Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida

Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida

Najua vile arosto inavotesa

Lakini tujitahidi kuvumilia dear maana nae ni binadamu ratiba yake inabana kama alivosema

Ukipata arosto njoo kule chitchat tuchit chatike kuvuta muda huku tukisubiri episode inayofata

Usikubali kua na makasiriko madogo madogo kama haya mpenzi msomaji[emoji9]

Sent from my vivo 1906 using JamiiForums mobile app
Namna hii hata kama hasira iko juu itashuka. Hongera mpenzi ubarikiwe sana.

Nimedandia treni kwa mbele [emoji1787][emoji1787]
 
Sasa hapa ndio kizungumkuti, aliyefariki ni bwana BIGI, Mkewe au Mwanae? Cz lazima dawa ya Bembela itakua imetingisha hii familia ya walozi kwakweli. Lakini Steve hivi hamna hata siku uliwaza ufanye dua kwa Mwenyezi Mungu au hata utafute maji au chumvi ukomeshe hii familia? au hizi level ni nyingine kabisa mzee?
Hapo Shangazi wa bembela kwaheri Big sio ntu wa mchezo
 
Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida - 02

Siku tatu baada ya tukio lile la mwizi, wakati nikiwa narudi nyumbani tokea kazini majira ya jioni ya saa moja, nikakutana na bwana BIGI akiwa amebebelea begi mgongoni. Bwana huyo alikuwa anashuka na njia ya kuelekea nyumbani, nikamsalimu na kumpakia tupate kumalizia safari yetu.

Kama ilivyo ada, nilimpomshusha akasema "Asante" lakini kabla hajaondoka nikampatia ule ujumbe wa mwenye nyumba kuhusu mkataba, akatikisa kichwa chake na kwenda zake ndani. Hakutia neno.

Siku hiyo katika majira ya saa saba hivi usiku, nikiwa bado nipo sebuleni natazama televisheni kabla sijaenda zangu kulala, nakumbuka nilikuwa nikirudia kutazama moja ya filamu yangu pendwa isiyoisha utamu 'TRIANGLE' maana sikuwa na filamu mpya ya kuitazama, ghafla nikasikia sauti ya kike ikipiga kelele fupi! Nikashtuka na kuanza kuhukumu masikio yangu kama yamesikia kitu sahihi ama ni mang'amng'amu ya filamu.

Nikazima sauti ya televisheni kisha nikatega masikio vema, sikusikia kitu tena, kwa kama dakika tatu hivi kukawa kimya kama ilivyokuwa hapo awali, ila nilipotaka kuendelea na filamu yangu tu mara nikasikia mlango unafunguliwa, si mlango wangu bali wa jirani, alafu kidogo mlango wangu ukagongwa - ngo ngo ngo, nikauliza nani? Sikujibiwa, nikasogea na kuufungua mlango, sikuwa na shaka sana maana niliusikia mlango wa jirani ukifunguliwa hivyo niliamini atakuwa ni jirani tu.

Nilipofungua mlango nikakutana uso kwa uso na BIGI, uso wake unachuruza jasho, amevalia bukta na kaushi tu, akaniomba samahani kunisumbua usiku huo mkubwa kisha akanitaka nimsaidie kumpeleka mkewe hospitali kwani hali yake si nzuri, hapo nikaikumbuka ile sauti niliyoisikia, ina maana ilikuwa ni ya mkewe au? Lakini mwanamke huyo si bubu? Ama ...

Hakukuwa na muda wa kutafakari maana hali yenyewe ni ya dharura, nikarejea ndani kuvaa nguo kamili kisha nikaufungua mlango na kuendea pikipiki nje kuwangoja wahusika, kidogo akatokea BIGI akiwa amembeba mke wake kama mtoto mkononi, nikafungua geti dogo na kutoa pikipiki nje, nao walipotoka nikaurejeshea ule mlango mdogo kisha tukaanza safari ya kwenda hospitali, mgonjwa aliketi katikati yetu, BIGI amekaa mwishoni kabisa kwenye chuma kwasababu ya mwili wake mpana, ukichanganya na uzito wa watu wawili niliowabeba nyuma basi nikawiwa ugumu sana kumudu pikipiki kwenye barabara ile ya vumbi na makorongokorongo, yani mpaka kuifikia barabara ya lami nimetota mgongo mzima kwa jasho, sitamaniki!

Muda wote huo nilikuwa nikimsihi tu BIGI amshikilie mgonjwa vizuri na asiweke miguu yake chini akaharibu balansi ya chombo.

