Salaam!
Anasimulia jirani.
Ilikuwa jioni ya takriban sasa mbili usiku, mtu huyu alikuwa akitoka nyumbani kwa mamaye mzazi aliyekwenda kumtembelea majira ya sasa kumi jioni.
Alipoaga na kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwake ambapo asingeweza kufika kwa usafiri wa daladala,aliamua kutembea kwa mguu, ingemchukua sasa moja kutoka nyumbani kwa mamaye kwenda kwake.
Akiwa anatembea njiani, alijikuta akiongozana na mama wa makamo mwenye umri unaokadiriwa miaka 40, mama huyu alikuwa anatoka kwenye shughuli zake kuelekea nyumbani kwake. Safari hii ilikuwa ya tahadhari sana maana ilisikika milio ya risasi Katika Barbara ya lami, wao waliamua kutumia njia za Chocho za vumbi Ili kuwa salama.
Walitembea kwa kadri ya nusu sasa, wakiwa njiani, walisikia sauti ikiwaamuru kusimama kutokea pembeni mwa barabara.
Walipogeuka kuangalia pembeni kujua ni nani aongeaye, walimwona askari mmoja aliyevalia sare za kawaida za khaki,akiwa ameambatana na askari wengine wawili walikuwa masked wakiwa wamevaa uniform black na wamebeba bunduki black pia , tofauti na bunduki ya askari wa kwanza aliyevalia khaki mwenye bunduki aina ya Ak 47.
Baada ya kusimama, askari yule wa kuvalia uniform ya khaki aliendelea kutoa amri kuwa pigeni magoti chini, wakatii na kwenda chini. Muda huo walikuwa wakimulikwa na tochi Kali za askari huyo wa kuvaa mavazi ya khaki.
Wakati hayo yakiendelea, askari wenye kuvaa black na kubeba bunduki black hawakuongea chochote zaidi ya kuanza kukoki silaha zao na kuwaelekezea tayari kwa kushoot wakisubiri maelekezo ya askari wa khaki ambaye ndiye alikuwa akiwaelekeza, askari yule mwenye kuvaa mavazi ya khaki alianza kuwaeleza jambo Fulani wakawa wakijadiliana kwa lugha ya kiingereza, ilionekana askari Hawa wavaa black,hawakuwa wakijua kiswahili, na walionekana ni wageni.
Wakiwa Katika kujadiliana, alitokea askari mwingine mwenye kuvaa mavazi ya khaki aliyefika pale na kuuliza wanasubiri Nini kuwashoot watu wale ambao aliwaita waandamanaji!
Askari mmoja wapo kati ya wale wawili wavaa khaki,aliweza kumtambua jirani YANGU na kumuita kwa JINA Shehe......, nawe ulikuwa unaandamana?
Jirani YANGU kumwangalia usoni,akamtambua askari yule aliyemsemesha mwenye kuvaa mavazi ya khaki,kumbe ni jirani yake wa siku nyingi tangu utotoni alipokuwa akiishi jirani na nyumbani kwao ambako ndiko alipokuwa ametoka kumsalimu mamaye.
Askari yule baada ya kumtambua jirani YANGU,alianza kuongea na wale askari special,wanyonya damu waliovalia mavazi ya black na kubeba bunduki black Ili wasitishe zoezi la kushoot.
Askari yule akawaambia simameni, wakasimama na kuwaelekeza watu wale, ( jirani YANGU na mama yule) njia salama ya kupita.
Wakawaambia piteni njia ya pembeni mwa lami, na mkikutana na land cruiser nyeupe, jificheni haraka maana gari Ile ndiyo ilikuwa na watu special kupiga risasi waandamanaji na yeyote wataekutana naye.
Baada ya jirani YANGU kusalimika kuuwawa, ilimchukua zaidi ya wiki nzima akiwa nyumbani kwa hofu aliyokuwa anesabishiwa kwa tukio lile.
Baadae ilikuja kufahamika kuwa, kumbe wale askari waliokuwa kwa mguu ,waliomsimamisha jirani YANGU, walikuwa wameshuka toka ndani ya gari Ile land cruiser nyeupe na kutawanyika mtaani kwenda kufanya uhuni ule.
Jirani YANGU amedai kamwe hawezi kwenda kutoa ushahidi mbeleni ya watu waliochaguliwa na mtuhumiwa namba moja. Nami nimemuunga mkono.
Kiukweli tarehe 29 Hadi 31 December 2025, Giza lilitanda nchini.
Mungu na atusaidie kupata malipo ya vitendo vya UOVU vya askari wale wavaa black na kubeba bunduki black.
Nawasilisha.