Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida

Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida

Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida – 09



KATIKATI ya usiku mke wangu alianza kuongea mwenyewe, mwanzoni nilidhani ni masikio yangu pengine yanasikia vibaya lakini nilipofungua macho kutazama nilibaini kile nilichokisikia kilikuwa ni kweli, mwanamke huyo alikuwa anaongea akiwa usingizini, maongezi ambayo kwa muda kidogo sikufahamu anachokimaanisha.

Kidogo, nikiwa namtazama na kumskiza, akakurupuka toka usingizini, aliponikuta namtazama akakurupuka tena zaidi kabla ya kutulia. Alikuwa ameparwa na hofu sana, macho ameyatoa akihema. Nilimuuliza ni nini kimemsibu lakini kabla hajaniambia kitu alinyoosha mkono wake kwenye swichi akawasha taa alafu akaniambia kwa kunong’ona, “kuna mtu mlangoni.” Akarudia tena akiwa amenishika mkono, “kuna mtu mlangoni.”

Nikatoka kwenda sebuleni kutazama, niliwasha taa nikaufungua mlango lakini huko sikuona kitu. Nilipogeuza uso kumtazama mke wangu nilimwona akiwa amesimama kwenye mlango wa chumbani ananitazama kwa macho ya hofu, nikamwambia hamna mtu hapa mlangoni wala koridoni kisha nikarejea naye chumbani, huko hakutaka tuzime taa abadan, alisema anaogopa sana.

Aliniambia alisikia mtu mwenye sauti kama ya kwake akiwa anagonga na kubisha hodi vilevile kama alivyokuwa anabisha hodi muda ule kwenye mlango wa BIGI. Alijaribu kuniamsha lakini sikuamka, punde kidogo ndo’ akasikia mlango unafunguliwa sebuleni.

Kwa kumtuliza, nikamwambia hiyo ni ndoto tu na jambo hilo ameliota maana alikuwa akilifikiria sana, cha muhimu apuuzie kisha alale hamna chochote kitakachotokea, kishingo upande akalala lakini akinisisitiza tena nisizime taa. Kama baada ya lisaa hivi akapitiwa na usingizi, lakini hakukucha mpaka asubuhi akawa anashtuka shtuka, si kwa kuota tena bali kwa uoga wake binafsi. Alikuja kulala kwa amani jua lilipomea.

Siku hiyo kama nilivyokuwa nimepanga, nilienda kumwona Tarimo kule hospitali, huko nikakutana na ndugu yuleyule ambaye nilimkuta siku ile kule Mwananyamala, ndugu huyo alikuwa pamoja na mke wa Tarimo, niliongea naye mambo kadha wa kadha kumhusu mgonjwa na nilipoona ni vema nikondoka zangu kurejea nyumbani. Nilipofika, hata sikupoa, nikapata taarifa kuwa mtoto wa Bembela, yule mwanamke mama ntilie, alizidiwa hoi bin taabani akafanya kuwahishwa hospitali ya Massana!

Yule jirani, mwanamke ambaye nilimdhania kuwa ni yeye ndiye alimpa maneno Bembela jana yake, alirejea majira ya jioni akitokea hospitali alipokuwapo na Bembela na mgonjwa akatuambia yale yaliyokuwa yamejiri, mtoto yule aliamka akiwa na homa kali tangu asubuhi na kutwa akilalamika mwili mzima unamuuma. Alimpatia dawa za kutuliza maumivu akidhani atapoa lakini kadiri muda ulivyoenda hakupata nafuu, ikambidi ampigie simu mama yake aje upesi waende hospitali. Maneno mengine aliyoyasema niliamini ni chumvi tu ya kwetu waswahili, sikuyatilia sana maanani mpaka pale kesho yake asubuhi mimi mwenyewe nilipopata kupitia hospitali ya Massana baada ya kupata upenyo mdogo kazini majira ya mchana, muda wa lunch. Hospitali hiyo haikuwa mbali na eneo ninapofanyia kazi, yaani hapo GOIG, hivyo haikuniwia ugumu kufika upesi kisha nikaendelea na mambo yangu mengine.

Hapo hospitali nilimkuta Bembela akiwa na mwanae kitandani anampatia chakula. Mtoto huyo alionekana hana nguvu, amevalia khanga aliyoifunga shingoni na uso wake unaugulia maumivu. Mwanamke yule, yaani Bembela, akanieleza ya kwamba usiku wa kuamkia siku ile mwanaye alikuwa anasumbuka sana na ndotoni, na mara mbili alikurupuka akisema kuna mtu anampiga, mtu asiyemwona, kwa maelezo hayo akaamini mwanaye anaota yale yaliyotokea siku ile.

