu timu ya watoto wanne hao hapo kasoro mkubwa tu ndio anajitambia maana mkubwa yupo drs la pili.
Kumbuka watoto ni malaika maana huwezi wanyima chakula ila kero na lawama zinarudi kwa mzazi hasa wa kiume ni Nyau saana yule mwamba
😀😀😀

😀😃😄
 
Kuna sehemu nimejenga kuna kanisa,mwanzo halikua na kelele coz walikua bado hawajaingiza umeme,ila toka juzi wameingiza umeme nimeona dalili za kelele...nimepanga kuwambia wakigoma,taenda serikali za mtaa,nisiposaidiwa taenda NEMC kushitaki,napo nisipofanikiwa taenda mahakamani kuomba tafsiri ya kisheria,maana siwezi vumilia upuuzi wa makelele.
 
Mimi jirani yangu kafuga mbuzi weengi kinoma usiku kucha mibeberu yanapiga show full mikelele bandani
nashukuru ganja inanisaidia!
 
Back
Top Bottom