Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida

Kwahiyo na mimi unataka kusema nikitaka kumiliki mabus lazima niloge !?[emoji848][emoji849]
hata sitashangaa ukiachilia mbali buses hata ukiamua kufungua duka tu lazima ukalichawie wateja waje naona kama inatrend now a days, kwamba lazima ukaboost biashara itoke, kuna kipindi ni muda kidogo umepita nilikua namsindikiza mam yangu akapande gari za pangani, nakumbuka tulichelewa mno mana ilikua karibu saa moja za usiku haikua kama sasa gari zi tele, tulikaa sana mpaka mwisho nikamwambia mama kama ikifika had saa mbili hakuna gari turudi tukalale utasafiri asbh, kiasi kidogo ikaja gari iko kama costa ile gari ilikua imepakwa pilau yani kama wamelifutia nje punje za pilau na harufu na hio safari ni either mama afike hio siku au kesho yake mapema sana nilichomuambia ni omba Mungu shoga angu ufike salama panda tu nikahakikisha imeondoka nikajirudia zangu kulala sasa imagine ubwabwa wa nn kwenye costa?? Mungu atusimamie
 
Kwanini?,hebu tuhadithie kidogo mrembo
Sitaki kukumbuka kabisa ile siku yanii mie nilikua Kazini bana sasa usiku wa kuamkia hio siku tulipika Chakula mboga ilikua samaki ikabaki.

Ile asubuhi nivoamka kujiandaa kwenda Job binti wa kazi nikamuachia maelekezo mchana atakata kabegi wamalizie na ile samaki ilobaki usiku wapike na ugali Kwani hio home walibaki yeye na jr tu!

Sasa nipo kazini mida kama ya saa 6 mchana nikaona napigiwa Simu na housegirl wa jirani madam Noela kadondoka yupo jikoni chini anapiga kelele tu Sisi tumeenda kumuangalia tunamuuliza amekuaje hajibu kitu fanya uje haraka!

Kutokana na hayo mauzauza aliyokuwa anatokewa mwanzo kwanza niliogopa sanaaaa akili yangu ikimuwazia Mwanangu tu kuwa nisije kuta kamuua mwanangu yani damu ilinichemkaaa hio siku duhh!

Kazini sio Mbali sana na home nikachukua boda fastaaa chap kufika chakwanza kuulizia Jr yukwapi na kumtafuta huku nimetoa macho balaa!

Kumbe Mtoto alikua zake nje huko anacheza hana hata habari!!
Kuingia ndani namkuta binti sebleni kumuuliza akaanza kunihafithia bana:

Ilikua mida ya saa tano unusu asubuhi alikata kabegi vizuri akaipika vizuri sasa ile ametoa sufuria jikoni kupeleka sehemu ya kutaka kuipakua aiweke kwenye sahani moja kwa moja kwani walikua wanaenda kula muda si mrefu so hakutaka kuiweka kwenye hotpot ndio ilikua mazingaombweee sasa!

Alipeleka kwanza sufuria lakabeji akaliweka hio sehemu vizuri sasa akarudi jikoni kufata samaki pia alikua ameipasha ile kufika anakuta sufuria lenye kabegi alizopika limejaa maji hadi juu na mboga Hizo zikiwemo ikumbukwe hapo ndani alikuepo yeye tu Jr alikua nje huko kwa wenzake anacheza hana hili wala like!! Akajiuliza nani kaweka haya majiii?
 
Sema wadada wa kazi napo ni kumuomba Mungu
 
Mmmmh polee, hivi vitu vipo mm nina rafiki yangu mtoto wake wa kwanza aliempata kwenye harakati za kutafuta maisha ana hizi mambo,na mtoto huwa anamuhadithia kabisa kuwa ni wakala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…