Asubuhi ilipowasili, aliondoka kwenda kuendelea na shughuli zake za kawaida, hakuona kama jambo lile ni ishu kubwa, lakini ajabu majira ya baadae ndipo alipigiwa simu na shoga yake akaambiwa hali ya mtoto imekuwa mbaya, aliporejea akamkuta mtoto amevimba na baadhi ya sehemu zake za mwili zimevilia damu, kama haitoshi homa yake ilipanda sana na tena anatapika damu mara kwa mara. Jambo hilo likamshtua maana mpaka anaondoka ile asubuhi hakupata kuona kama kuna cha ajabu kumhusu mwanaye.

Mtoto alipimwa ikabainika ana majeraha ya ndani, lakini pia maumivu yake makali, kwa mujibu wa daktari, hayakusababishwa na kitu kingine isipokuwa kipigo, swala hilo likafanya daktari amtake Bembela kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi kwanza kwa kuhofia huenda mtoto yule alikuwa ni mhanga wa ukatili wa majumbani, naye akafanya hivyo lakini akiwa tayari ameshamkabidhi mtoto kwa ajili ya huduma. Lakini ajabu ni kwamba sisi sote tulikuwa tunafahamu kilichomtokea mtoto yule, tukio lililomtokea halikuwa cha kiasi hicho cha kumtia hali mbaya namna ile, hayo mambo ya kuvilia na kutapika damu yalikuwa yanashangaza sana.

Nilipomaliza kumwona mgonjwa nikaenda nyumbani na huko nikaeleza kwa wengine hali ya mtoto. Kesho yake, jumatatu, asubuhi nikiwa kazini nikapigiwa simu kuwa mtoto yule amefariki usiku, hivyo nyumbani kuna msiba. Jambo hilo likanishtua sana kwani sikutegemea kama lingetokea haraka hivyo, ndio mtoto yule alikuwa anaumwa lakini sikudhani kwa jinsi nilivyomwona siku ile basi angelifariki usiku wake. Wenyeji wa yale maeneo watakuwa wanaukumbuka msiba huu vema.

Msiba huo ulipelekwa nyumbani kwa wakina Bembela, maeneo ya Mbezi Mwisho, huko kwa wazazi wake. Wapangaji wote walihidhuria huo msiba isipokuwa bwana BIGI na familia yake. Hakuna aliyepata kuwaona mwanzo mpaka mwisho wa shughuli hiyo. Baadae, kwasababu ya kutokuwepo ama kushinda nyumbani muda mrefu wa siku, nilikuja kupata taarifa kuwa maafisa wa polisi walifika pale nyumbani kuwahoji baadhi ya watu kuhusu kesi ile ya mtoto. Walihitaji kuonana na bwana BIGI na familia yake lakini hakuwapo hata mmoja, wakaomba mawasiliano ya hao watu lakini hamna hata mtu mmoja alokuwa nayo, wengine walidhani mimi ningelikuwa nayo kwasababu ya yale madhali ya kipindi kile kuja naye na pikipiki lakini hata mimi sikuwahi kuwa nayo, basi wakachukua namba ya mwenye nyumba kisha wakajiondokea.

Baadae mimi nikiwa nipo nyumbani naambiwa hayo yaliyotokea, ndipo simu yangu inaita akipiga mwenye nyumba. Bwana huyo akaniambia ametafutwa na polisi anatakiwa atoe taarifa za bwana BIGI na ubaya ni kwamba yeye hana chochote kwani hakuwahi kupeana makaratasi yoyote na yule bwana, aliniuliza kama ninayo namba yake nikamwambia sina, mimi nilimshafikishia BIGI ule ujumbe wake kuhusu mkataba muda mrefu tu hivyo sikufahamu kama muda wote huo hawakupata kuonana, basi yule bwana aka-panick sana, alihofia atawaambia nini polisi wakamwelewa na vipi kama BIGI hatopatikana tena?

Zilipita siku kadhaa, kama mbili au tatu hivi, baadae nikaja kusikia tetesi kwa watu kuwa mtoto yule marehemu kabla ya kukumbana na kifo chake aliendelea kulalamika akiwa pale hospitali ya kwamba maumivu yanamzidi na kumzidi. Ni kana kwamba aliendelea kupigwa na kupigwa lakini alokuwa anampiga haonekani. Zoezi hilo lilidumu kwa muda kidogo tu akapoteza maisha.

Tetesi hizo zilisambaa sana pale nyumbani na zikajenga hofu kubwa kumhusu bwana BIGI, wengine wakarejea kauli ya Bembela akiwa pale mlangoni mwa BIGI kuwa kauli hiyo imemponza, na wengine wakasema bwana huyo hatokuja kurejea tena pale alipokuwa anaishi, kwamba ametoroka baada ya kufanya tukio.

Basi bwana, kama mchezo hivi, siku hiyo nikiwa natoka kazini na pikipiki, nikamwona bwana BIGI akiwa anashuka na begi lake mgongoni mwelekeo wake ni kule nyumbani. Sikujua kwamba ndo alikuwa anarejea nyumbani kutoka safari au alikuwapo tu hapa mjini, na kama anarejea kutoka safari mbona alikuwapo mwenyewe ingali pale nyumbani kwa maelezo ya majirani na polisi familia yake nzima haikuwapo? Au waliongea pasi na uhakika?

