Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida

Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida

Story inaukakasi kidogo?


Mwanzo wa story ulisema una mke na familia kubwa

Ila ndani ya story mkeo kaja kuonekana sehemu ya 7

Vipi apo brother
Boss sasa anawazungumzia vipi kama part yao ilikuwa haijafika....kwenye picha sio lazima star family yake ionekane au aonekane akifanya vitu vifuatavyo
Kula, Kuoga, sex, kulala na kama havina sababu ya kuonekana...
 
Hamna mahali nilisema nina familia kubwa, bali nilisema nilihamia Goba kukidhi ukubwa wa familia maana kule Makonde nilikuwa nakaa kibachelor, kule Goba nikawa nakaa na mwanamke na mtoto.

Na sababu iliyofanya huyo mwanamke nisimtaje ni kwasababu hakukuwa na tukio lolote la kunifanya nimtaje mpaka pale sehemu yake ndani ya matukio ilipowadia, na nikasema kwanini muda wote huo haikuwa hivyo.

Ni kheri tukatulia na kusoma mpaka mwisho, every stone will be unturned.
Mkuu endelea..Maswali yaende darasani..
 
Huyu msimuliaji ana vitu vifuatavyo:-
1. Ana kiasi kikubwa sana cha umbea, kuacha uaingizi saa tisa usiku kukaa dirishani kuangalia nani ataingia.
2. Ulinzi ungemfaa zaidi kuliko kazi anayofanya kwa sasa, haiwezekani ukeshe usiku kucha kulinda nyumba kwa niaba ya wapangaji wote ambao hawajakuomba.
 
Hamna mahali nilisema nina familia kubwa, bali nilisema nilihamia Goba kukidhi ukubwa wa familia maana kule Makonde nilikuwa nakaa kibachelor, kule Goba nikawa nakaa na mwanamke na mtoto.

Na sababu iliyofanya huyo mwanamke nisimtaje ni kwasababu hakukuwa na tukio lolote la kunifanya nimtaje mpaka pale sehemu yake ndani ya matukio ilipowadia, na nikasema kwanini muda wote huo haikuwa hivyo.

Ni kheri tukatulia na kusoma mpaka mwisho, every stone will be unturned.
[emoji58][emoji58][emoji58]
Screenshot_20230206_211832.jpg
 
Hii nayo kali sana tunapaswa tuimalize
 
Huyu msimuliaji ana vitu vifuatavyo:-
1. Ana kiasi kikubwa sana cha umbea, kuacha uaingizi saa tisa usiku kukaa dirishani kuangalia nani ataingia.
2. Ulinzi ungemfaa zaidi kuliko kazi anayofanya kwa sasa, haiwezekani ukeshe usiku kucha kulinda nyumba kwa niaba ya wapangaji wote ambao hawajakuomba.
Nimeeleza kwa kina lifestyle yangu na changamoto niliyokuwa nayo kwenye upande wa usafiri wangu na pia udhaifu wa makazi tulokuwapo.

Ungeweza kulala fofofo huku umeacha chombo ambacho hakipo locked na mahali pana kadhia ya vibaka mara kwa mara? Huku miundombinu ikiwa so rafiki?

Anyways mkuu, tunatofautiana maisha, akili na tabia.

Napokea vyote maua na mawe.
 
Nimeeleza kwa kina lifestyle yangu na changamoto niliyokuwa nayo kwenye upande wa usafiri wangu na pia udhaifu wa makazi tulokuwapo.

Ungeweza kulala fofofo huku umeacha chombo ambacho hakipo locked na mahali pana kadhia ya vibaka mara kwa mara? Huku miundombinu ikiwa so rafiki?

Anyways mkuu, tunatofautiana maisha, akili na tabia.

Napokea vyote maua na mawe.
Mkuu tuendelee achana na hawa wasaga sumu.
 
Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida - 02

Siku tatu baada ya tukio lile la mwizi, wakati nikiwa narudi nyumbani tokea kazini majira ya jioni ya saa moja, nikakutana na bwana BIGI akiwa amebebelea begi mgongoni. Bwana huyo alikuwa anashuka na njia ya kuelekea nyumbani, nikamsalimu na kumpakia tupate kumalizia safari yetu.

Kama ilivyo ada, nilimpomshusha akasema "Asante" lakini kabla hajaondoka nikampatia ule ujumbe wa mwenye nyumba kuhusu mkataba, akatikisa kichwa chake na kwenda zake ndani. Hakutia neno.

Siku hiyo katika majira ya saa saba hivi usiku, nikiwa bado nipo sebuleni natazama televisheni kabla sijaenda zangu kulala, nakumbuka nilikuwa nikirudia kutazama moja ya filamu yangu pendwa isiyoisha utamu 'TRIANGLE' maana sikuwa na filamu mpya ya kuitazama, ghafla nikasikia sauti ya kike ikipiga kelele fupi! Nikashtuka na kuanza kuhukumu masikio yangu kama yamesikia kitu sahihi ama ni mang'amng'amu ya filamu.

Nikazima sauti ya televisheni kisha nikatega masikio vema, sikusikia kitu tena, kwa kama dakika tatu hivi kukawa kimya kama ilivyokuwa hapo awali, ila nilipotaka kuendelea na filamu yangu tu mara nikasikia mlango unafunguliwa, si mlango wangu bali wa jirani, alafu kidogo mlango wangu ukagongwa - ngo ngo ngo, nikauliza nani? Sikujibiwa, nikasogea na kuufungua mlango, sikuwa na shaka sana maana niliusikia mlango wa jirani ukifunguliwa hivyo niliamini atakuwa ni jirani tu.

Nilipofungua mlango nikakutana uso kwa uso na BIGI, uso wake unachuruza jasho, amevalia bukta na kaushi tu, akaniomba samahani kunisumbua usiku huo mkubwa kisha akanitaka nimsaidie kumpeleka mkewe hospitali kwani hali yake si nzuri, hapo nikaikumbuka ile sauti niliyoisikia, ina maana ilikuwa ni ya mkewe au? Lakini mwanamke huyo si bubu? Ama ...

Hakukuwa na muda wa kutafakari maana hali yenyewe ni ya dharura, nikarejea ndani kuvaa nguo kamili kisha nikaufungua mlango na kuendea pikipiki nje kuwangoja wahusika, kidogo akatokea BIGI akiwa amembeba mke wake kama mtoto mkononi, nikafungua geti dogo na kutoa pikipiki nje, nao walipotoka nikaurejeshea ule mlango mdogo kisha tukaanza safari ya kwenda hospitali, mgonjwa aliketi katikati yetu, BIGI amekaa mwishoni kabisa kwenye chuma kwasababu ya mwili wake mpana, ukichanganya na uzito wa watu wawili niliowabeba nyuma basi nikawiwa ugumu sana kumudu pikipiki kwenye barabara ile ya vumbi na makorongokorongo, yani mpaka kuifikia barabara ya lami nimetota mgongo mzima kwa jasho, sitamaniki!

Muda wote huo nilikuwa nikimsihi tu BIGI amshikilie mgonjwa vizuri na asiweke miguu yake chini akaharibu balansi ya chombo.

Basi niliposhika lami na kutembea mwendo wa kama dakika hivi, ndo' nikaanza kuhisi vema na mwili wangu, kule korongoni akili haikuwa imetulia kabisaa, mawazo yote yalikuwa ardhini tunapokanyaga, ila hapa lami nikaanza kuhisi baridi fulani hivi, si baridi la upepo, la hasha, bali baridi la mgonjwa!

Mara kadhaa mwanamke yule aliponiegamia nilihisi baridi mgongoni mwangu, nguo niliyokuwa nimevaa ilikuwa ni shati la kawaida tu sema kifuani ndo nilijiziba na kizibao cha ngozi kinachozuia upepo kuniingia ndani, hivyo nilikuwa na uwezo wa kuhisi vizuri tu na mgongo wangu pasi na shida, na mwanamke yule alikuwa ni wa baridi.

Sijawahi kuona mgonjwa anakuwa wa baridi kiasi kile, kwa nijuavyo mimi mgonjwa akiwa anaumwa, tuseme homa, joto la mwili wake hupanda sana, sikuwahi kujua kuna mambo ya joto kushuka kiasi hiki lakini kwasababu sijawahi kuwauguza wagonjwa wote duniani nikaona hilo nalo litakuwa ni jipya kwangu kujifunza.

Baada ya muda wa dakika kumi na tano hivi barabarani, kwa kufuata maelekezo ya BIGI, tukawa tumefika maeneo ya Kawe, Ukwamani. Upande ule wa kulia wa soko, kwa mbele kidogo kuna kibao cha dispensary kinachoonyeshea njia ya vumbi, tukashika njia hiyo mpaka kutokea kwenye zahanati fulani hivi kubwa, hapo BIGI akambeba mgonjwa wake na kunyookea naye mapokezi, mimi nikahangaika kidogo na pa kupakia pikipiki mpaka nilipokuja kusogea mapokezini wao wakawa wameshaenda kuonana na daktari, basi nikaketi kwenye benchi kungoja.

Hapo kwa benchi alikuwepo mama mmoja aliyejitanda kanga, amejiinamia simwoni uso wake, tulikuwa mimi na yeye tu hapo kwa benchi, hakukuwa na mtu mwingine, mazingira ya hapo yalikuwa yametulia mno, ungeweza kusikia kila mbu anayekatiza huku na kule kusaka ridhiki yake, nikamsalimu mama yule, "za saa hizi?" Akanyanyua uso wake kunitazama, alikuwa ni mwanamke mzee, macho yake mekundu kwa kulia. Aliitikia salamu yangu kwa sauti ya chini, "salama" kisha akaunamisha tena uso wake kama nilivyomkuta.

Nikatulia kidogo nikimtazama, bila shaka alikuwa na kubwa linalomsibu, nikashindwa kuvumilia nikamuuliza, "mama kulikoni?" Akiwa amejiinamia vile, akaniambia anajiskia vibaya sana, amekuja hapo kupima na ameambiwa ana maradhi lakini ameshindwa kumudu kununua dawa, mwili wake ni dhaifu na usiku ule alishindwa kabisa kupata hata usingizi wa kuibia mpaka alione jua la asubuhi.

Nikashikwa na imani sana. Mzee kama yule majira yale ya usiku mkubwa yuko kwenye benchi la zahanati tena akiwa hajui hatma yake, kweli dunia haina huruma! Nikajisachi na kutoa noti ya alfu kumi ambayo nilikuwa nimepanga kuiwekea mafuta kwenye pikipiki baadae nikienda kazini, nikampatia mama yule na kumsihi akachukue dawa na kiasi itakayobakia atapata chakula, mama huyo akanishukuru sana sana, kwakweli sikuwahi kuona mtu akishukuru kiasi kile maishani mwangu, laiti ungeliona alivyokuwa ananitazama ungepata picha halisi namaanisha nini hapa, alinyanyuka na kuendea taratibu duka la dawa la hapo zahanati, duka hilo lilikuwa linatazamana na sisi, akachukua dawa na kunirejea tena kuniaga.

Nikamuuliza, "Utaenda na usiku huu?" Akanijibu, "kwangu si mbali, ni hapo tu nyuma." Akaenda zake. Alipiga kama hatua nne hivi za kichovu, akageuka ghafla na kuniuliza, "yule bwana mnene aliyekuwa amebebelea mwanamke, umekuja naye?" Nikamjibu ndio, akaniuliza tena, "ni wateja ama watu unaowafahamu?"

Nikabaini mama huyo atakuwa aliniona nilipoingia eneo hilo na pikipiki hivyo akadhani huenda mimi ni bodaboda, kabla sijamjibu, akaongezea, "kama ni wateja tu wa barabarani, ondoka upesi achana nao."

Sikuelewa anamaanisha nini kwa kuniambia hivyo, nilimwambia wale ni majirani zangu, si wateja, basi akanitazama kwa macho ambayo niliyatafsiri kama mtu anayewazua jambo kichwani lakini hakusema kitu, nikamuuliza, "kwanini umesema hivyo?" Hakunijibu, akageuka na kuendelea na safari yake, nikatamani kumfuata kumuuliza lakini punde bwana BIGI alijiri akinifuata, alikuwa anatokea kule chumba cha daktari, akaniambia mkewe ameshaanza matibabu hivyo ni vema mimi nikarudi nyumbani kwani wao watabaki hapo usiku mzima.

Kwasababu hiyo, nikamuaga na kwenda zangu kuifuata pikipiki nijiondokee, njiani nikatazama huku na kule kama ntamwona mwanamke yule mzee niliyemsadia lakini sikufanikiwa, ni mataa tu na giza za vichochoro, basi nikalazimika kuamini atakuwa ameshafika nyumbani kwake kwani kwa maelezo yake nyumbani ni karibu tu na pale.

Nikawasha pikipiki na kuondoka, njiani nikiwaza mambo haya ambayo yametoka kujiri kuanzia nyumbani mpaka kule zahanati, mawazo hayo yakanifanya nikaona safari imekuwa fupi sana, yani kitambo kidogo tu nikawa tayari nipo mbele ya geti dogo la kuingia nyumbani.

Nikalifungua geti hilo na kuingia ndani, nilipoufunga mlango wa grill wa nyumba kubwa na kushika korido kwenda kwangu nikasikia sauti ya watu wanaongea, nikashtuka, sauti hiyo inatokea wapi? Niliposkiza vizuri nikabaini inatokea kwenye mlango wa chumba anachokaa BIGI, nikasogea karibu hapo mlangoni na kuskiza kwa umakini, nikagundua ni sauti ya televisheni sio watu wa kawaida, bila shaka yule mtoto wao ndo' alikuwa anatazama, nikajiendea zangu ndani kupumzika.

Zilipita kama siku kama nne hivi bila ya kuwa na makutano na familia hiyo, siku ya tano sasa kama sijakosea, katika majira ya usiku wa saa tisa nikiwa chumbani napambana kuupata usingizi, nikasikia kama kuna mtu huko nje, nikajua ni mwizi sasa ametutembelea tena, basi taratibu nikatoka kitandani na kuchungulia dirishani, dirisha la kule magharibi sikuona kitu ila dirisha hili la kaskazini nikamwona mtu ameketi kibarazani, mtu huyo ameketi akitulia tuli kama mbuyu wa nyikani! Nikastaajabu, huyu sio mwizi, lakini ni nani na anafanya nini kibarazani majira yale?

Niliendelea kutazama, taratibu taratibu nikajiridhisha kuwa mtu yule alikuwa ni mke wa BIGI, kumbe alikuwa amesharejea kutoka hospitali, lakini anafanya nini pale usiku mkubwa? Nilijaribu kukumbuka kama nilisikia mtu akiufungua mlango mkubwa kutoka nje lakini sikukumbuka kabisa, kidogo nikasikia mlango unafunguliwa, mlango wa ndani, alafu kidogo mlango wa grill ukachokonolewa na funguo, tulikuwa tunaweka funguo ya grill kwa juu, mlango ukalia kaaakakaaa alafu ukafunguka, huo mlango ndio ulikuwa unalia hivyo ukifunguliwa, akatoka BIGI akiwa anatembea upesi, akamnyakua mwanamke yule kama kipanga na kifaranga cha kuku, wakaingia ndani!

Kama dakika tu, nikamsikia sauti ya mtoto analia...
Ukivuta hisia, INA mafunzo
 
Back
Top Bottom