Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida

Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida

Familia yako uliyohama nayo sijaisoma popote kwenye story. Hukuwa na mke na mtoto?
Yule Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida ~ 05




Tangu ujenzi wa uzio ulipoanza niliongeza zaidi umakini wangu kwenye kutazama usalama wa nje ya nyumba kwasababu geti lile dogo lililokuwa hapo sasa halikuwapo tena kwenye kingo za ukuta, badala yake lilikuwa linaegeshwa na kuondolewa, hivyo mtu asipoliegesha basi ndo tunakaa wazi kama behewa kitu ambacho kwangu kilikuwa na hatari sana maana usafiri wangu ulikuwa unakaa karibu na geti hilo. Yeye mwenye nyumba alisema anataka kuleta geti jingine, lile la zamani lisirudishwe, lakini kwa siku tatu mfululizo hakuleta geti hilo, hata mafundi wenyewe walikuwa wanalalamika hawajalipwa pesa zao, mara kadhaa walikuwa wanasaidiwa kupewa chakula na wapangaji.

Sijawahi kujua kwanini wenye nyumba wanakuwaga wagumu mno kufanya marekebisho ya mapango yao, yani mikono yao imezoea kupokea na kuchuma tu, kwenye kutoa wanaona kama vile hawastahili, yaani wanaumiaaaa.

Turudi kwenye usiku ule. Baada ya BIGI kupotelea kule kizani nilijazwa na hamu ya kwenda kutazama kule korongoni anapoenda. Nilijiuliza mara mbilimbili nikaona haitakuwa vema kwani nikitoka pale na kuacha geti dogo wazi kiasi kile nitakuwa nimejiweka matatani kiusalama, haswa wa pale nyumbani, hivyo nikaona kheri nibakie palepale kungoja lakini kwasababu sikutaka bwana yule anione kuwa namtazama nilienda zangu maeneo ya bafuni, huko kulikuwa na kiza sababu ya taa haikuwashwa, nikajibanza hapo kiubavu kutazama geti dogo.

Yani kama sekunde nne tu yule bwana akawa ametokea getini, Ilibakia kidogo tu angeniona maana ilikuwa ni upesi mno kiasi cha kunishangaza, alipoingia alitazama huku na kule, huku na kule, alafu akaufuata mlango wa grill lakini alipoufikia mlango huo, kabla hajaingia, alifanya jambo ambalo lilinifanya nihisi huenda aliniona. Alisimama hapo akitazama upande ule wa bafuni kwa kama dakika tatu pasipo kupepesa, moyo wangu ukawa unaenda mbio sana. Sikumchukulia bwana yule kama mtu wa kawaida tena bali kama dubwana lililopo mbele yangu katika mawindo yake.

Nilitulia kadiri nilivyoweza, alipotosheka akaingia ndani na kisha akaufunga mlango ule wa grill kwa funguo, kitu ambacho siku zingine huwa hakifanyi, mimi nikaachwa pale nje nisijue nini cha kufanya.

Nilikaa nikawaza niugonge mlango wa grill? Hapana, nikiugonga maana yake yule bwana atajua nilikuwa nje namfuatilia nami sikutaka kumthibitishia hilo, basi nikaona cha kufanya niendee dirisha la chumba changu, japo lipo juu, nihangaike nalo kuwaita waliomo ndani wapate kunisaidia, wakati nashuka ngazi mara nilisikia sauti ya kiume ikifoka:

"Wewe nani?"

Nilishtuka sana. Niligeuka kutazama sauti inatokea wapi nikabaini ni kwenye dirisha la yule jirani yangu mwenye duka, hapo dirishani alikuwa amesimama mtu aliyeshikilia pazia kutazama nje. Kabla sijajibu kitu, mtu huyo alinitambua akasema,

"Aah kumbe ni wewe, kaka! Vipi tena huko nje mida hii?"

Nikamdanganya nilienda maliwatoni lakini kwa bahati mbaya kurudi nikaukuta mlango umefungwa, basi kwa kunisaidia alitoka ndani kwake kuja kunifungulia.

Alinijulia hali na kidogo kwa kama dakika mbili hivi tukawa na mazungumzo mafupi. Aliniambia alisikia mtu anaufungua mlango wa grill kwenda nje, akaniuliza nilikuwa ni mimi?

Kabla sijamjibu nilitazama kwanza kwenye korido kisha nikamweleza kwa sauti yangu ya chini kuwa aliyeufungua mlango huo ni BIGI, mimi nilitoka hapo baadae kwenda maliwatoni ndipo nikaukuta tayari ameshaufunga. Sikutaka kumwambia kuhusu yale ya korongoni wala ya kujificha bafuni.

Nilipomjibu hayo naye alinieleza kuwa muda wote huo alikuwa akimshuku bwana huyo kuwa ndo' anaacha mlango wazi lakini hakuwa na uhakika, zaidi aliniambia anahisi kuna jambo haliko sawa kumhusu bwana yule kwani kuna mambo ambayo amemshuhudia yakamwacha mdomo wazi.

Hakutaka kunieleza mengi kwasababu wasaa haukuwa unaruhusu, tulikubaliana tutakapoonana na tukiwa na muda basi tutayajenga. Aliniaga akaenda zake na mimi nikaenda zangu.

Wiki iliyokuja nilipata safari ya siku tatu ya kwenda Tabora, wilaya ya Igunga, kwasababu ya msiba wa mmoja wa jamaa yetu wa kazini ambaye alifiwa na mama yake mzazi. Safari hiyo ndefu ilikomea kwenye kijiji fulani ambacho sikikumbuki jina ila ninachokumbuka nyumba ambayo tulifikia haikuwa mbali sana na shule moja ya sekondari inayoitwa Mwamashiga, huko hapakuwa na mtandao wa simu wala umeme, ni nyumba chache chache ndo' zilikuwa na taa zinazotumia nishati ya jua kwahiyo sehemu kubwa ilikuwa kizani nyakati za usiku.

Muda wote nikiwa huko sikuweza kutumia simu yangu kwaajili ya mawasiliano, simu iligeuka kuwa 'toy' la kuchezea game ama kukokotoa hesabu. Nilikuja kupata mawasiliano siku tulipotoka huko kijijini njiani kuelekea Igunga mjini, kitu kilichonifanya nikajua kuwa mtandao umerudi ni ujumbe ulioingia kwenye simu yangu; ujumbe kutoka Airtel kuwa kifurushi changu kimeisha, baada ya ujumbe huo nilipokea ujumbe mwingine toka kwenye namba ngeni ukisema (nanukuu):

"Kaka ukirudi nyumbani fanya tuonane upesi, nimejaribu kukutafuta kwa simu sikupati. Tarimo."

Nilijiuliza ujumbe huo umetokea wapi lakini baada ya punde ya kuwaza na kuunganisha matukio nilipata jibu langu, aliyetuma ujumbe ule alikuwa ni jirani yangu mwenye duka, yeye ndiye Tarimo na mara ya mwisho mimi kuonana naye alitaka tuongee tukipata nafasi.

Nilijaribu kumtafuta hewani pasipo mafanikio, si kwamba alikuwa hapatikani, lah, mimi sikuwa na salio. Nilicheki pia kwenye AirtelMoney lakini napo hola, hapakuwa na kiasi cha kunitosha kumpigia, ilinilazimu niwe mpole mpaka nitakapopata sehemu rafiki ya kununua vocha.

Wakati huo nilikuwa nawaza sana kuwa ni nini ambacho Tarimo alikuwa anataka kuniambia kwa dharura hiyo lakini pia nikajikuta nayakumbuka na kuyawaza yale ya kule nyumbani, kwa muda huo nikawa katika ulimwengu wangu wa pekee, nilikaa na watu lakini nilijihisi niko mwenyewe kabisa.

Tulipofika Igunga mjini gari lilisimama ili tupate mahitaji muhimu mathalani maji maana kuna watu walishindwa kunywa maji ya kule kijijini, maji yao ni ya kuchimba chini na kuyahifadhi kwenye ndoo, maji hayo ukiyatazama kwa haraka unaweza dhani ni chai nyepesi ya maziwa na ladha yake si kama maji uloyazoea, hapo ndipo na mimi nilipata mwanya wa kununua vocha nikapiga simu kwa Tarimo huku nikiomba apokee upesi maana simu yangu ilikuwa taabani kwa kuishiwa na charge, muda wote ambao nilikuwa kule sikuwahi kuicharge na kama matumizi yangekuwa makubwa basi bila shaka ingeshalizima muda mrefu sana.

Kidogo Tarimo alipokea simu nikamsalimu na kumweleza kuwa nimepata ujumbe wake na nilikuwa mbali mahali ambapo mtandao unasumbua, basi akanipa pole na kunitaka nikifika Dar Es Salaam nionane naye mara moja kwani kuna jambo alitaka kunishirikisha kabla hajachukua hatua zingine. Nakumbuka kauli yake moja akisema,

"Kaka, tufanye juu chini huyu jamaa aondoke hapa nyumbani kama tunataka kuwa salama."

Basi kwasababu tulishapangiana kuonana, nilikata simu na kuwatafuta watu wangu wengine wa karibu ili nipate kuwajulia hali maana sikuwa hewani kwa kitambo kidogo na sikutaka simu izime kabla sijateta nao, baada ya hapo haikupita muda mrefu simu ikazima nikabaki mpweke, wengi niliokuwa nao ndani ya gari sikuwa nafahamiana nao zaidi tu ya mfiwa na majamaa wawili wa kutoka kazini, nao walikuwa wameketi mbali na mimi.

Sikudumu muda mrefu nikapitiwa na usingizi mzito kwelikweli kwani kwa muda niliokuwa kule kijijini sikupata kulala vema, mahali pa kulala hapakuwapo, ni mara chache ndo' ningejibanza sebuleni majira ya mchana pale kwenye kochi nikalala huku nimeshika tama, usingizi wa mlinzi, hivyo nilivyotulia kwenye kiti cha basi na huku upepo unanipuliza sikuweza kuvumilia kabisa, macho yalinishinda vita.

Nilifika Dar majira ya jioni, kabla ya kunyookea nyumbani nilipitia kazini ili niuchukue usafiri wangu ambao niliuacha huko kwasababu ni salama zaidi kuliko kule nyumbani ambapo niliacha bado ujenzi unaendelea, baada ya hapo nilinyookea nyumbani na nilichokifanya baada ya kufika tu nilimpigia simu bwana Tarimo kumwambia kwamba nimewasili, bwana huyo akaniambia yuko mbali kidogo kuna mtu alimpelekea mzigo maeneo ya Mbweni lakini akitoka huko atanipigia na kunipa muafaka, basi nikangoja, wakati huo nikautumia kwenye mambo yangu mengine ya hapa na pale.

Mpaka inafikia saa nne usiku bwana Tarimo hakuwa amenitafuta, si kwa ujumbe wala kupiga, na mimi sikuona haja ya kumtafuta maana aliniambia atanijuza yeye hivyo nikatulia kungoja nikiamini atakuwa ametingwa na mambo yake ya kikazi, muda ukaenda na kuenda.

Kwenye majira ya saa tano ya usiku, nikiwa nimepumzika sebuleni, ndipo nilisikia watu wakiwa wanazungumzazungumza huko nje, haswa wanawake, katika mtindo wa zogo fulani hivi na mimi sikuwa nayasikia maneno yao wanayoyasema.

Lakini ghafla katika zogo hilo nilisikia ukunga uuuuuuuuuwiiiiii! Uuuuuuuuuwiii! Nikapata mshtuko. Kidogo nikiwa hapo, bado sijafanya kitu, mlango uligongwa na nilipoufungua nilikutana na mwanamke mmoja ambaye anakaa kwenye zile nyumba za nje, mwanamke huyo aliniambia kuwa amepata habari toka kwa mke wa yule jirani yangu wa dukani, yaani mke wa bwana Tarimo, ya kwamba bwana huyo amepata ajali mbaya ya pikipiki maeneo ya Kunduchi, mbuyuni, kwenye mataa.

Nikaduwaa.
 
Kisa kataja bodaboda? Uandishi wao wala haufanani. Na ana sababu ya gani ya kuja na ID tofauti?
Wengi wasichokijua ni kwamba huyu SteveMollel ndiye UMUGHAKA ni mtu mmoja ID tofauti, hata ukifuatilia aina ya uandishi nadhani ndiyo maana alipomaliza tu kule kwenye utajiri wa Ally Mpemba akalianzisha huku!
 
Nimejiuliza Mambo mengi Sana
1. Kwann yule Bibi alikuambia vile? Mazingira ya hiyo zahanati hapana nyumba ya karibu kiasi kwamba ushindwe kumkuta njiani kwa muda mchache uliyopishana nae baada ya wewe kuruhusiwa kurudi nyumbani na Big
Kimazingira ya kawaida huwezi kwenda hospitali private bila pesa na endapo ukiwa mgonjwa Sana unahudumiwa baadae unalipia na kwa umri wake usiku ule kwenda hospitali peke yake ni changamoto

2. Kwanini mke wa big akukate jicho kiasi kile? Kwenye kikao

3. Mwili wa mke wa big kuwa wabaridi Sana mithili ya maiti

4. Ulijificha chooni big akahisi Kuna mtu means machale yalimcheza


Haya tupo twasubiri muendelezo
Mimi nahis mke wa big ni mwanaume kajifanya kama mwanamke
 
Back
Top Bottom