Nilimsalimu na kumtaka apande tumalizie safari yetu lakini alikataa, kabla ya kuachana nikamwambia anatafutwa sana na mwenye nyumba kuhusu swala lile la mkataba basi afanye namna wawasiliane, akaniambia anajua kila kitu, na anajua pia polisi wanamhitaji.

Baada ya hapo sikupata kuonana na bwana huyo kwa muda wa siku kadhaa, nilikuja kusikia polisi walionana naye na pia walimwona mtoto wake, yule mwenye utindio, lakini hamna cha maana na kikubwa kilichojiri. Kwa maneno ya yule shoga yake Bembela , maneno ambayo alipata kumwambia mke wangu, Bembela alikuwa amesafiri kwenda mkoani kuonana na mtaalam. Mwanamke huyo , yaani Bembela, hakupata kuwa sawa tena tangu tukio lile la mwanae na aliamini kabisa lina mkono wa mtu.

Lakini mbali na mwanamke huyo, hata mimi mwenyewe mke wangu hakupata kuwa sawa tena tangu siku ile. Hali ambayo ilikuja kupelekea hata baadae mimba yake kuharibika, hili ntakuja kulieleza hapo mbele, lakini punde kama siku chache mbele ya lile tukio, mke wangu alianza kuona siku zake pamoja na kuwa mjamzito.



***
@Demi
 
story ya huyu jamaa haina tofauti na series za kihindi. mara nyingi huwa na visa vingi ambavyo ni useless ktk movie. lengo lao ni kurefusha urefu wa series ili kuwe na episode nyingi.
Ikiwemo na vikota😀😀
 
Ndugu Mollel, nimepitia posts nyingi za chalenji humu na nimegundua wengi wao hawana nia mbayaukiangalia kwa jichola 3.
Nakushauri uwe na moyo wa kiume na uhesabu kama changamoto za kukufanya uwe bora zaidi katika utunzi au usimuliaji wako.

Mwisho; kuwa mwanaume usiyeondolewa kwenye lengo kirahisi
Tatizo Masai wanahasira Sana,..usije kuta kapandisha Mori huko 😄😄,...kwanza nnawasiwasi Masai gani anakunywa mbege ilifaa anywe loshoroo akishushia ugoro!!...sheer!
 
Simulizi nzuri ila burudani zaidi inatoka kwenye malumbano ya wachangiaji. Kwa kweli ukiwa na stress pitia tu JF zitqisha
Wanalumbana na kupeana majibu wenyewe[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Kuna mahali msimuliaji alisema ni story tu, lakini kwa mtoto aliyekufa anasema "nadhani watu mlioishi eneo hilo mnakumbuka vizuri kifo cha mtoto huyo kilivyoleta utata" Labda story ina ukweli kiasi na kuongezewa chumvi nyingi ili inoge.
Hujawahi kucheki movie halafu kuna sehemu unawasikia wakisema ...kama movie vile!!...
 
  • Thanks
Reactions: ARV
Tatizo Masai wanahasira Sana,..usije kuta kapandisha Mori huko 😄😄,...kwanza nnawasiwasi Masai gani anakunywa mbege ilifaa anywe loshoroo akishushia ugoro!!...sheer!
Hujashangaa masai anajua simulia tena kwa kiswahili kilicho nyooka!?!.. haya twende pamoja ......
 
Ilikua balaa mkuu nilikimbizwa nikarushiwa fuko nlilotupa mgongoni likanibwaga nikachezea kichapo raia wamechukua simu saa mkanda viatu soks kila kitu na ela kwenye suruali wanalazmisha nikawape laki mbili home au nile mavi yangu tukaenda mpk home nimevaa niko hoi mpk atm enzi hizo karibu na fire kwa mguu wanatimba nyuma mie mbele nikawapa chao wanasema nenda nikianza kwenda wananilamba fimbo aloo nlitoka nduki magetoni kusanya kila kitu vingine nimeacha nikaanza kuhaha usiku kutafta nyumba kummbuka sina simu nimevimba kote aisee zilikua siku tatu chungu ule mtaa sijapita tena
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]litro umenifanya nicheke sana
 
Tatizo Masai wanahasira Sana,..usije kuta kapandisha Mori huko 😄😄,...kwanza nnawasiwasi Masai gani anakunywa mbege ilifaa anywe loshoroo akishushia ugoro!!...sheer!
Kuna maasai wa porini...njere na kuna masai wa mjini yaani maasai ma masai🤣🤣🤣
Masai wa mjini ameendelea sana amejenga kisasa mno, mfugaji wa zero grazing, na ni matajiri...ukoo wa Mollel ndio ukoo tajiri zaidi kuliko masai na maasai wengine kama akina Laiza, ma kivuyo.

Hivyo usimchukulie poa kivile🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom