Kalpana
JF-Expert Member
- Jun 16, 2017
- 32,603
- 62,269
Kheeee bora ulimrudisha sisy..Heeeeeeeehhh kupita mlangoni na mlango umefungwa? Duuuuuhhhh! Dunia ina mauzauza sio poa mkuu!!
Sasa juzikati nilipata Binti wa kazi kwao walikua walozii nyieeee ๐๐๐๐๐๐!
Ni alikua anatokewa na mauzauza hadi nilimrudisha kwao ghafla tu sikuwaziii na namna!
Eti mtu mmelala ndani Usiku binti yeye anasikia geti kama linagongwa gongwa kwanguvu na chuma muda mwingine kama linatikiswatikiswa ile ya kudisturb mtu alielalaa sasa hapo anayesikia hivo ni yeye tu sasa unamsikia binti anafungua ili aone nani anapigapiga vile yeye anavofungua mlango unamsikia unatoka kumuuliza anafungua kwenda wapi?? kufanya nini?? Anakusimulia anavosikia hapo wewe hata huoni wala kusikia chochote unabaki kutoa macho tu. Siku nyingine anatokewa na watu anawaona wanaelea juu ya kichwa chake mara awaone juu ya dari huko watu wawili wamejifunga mabegani kama mashuka mekundu kichwani hadi usoni wamejipaka maungaunga meupee anakwambia anawaona wanamwita kwa kurudia rudia ' Noela njoooo Noela njoooo Noela njoooo' ivoivo huku kama wanamvuta sasa kuna muda unasikia anaongea nao kama wanabishana hivi kuna siku nivomsikia nikashtuka kutega vizuri sikio nasikia mtu anaongea kwanguvu chumbani kwakee nikaamka kwenda kuangalia ninini anasema tangu alivoenda kulala tu hajasinzia kabisa Hao watu walimtokea wanamuita... mara wabadilike kuwa watu kabisa ambapo aliona kibibi kizee fulani cha kwao ( ni jirani yake) na mbaba wa makamu mara hapohapo wanabadilika kuwa kuku mara ng'ombe mara dude ambalo hata halieleweki hio siku alitoka nje Usiku mlangoni kwake akakuta kisu kina damuu .. hirizi nyeusi na tudawa dawa kama vumbi la mkaa..yeye pekee ndio anaviona Hivo vitu nyie wengine hata hamuoni! baby zu Kalpana
Mi kunq mmoja alikua anaota manyoka nyoka kila.siku akampigia baba yake siku hyo aliweka loud speaker eti baba yake anasema hao ni walinzi wake asiogope watakuja sana tuu...yani chatu nikasema iswe tabu bora arudi tuu kwao