Jirani anazalisha K Vant feki na kuziingiza sokoni, nimripoti wapi?

Jirani anazalisha K Vant feki na kuziingiza sokoni, nimripoti wapi?

Status
Not open for further replies.
Ni nyumba jirani na yangu lakini huyu ni mpangaji. Usiku kucha ni kelele za kiwanda chake feki cha kuzalisha KVant feki na kuzijaza kwenye chupa za KVant.

Ni kazi inayofanyika usiku tu. Nimripoti wapi haramia huyu maana naamini vinywaji hivyo feki vinaathiri wanywaji huko nje kwani havina ubora sahihi.

Nipo Kigamboni.
Mind your business
 
Mambo kama hayo yapo mengi sana Nchi zetu hizi za dunia ya tatu

Na serikali zetu zinapoteza mapato mengi sana kupitia viwanda bubu, magendo na maeneo mengine mengi ajabu.

Alishawahi kulipotiwa mtu mwenye kiwanda bubu cha mikate mtaani kwetu
Taarifa ya mtoaji hazikulindwa ulizuka ugomvi mkubwa sana.

Sasa mkuu wasiwasi wangu hakikisha kwanza unapoenda kulipoti usalama wa taarifa yako
 
Ni nyumba jirani na yangu lakini huyu ni mpangaji. Usiku kucha ni kelele za kiwanda chake feki cha kuzalisha KVant feki na kuzijaza kwenye chupa za KVant.

Ni kazi inayofanyika usiku tu. Nimripoti wapi haramia huyu maana naamini vinywaji hivyo feki vinaathiri wanywaji huko nje kwani havina ubora sahihi.

Nipo Kigamboni.
Hao wapuuzi wanaharibu sana bidhaa za watu kwani wanaingiza pombe feki mtaani na matokeo yake zinaua figo za wanywaji.
Naomba umchunguze vizuri inawezekana anatengeneza vinywaji vya aina nyingi ikiwepo SmartGin maarufu kisungura .
Ukigundua anatengeneza na Smart Gin please usisite kuwasiliana na uongozi
 
Ndio maana nami ningependa kuwapa taarifa wenye kiwanda moja kwa moja na sio kwa Mjumbe sijui Polisi NO. Kuwapa taarifa hao hawakawii kunichoma kwa hawa wahuni kwamba tumeambiwa na jirani yako UKEREWEKWETU kwamba unazalisha vinywaji feki,mwisho wa siku nikajihatarishia maisha yangu
 
Hiii chukua kabisaa ukienda polisi wakipewa chochote kitu watakutaja mapema ukienda kwa balozi akipata ya supu mapema tu anakuchomea na ukumbuke watu wa madili haramu wanakua na tabia za kimafia mafia we nenda kiwanda cha k vant moja kwa moja uokoe figo za walevi hao
 
TBS, wanazo namba za bure. Japo na yenyewe yanakula rushwa tu.

Kama vipi mwache tu, nchi imejaa majizi kila kona. Kila mtu aendelee kuiba tu.
 
Hilo tukio ukiwapa police watamvuna mamilioni wewe hupati hata Senti.
Ukiwapa tbs pia watamvuna mamilioni wewe hupati hata Senti.
Kidogo wape taarifa K vant wataweza kumdhibiti na police lazima watamvuna kidogo.
Huyo kafanya jambo baya sana
Kamripoti TRA hao watamuunganishia na kesi ya uhujumu uchumi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom