Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida

Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida

Hao ndio binadamu.....hatupendezwi na jambo moja kwa pamoja.....hata katika mafanikio huwa hiv hiv...sio wote watakao kubaliana na hatua unayochukua japo haiwahusu ila watakuandama sana tena ndio wakiona unaenda kufanikiwa.

Kikubwa unapo amua kufanya jambo lako usiwafikirie sana walimwengu ili mradi tu huingilii maisha ya mwingine....kila mtu ana njia yake pekeyake.
Binafsi nampongeza Mwandishi, Mimi siwezi kuandika kama yeye. Naona furaha kuona watu wa namna yake.

Kama Kuna makosa ni kidogo sana. Siwezi kuhukumu mtu, nimejileta mwenyewe kusoma alichoandika .

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
 
Kweli eeehh!!
Halafu wachawi wanapenda sana mimbaaaa ..vitoto vichanga na watoto wa kiumee wakwanzaa wanaina lango wenyewe!!
Hio ya mke wa Steve kuota imenikumbusha kipindi fulani nilikua nalala na mjamzito.... huyo ndugu yanguu...alikua anaota ota anaweweseka sana ndotoni namsikia kama analalamika kama anatoa sauti fulani ambayo nikiyasikiliza vizuri manenoo siyaelewi anatamka maneno gani!
kwakua Kwakua ni mjamzito namuacha alale nisimkatishe usingizi wake heee akiamka namuuliza mbona kuna muda ulikua umelala nilisikia hivi na vilee nayeye anakumbuka anasema alikua anaota na ndotoni aliwaona watu fulani ila walikua wanamfuata kishari Hivi sasa ile kukimbia ili kuepuka kupambana nao ndio akawa kama analalamika kwa sauti kubwaaa ya kuomba msaaada kwangu nilieko pembeni yake yeye anaona kama ananiita kwa nguvu sana ilhali pia anaona sisikii chochote so anakua a anabaki kuhangaika Huku mimi nasikia tu mtu anatoa sauti fulani ila matamshi siyasikii vizuri!
Ungekua unamuamsha
 
Binafsi nampongeza Mwandishi, Mimi siwezi kuandika kama yeye. Naona furaha kuona watu wa namna yake.

Kama Kuna makosa ni kidogo sana. Siwezi kuhukumu mtu, nimejileta mwenyewe kusoma alichoandika .

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
Kweli kabisa mkuu, sisi tunataka burudani mambo ya uhariri hata hayatuhusu
 
Hio sh 50 uloiokota Steve umechukua mikosiiiiiiiii!!
Wachawi/walozi wanapenda sana kutumia pesa za sarafu kwenye shirki zao / maulozi yao
Ilitokea kibibi kizeee au mtu ambae unajua/ kuhisi ni mchawi akakuomba sh 50 ...100 au hata 200 usimpee hio ya coin moja kwa moja mpe Ya note ikiwezekana kubwa kabisa akatafute chenchi mwenyewe akurudishie yeyee!!
Giza lina mauzauza sio poaahhh!!
Dooo
 
Mkuu ongeza japo moja aisee mwanzoni nilijua ile mifurushi big wanakunya ndani wanaenda kumwaga nikachukulia poa maana ilikua ndo zangu kipindi flan chuga maji kisoda bas ile mifuko laini ya zamani ilikoma. Kwangu ilikua kila ukiingia kunanuka puu mbaya sjui nlikua nawaza nn mbaya zaid akija mama yeyo nae anafanya yake tunamix tunavizia mtaa umepoa tunaenda kutupa nje mbali kidogo sitasahau mtego niliowekewa na kunaswa mpk nikahama saa kumi usiku sjui naenda wapi life la kukosa ela mtu unakuwa nusu mwehu
Duuh...! Kumbe duniani kuna watu wanaishi kiajabu,halafu mnasingizia ksbb huna hela. Sasa kujinyea na kutokuwa na hela vinaendana?
 
Duuh...! Kumbe duniani kuna watu wanaishi kiajabu,halafu mnasingizia ksbb huna hela. Sasa kujinyea na kutokuwa na hela vinaendana?
Mkuu ningekua na ela ningenunua maji ya madumu ninye chooni nimwage maji au niamie njiro kwenye maji bwerere mimi nlikua kwa siku nameki elf3 to 5 ninunue maji ya kuoga kunywa kupikia af na ya kumwaga toi burebure no way
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Bigi huyo anatishaaa namambo yake yakutoeleweka ni mchawi au jambaziiii?
Yani mpk sasa hatuelewi kabisa ni tafrani
 
Mtu bundle umenunua mwenyewe kwa hela yako,device ni yako muda ni wako kila kitu ni chako but toka post #180 sasa story ipo post 1K+ wewe bado upo hapa unasoma and still unalalamika kwanini usiachane na hili jambo?

Mnaolalamika kuweni kama mimi tu nimeamua kusoma kujifurahisha as long as simlipi mtu ni bundle langu na muda wangu japo story inachosha kuisubiri.

Jama ikitokea ikaendelea naomba atokee msamaria mwema ani-tag ili niendelee kuburidika na mimi.
 
Kweli Kabisa sis ukiona Mtu anaota inatakiwa unapigapiga hata began ilev kumshtua/ kumuamsha hata mtoto pia
Kweli mpendwa hali hyo huwa inatesa sanaaa ya kuita bila jirani kukusikia...nimeota sana hizo.ndoto pindi mdogo ila kwa sasa zimeishaga..yani upo na mtu jirani hakusikii ila anaona unahangaika tuu...ukiwa unajua unamuamsha maana anaweza fia ndotoni aiseee.
 
Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida – 09



KATIKATI ya usiku mke wangu alianza kuongea mwenyewe, mwanzoni nilidhani ni masikio yangu pengine yanasikia vibaya lakini nilipofungua macho kutazama nilibaini kile nilichokisikia kilikuwa ni kweli, mwanamke huyo alikuwa anaongea akiwa usingizini, maongezi ambayo kwa muda kidogo sikufahamu anachokimaanisha.

Kidogo, nikiwa namtazama na kumskiza, akakurupuka toka usingizini, aliponikuta namtazama akakurupuka tena zaidi kabla ya kutulia. Alikuwa ameparwa na hofu sana, macho ameyatoa akihema. Nilimuuliza ni nini kimemsibu lakini kabla hajaniambia kitu alinyoosha mkono wake kwenye swichi akawasha taa alafu akaniambia kwa kunong’ona, “kuna mtu mlangoni.” Akarudia tena akiwa amenishika mkono, “kuna mtu mlangoni.”

Nikatoka kwenda sebuleni kutazama, niliwasha taa nikaufungua mlango lakini huko sikuona kitu. Nilipogeuza uso kumtazama mke wangu nilimwona akiwa amesimama kwenye mlango wa chumbani ananitazama kwa macho ya hofu, nikamwambia hamna mtu hapa mlangoni wala koridoni kisha nikarejea naye chumbani, huko hakutaka tuzime taa abadan, alisema anaogopa sana.

Aliniambia alisikia mtu mwenye sauti kama ya kwake akiwa anagonga na kubisha hodi vilevile kama alivyokuwa anabisha hodi muda ule kwenye mlango wa BIGI. Alijaribu kuniamsha lakini sikuamka, punde kidogo ndo’ akasikia mlango unafunguliwa sebuleni.

Kwa kumtuliza, nikamwambia hiyo ni ndoto tu na jambo hilo ameliota maana alikuwa akilifikiria sana, cha muhimu apuuzie kisha alale hamna chochote kitakachotokea, kishingo upande akalala lakini akinisisitiza tena nisizime taa. Kama baada ya lisaa hivi akapitiwa na usingizi, lakini hakukucha mpaka asubuhi akawa anashtuka shtuka, si kwa kuota tena bali kwa uoga wake binafsi. Alikuja kulala kwa amani jua lilipomea.

Siku hiyo kama nilivyokuwa nimepanga, nilienda kumwona Tarimo kule hospitali, huko nikakutana na ndugu yuleyule ambaye nilimkuta siku ile kule Mwananyamala, ndugu huyo alikuwa pamoja na mke wa Tarimo, niliongea naye mambo kadha wa kadha kumhusu mgonjwa na nilipoona ni vema nikondoka zangu kurejea nyumbani. Nilipofika, hata sikupoa, nikapata taarifa kuwa mtoto wa Bembela, yule mwanamke mama ntilie, alizidiwa hoi bin taabani akafanya kuwahishwa hospitali ya Massana!

Yule jirani, mwanamke ambaye nilimdhania kuwa ni yeye ndiye alimpa maneno Bembela jana yake, alirejea majira ya jioni akitokea hospitali alipokuwapo na Bembela na mgonjwa akatuambia yale yaliyokuwa yamejiri, mtoto yule aliamka akiwa na homa kali tangu asubuhi na kutwa akilalamika mwili mzima unamuuma. Alimpatia dawa za kutuliza maumivu akidhani atapoa lakini kadiri muda ulivyoenda hakupata nafuu, ikambidi ampigie simu mama yake aje upesi waende hospitali. Maneno mengine aliyoyasema niliamini ni chumvi tu ya kwetu waswahili, sikuyatilia sana maanani mpaka pale kesho yake asubuhi mimi mwenyewe nilipopata kupitia hospitali ya Massana baada ya kupata upenyo mdogo kazini majira ya mchana, muda wa lunch. Hospitali hiyo haikuwa mbali na eneo ninapofanyia kazi, yaani hapo GOIG, hivyo haikuniwia ugumu kufika upesi kisha nikaendelea na mambo yangu mengine.

Hapo hospitali nilimkuta Bembela akiwa na mwanae kitandani anampatia chakula. Mtoto huyo alionekana hana nguvu, amevalia khanga aliyoifunga shingoni na uso wake unaugulia maumivu. Mwanamke yule, yaani Bembela, akanieleza ya kwamba usiku wa kuamkia siku ile mwanaye alikuwa anasumbuka sana na ndotoni, na mara mbili alikurupuka akisema kuna mtu anampiga, mtu asiyemwona, kwa maelezo hayo akaamini mwanaye anaota yale yaliyotokea siku ile.

Asubuhi ilipowasili, aliondoka kwenda kuendelea na shughuli zake za kawaida, hakuona kama jambo lile ni ishu kubwa, lakini ajabu majira ya baadae ndipo alipigiwa simu na shoga yake akaambiwa hali ya mtoto imekuwa mbaya, aliporejea akamkuta mtoto amevimba na baadhi ya sehemu zake za mwili zimevilia damu, kama haitoshi homa yake ilipanda sana na tena anatapika damu mara kwa mara. Jambo hilo likamshtua maana mpaka anaondoka ile asubuhi hakupata kuona kama kuna cha ajabu kumhusu mwanaye.

Mtoto alipimwa ikabainika ana majeraha ya ndani, lakini pia maumivu yake makali, kwa mujibu wa daktari, hayakusababishwa na kitu kingine isipokuwa kipigo, swala hilo likafanya daktari amtake Bembela kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi kwanza kwa kuhofia huenda mtoto yule alikuwa ni mhanga wa ukatili wa majumbani, naye akafanya hivyo lakini akiwa tayari ameshamkabidhi mtoto kwa ajili ya huduma. Lakini ajabu ni kwamba sisi sote tulikuwa tunafahamu kilichomtokea mtoto yule, tukio lililomtokea halikuwa cha kiasi hicho cha kumtia hali mbaya namna ile, hayo mambo ya kuvilia na kutapika damu yalikuwa yanashangaza sana.

Nilipomaliza kumwona mgonjwa nikaenda nyumbani na huko nikaeleza kwa wengine hali ya mtoto. Kesho yake, jumatatu, asubuhi nikiwa kazini nikapigiwa simu kuwa mtoto yule amefariki usiku, hivyo nyumbani kuna msiba. Jambo hilo likanishtua sana kwani sikutegemea kama lingetokea haraka hivyo, ndio mtoto yule alikuwa anaumwa lakini sikudhani kwa jinsi nilivyomwona siku ile basi angelifariki usiku wake. Wenyeji wa yale maeneo watakuwa wanaukumbuka msiba huu vema.

Msiba huo ulipelekwa nyumbani kwa wakina Bembela, maeneo ya Mbezi Mwisho, huko kwa wazazi wake. Wapangaji wote walihidhuria huo msiba isipokuwa bwana BIGI na familia yake. Hakuna aliyepata kuwaona mwanzo mpaka mwisho wa shughuli hiyo. Baadae, kwasababu ya kutokuwepo ama kushinda nyumbani muda mrefu wa siku, nilikuja kupata taarifa kuwa maafisa wa polisi walifika pale nyumbani kuwahoji baadhi ya watu kuhusu kesi ile ya mtoto. Walihitaji kuonana na bwana BIGI na familia yake lakini hakuwapo hata mmoja, wakaomba mawasiliano ya hao watu lakini hamna hata mtu mmoja alokuwa nayo, wengine walidhani mimi ningelikuwa nayo kwasababu ya yale madhali ya kipindi kile kuja naye na pikipiki lakini hata mimi sikuwahi kuwa nayo, basi wakachukua namba ya mwenye nyumba kisha wakajiondokea.

Baadae mimi nikiwa nipo nyumbani naambiwa hayo yaliyotokea, ndipo simu yangu inaita akipiga mwenye nyumba. Bwana huyo akaniambia ametafutwa na polisi anatakiwa atoe taarifa za bwana BIGI na ubaya ni kwamba yeye hana chochote kwani hakuwahi kupeana makaratasi yoyote na yule bwana, aliniuliza kama ninayo namba yake nikamwambia sina, mimi nilimshafikishia BIGI ule ujumbe wake kuhusu mkataba muda mrefu tu hivyo sikufahamu kama muda wote huo hawakupata kuonana, basi yule bwana aka-panick sana, alihofia atawaambia nini polisi wakamwelewa na vipi kama BIGI hatopatikana tena?

Zilipita siku kadhaa, kama mbili au tatu hivi, baadae nikaja kusikia tetesi kwa watu kuwa mtoto yule marehemu kabla ya kukumbana na kifo chake aliendelea kulalamika akiwa pale hospitali ya kwamba maumivu yanamzidi na kumzidi. Ni kana kwamba aliendelea kupigwa na kupigwa lakini alokuwa anampiga haonekani. Zoezi hilo lilidumu kwa muda kidogo tu akapoteza maisha.

Tetesi hizo zilisambaa sana pale nyumbani na zikajenga hofu kubwa kumhusu bwana BIGI, wengine wakarejea kauli ya Bembela akiwa pale mlangoni mwa BIGI kuwa kauli hiyo imemponza, na wengine wakasema bwana huyo hatokuja kurejea tena pale alipokuwa anaishi, kwamba ametoroka baada ya kufanya tukio.

Basi bwana, kama mchezo hivi, siku hiyo nikiwa natoka kazini na pikipiki, nikamwona bwana BIGI akiwa anashuka na begi lake mgongoni mwelekeo wake ni kule nyumbani. Sikujua kwamba ndo alikuwa anarejea nyumbani kutoka safari au alikuwapo tu hapa mjini, na kama anarejea kutoka safari mbona alikuwapo mwenyewe ingali pale nyumbani kwa maelezo ya majirani na polisi familia yake nzima haikuwapo? Au waliongea pasi na uhakika?

Nilimsalimu na kumtaka apande tumalizie safari yetu lakini alikataa, kabla ya kuachana nikamwambia anatafutwa sana na mwenye nyumba kuhusu swala lile la mkataba basi afanye namna wawasiliane, akaniambia anajua kila kitu, na anajua pia polisi wanamhitaji.

Baada ya hapo sikupata kuonana na bwana huyo kwa muda wa siku kadhaa, nilikuja kusikia polisi walionana naye na pia walimwona mtoto wake, yule mwenye utindio, lakini hamna cha maana na kikubwa kilichojiri. Kwa maneno ya yule shoga yake Bembela , maneno ambayo alipata kumwambia mke wangu, Bembela alikuwa amesafiri kwenda mkoani kuonana na mtaalam. Mwanamke huyo , yaani Bembela, hakupata kuwa sawa tena tangu tukio lile la mwanae na aliamini kabisa lina mkono wa mtu.

Lakini mbali na mwanamke huyo, hata mimi mwenyewe mke wangu hakupata kuwa sawa tena tangu siku ile. Hali ambayo ilikuja kupelekea hata baadae mimba yake kuharibika, hili ntakuja kulieleza hapo mbele, lakini punde kama siku chache mbele ya lile tukio, mke wangu alianza kuona siku zake pamoja na kuwa mjamzito.



***
Huyu BIGI ni very mysterious and dangerious man.
 
Kweli mpendwa hali hyo huwa inatesa sanaaa ya kuita bila jirani kukusikia...nimeota sana hizo.ndoto pindi mdogo ila kwa sasa zimeishaga..yani upo na mtu jirani hakusikii ila anaona unahangaika tuu...ukiwa unajua unamuamsha maana anaweza fia ndotoni aiseee.
Kumbe!! Lol asante sis! Ndio ile mtu amelala mzima kuamka keshakata roho zamanii na alikua haumwi wala nini!!
Hii ilimtokea jirani mmoja mpaka leo kifo cha mwanae hakijulikani sababu!!

Mama mtoto na mwanae Walikua wameenda ukweni kusalimia ilikua weekend mtoto alikua na 2 years. Walienda ijumaa wakasalimia sasa Jumapili mida kama ya saa 9 alasiri wakawa wanataka Kurudi mama mtu keshamuogesha mtoto kamvalisha kabisa mtoto akawa anasinzia sinzia mama mtu akaona ngoja kwanza amuache alale walau hata nusu saa tu akiamka ndio waanze Safari ya kurudi kwa mume sasa kwakua hapakua mbali sana! akamlaza mtoto akasinzia vizuri tu.

Sasa mama mtu subiri mtoto aamke amka nawewee subirii weee subiri naweeee mtoto haamki... mama mtu si ndio kwenda atake kumuamsha ili waanze Safari ya kurudi sasa Lahaulaaahhh tikisa tikisa nawewe mtoto kimyaa hata hashtuki alikua amemlaza kifudifudi si ndio kumgeuza mtoto anashagaa mtoto kakakamaa keshakata kauli zamaniiiiii mwili umeshapoaa hadi kuanza kuwa mweusi tiii! Ndio kuwahi kumnyanyua haraka hapoo Binti mwenyewe alikua mdogo hana uzoefu mtoto mwili ushakua mzitooo badae alishafariki zamanii na alikua mzima kabisa wa afya! Mama mtu anasema alipomyanyua alikua haja kubwa sasa mtoto ni alikabwa alikuaje haijulikani!!!
 
Back
Top Bottom