Basi niliposhika lami na kutembea mwendo wa kama dakika hivi, ndo' nikaanza kuhisi vema na mwili wangu, kule korongoni akili haikuwa imetulia kabisaa, mawazo yote yalikuwa ardhini tunapokanyaga, ila hapa lami nikaanza kuhisi baridi fulani hivi, si baridi la upepo, la hasha, bali baridi la mgonjwa!

Mara kadhaa mwanamke yule aliponiegamia nilihisi baridi mgongoni mwangu, nguo niliyokuwa nimevaa ilikuwa ni shati la kawaida tu sema kifuani ndo nilijiziba na kizibao cha ngozi kinachozuia upepo kuniingia ndani, hivyo nilikuwa na uwezo wa kuhisi vizuri tu na mgongo wangu pasi na shida, na mwanamke yule alikuwa ni wa baridi.

Sijawahi kuona mgonjwa anakuwa wa baridi kiasi kile, kwa nijuavyo mimi mgonjwa akiwa anaumwa, tuseme homa, joto la mwili wake hupanda sana, sikuwahi kujua kuna mambo ya joto kushuka kiasi hiki lakini kwasababu sijawahi kuwauguza wagonjwa wote duniani nikaona hilo nalo litakuwa ni jipya kwangu kujifunza.

Baada ya muda wa dakika kumi na tano hivi barabarani, kwa kufuata maelekezo ya BIGI, tukawa tumefika maeneo ya Kawe, Ukwamani. Upande ule wa kulia wa soko, kwa mbele kidogo kuna kibao cha dispensary kinachoonyeshea njia ya vumbi, tukashika njia hiyo mpaka kutokea kwenye zahanati fulani hivi kubwa, hapo BIGI akambeba mgonjwa wake na kunyookea naye mapokezi, mimi nikahangaika kidogo na pa kupakia pikipiki mpaka nilipokuja kusogea mapokezini wao wakawa wameshaenda kuonana na daktari, basi nikaketi kwenye benchi kungoja.

Hapo kwa benchi alikuwepo mama mmoja aliyejitanda kanga, amejiinamia simwoni uso wake, tulikuwa mimi na yeye tu hapo kwa benchi, hakukuwa na mtu mwingine, mazingira ya hapo yalikuwa yametulia mno, ungeweza kusikia kila mbu anayekatiza huku na kule kusaka ridhiki yake, nikamsalimu mama yule, "za saa hizi?" Akanyanyua uso wake kunitazama, alikuwa ni mwanamke mzee, macho yake mekundu kwa kulia. Aliitikia salamu yangu kwa sauti ya chini, "salama" kisha akaunamisha tena uso wake kama nilivyomkuta.

Nikatulia kidogo nikimtazama, bila shaka alikuwa na kubwa linalomsibu, nikashindwa kuvumilia nikamuuliza, "mama kulikoni?" Akiwa amejiinamia vile, akaniambia anajiskia vibaya sana, amekuja hapo kupima na ameambiwa ana maradhi lakini ameshindwa kumudu kununua dawa, mwili wake ni dhaifu na usiku ule alishindwa kabisa kupata hata usingizi wa kuibia mpaka alione jua la asubuhi.

Nikashikwa na imani sana. Mzee kama yule majira yale ya usiku mkubwa yuko kwenye benchi la zahanati tena akiwa hajui hatma yake, kweli dunia haina huruma! Nikajisachi na kutoa noti ya alfu kumi ambayo nilikuwa nimepanga kuiwekea mafuta kwenye pikipiki baadae nikienda kazini, nikampatia mama yule na kumsihi akachukue dawa na kiasi itakayobakia atapata chakula, mama huyo akanishukuru sana sana, kwakweli sikuwahi kuona mtu akishukuru kiasi kile maishani mwangu, laiti ungeliona alivyokuwa ananitazama ungepata picha halisi namaanisha nini hapa, alinyanyuka na kuendea taratibu duka la dawa la hapo zahanati, duka hilo lilikuwa linatazamana na sisi, akachukua dawa na kunirejea tena kuniaga.

Nikamuuliza, "Utaenda na usiku huu?" Akanijibu, "kwangu si mbali, ni hapo tu nyuma." Akaenda zake. Alipiga kama hatua nne hivi za kichovu, akageuka ghafla na kuniuliza, "yule bwana mnene aliyekuwa amebebelea mwanamke, umekuja naye?" Nikamjibu ndio, akaniuliza tena, "ni wateja ama watu unaowafahamu?"

Nikabaini mama huyo atakuwa aliniona nilipoingia eneo hilo na pikipiki hivyo akadhani huenda mimi ni bodaboda, kabla sijamjibu, akaongezea, "kama ni wateja tu wa barabarani, ondoka upesi achana nao."

Sikuelewa anamaanisha nini kwa kuniambia hivyo, nilimwambia wale ni majirani zangu, si wateja, basi akanitazama kwa macho ambayo niliyatafsiri kama mtu anayewazua jambo kichwani lakini hakusema kitu, nikamuuliza, "kwanini umesema hivyo?" Hakunijibu, akageuka na kuendelea na safari yake, nikatamani kumfuata kumuuliza lakini punde bwana BIGI alijiri akinifuata, alikuwa anatokea kule chumba cha daktari, akaniambia mkewe ameshaanza matibabu hivyo ni vema mimi nikarudi nyumbani kwani wao watabaki hapo usiku mzima.

Kwasababu hiyo, nikamuaga na kwenda zangu kuifuata pikipiki nijiondokee, njiani nikatazama huku na kule kama ntamwona mwanamke yule mzee niliyemsadia lakini sikufanikiwa, ni mataa tu na giza za vichochoro, basi nikalazimika kuamini atakuwa ameshafika nyumbani kwake kwani kwa maelezo yake nyumbani ni karibu tu na pale.

Nikawasha pikipiki na kuondoka, njiani nikiwaza mambo haya ambayo yametoka kujiri kuanzia nyumbani mpaka kule zahanati, mawazo hayo yakanifanya nikaona safari imekuwa fupi sana, yani kitambo kidogo tu nikawa tayari nipo mbele ya geti dogo la kuingia nyumbani.

Nikalifungua geti hilo na kuingia ndani, nilipoufunga mlango wa grill wa nyumba kubwa na kushika korido kwenda kwangu nikasikia sauti ya watu wanaongea, nikashtuka, sauti hiyo inatokea wapi? Niliposkiza vizuri nikabaini inatokea kwenye mlango wa chumba anachokaa BIGI, nikasogea karibu hapo mlangoni na kuskiza kwa umakini, nikagundua ni sauti ya televisheni sio watu wa kawaida, bila shaka yule mtoto wao ndo' alikuwa anatazama, nikajiendea zangu ndani kupumzika.

Zilipita kama siku kama nne hivi bila ya kuwa na makutano na familia hiyo, siku ya tano sasa kama sijakosea, katika majira ya usiku wa saa tisa nikiwa chumbani napambana kuupata usingizi, nikasikia kama kuna mtu huko nje, nikajua ni mwizi sasa ametutembelea tena, basi taratibu nikatoka kitandani na kuchungulia dirishani, dirisha la kule magharibi sikuona kitu ila dirisha hili la kaskazini nikamwona mtu ameketi kibarazani, mtu huyo ameketi akitulia tuli kama mbuyu wa nyikani! Nikastaajabu, huyu sio mwizi, lakini ni nani na anafanya nini kibarazani majira yale?

Niliendelea kutazama, taratibu taratibu nikajiridhisha kuwa mtu yule alikuwa ni mke wa BIGI, kumbe alikuwa amesharejea kutoka hospitali, lakini anafanya nini pale usiku mkubwa? Nilijaribu kukumbuka kama nilisikia mtu akiufungua mlango mkubwa kutoka nje lakini sikukumbuka kabisa, kidogo nikasikia mlango unafunguliwa, mlango wa ndani, alafu kidogo mlango wa grill ukachokonolewa na funguo, tulikuwa tunaweka funguo ya grill kwa juu, mlango ukalia kaaakakaaa alafu ukafunguka, huo mlango ndio ulikuwa unalia hivyo ukifunguliwa, akatoka BIGI akiwa anatembea upesi, akamnyakua mwanamke yule kama kipanga na kifaranga cha kuku, wakaingia ndani!

Kama dakika tu, nikamsikia sauti ya mtoto analia...

Muendelezo soma Jirani yangu wa Kule Goba hakuwa mtu wa kawaida
Duuh ngoja nijiwekee alama
 
Yule Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida - Usiku wa mateso.

Usiku ule sitakuja kuusahau maana yale nloshuhudia yalikuwa nje kabisa ya ulimwengu huu wa nyama na damu, sijui niseme ni ulimwengu gani ule lakini itoshe kusema ni ulimwengu wa ajabu mno nilioonyeshwa na bwana yule ...

Nilikurupuka usiku baada ya kusikia mtu anagonga hodi mlangoni nikadhani nipo ndotoni lakini kumbe haikuwa hivyo, ilikuwa ni kweli mtu anagonga mlangoni, wala sio kwamba masikio yangu yalisikia vibaya, lah, ilikuwa ni uhalisia.

Kabla ya kunyanyuka kitandani nikatazama nje dirishani, huko palikuwa shwari, kumetulia tuli-tuli, hata nilipoangaza mlangoni niliona mlango wa grill umefungwa, basi nikatulia kidogo nikijiuliza yanayoendelea, bado hapo mlango wangu ukiwa unaendelea kugongwa na kugongwa.

Mwishowe wa kufikiri niliamua kupiga moyo konde nikaenda sebuleni, nikawasha taa kisha nikaufuata mlango na kuufungua, kutazama simwoni mtu! Nilitazama korido nzima nisiambulie kitu wala mdudu yoyote anayetembea ukutani, nikatazama milangoni, nikaona kila mlango kwa chini yake ukiwa ni kiza totoro, taa zimezimwa huko ndani, ni kimya cha mwituni! Moyo wangu unapiga kana kwamba unataka kutoka kifuani.

Kabla sijaufunga mlango, yaani nikiwa hapohapo bado naangaza, mara nilisikia sauti ya kikombe kikidondoka - puuh!- alafu ikafuatia na kilio kikali cha mtoto kule chumbani! Basi haraka nikaurejesha mlango wangu pasipo hata kuufunga na funguo, nikakimbilia kule chumbani kama mwendawazimu, kufika huko nikawasha taa upesi, kurusha macho kitandani namwona mtoto ameegamia ukuta, uso wake ameufinyaga kwa kilio na hofu. Chini kuna maji yaloyomwagika pamoja nayo kikombe cha plastiki ambacho huwa tunatumia kunywea maji.

Mtoto aliponiona alinikimbilia akanikumbatia kwanguvu akinambia baba kuna mtu baba kuna mtu ... Nikamuuliza mtu gani? Yuko wapi? Hakusema cha kueleweka.

Alikuwa anatetemeka mwili mzima, macho yake hayakomi kumwaga machozi, hapo amening'ang'ania kana kwamba nilimuahidi nitamrushia korongoni.

Nilitazama kila kona ya chumba lakini sikuona chochote kilichomtisha, kidogo nilipotazama dirishani, ndo' nikaona kivuli cha mtu akiwa anachungulia, kivuli kipana katika kingo ya dirisha langu la kaskazini, lakini kivuli hicho -kufumba na kufumbua - kilitokomea kwa kushuka chini! Nikastaajabu kuona.

Nilitulia hapo kidogo nikitazama, kila kitu mbele ya macho nikiona kama miujiza ama ndoto hivi, yaani muujiza mbele ya mboni zangu, niliporadhi ndipo nikasogea taratibu dirishani kutazama nje. Huko palikuwa pametulia tuli, hamna mtu wala kiumbe ninayemwona, lakini niliporusha macho kule kwenye mlango wa grill, nikaona mlango huo uko wazi! Sikujua nani nani aliufungua na ni muda gani alifanya hivyo maana sikusikia mlango huo ukipiga kelele zake za siku zote, nikabaki tu nikiutazama kwa kama dakika moja, sikuona kitu wala mtu hapo, kidogo nikasikia tena mtu akiugonga mlango wangu kwa mtindo uleule --- ngo ngo ngo ngo! "Nataka tuongee, nina shida na wewe!"

Aisee nikahisi tumbo linakoroga, miguu yangu inapoteza nguvu, pumzi yangu mwenyewe inanikaba. Kwa muda huo nilitamani pakuche lakini wapi! Nilihisi muda umekwama kunikomoa na mateso ya usiku ule. Nilitazama saa ya simu yangu nikaona zimepita dakika tano tu tangu nikurupuke toka usingizini, nikaamini kabisa muda unashirikiana vema na mtesi wangu. Ule ulikuwa usiku wangu wa adhabu.

Nikajitahidi kutulia kadiri nilivyoweza lakini sikufua dafu abadan, mlango wangu uliendelea kugongwa pasipo kukoma huku mtu anayegonga akinitaka tukaongee tena akitumia sauti yangu, moyoni nikaapa siendi popote, nitabaki palepale kitandani na mtoto wangu mpaka nione nini kitakachojiri.

Baada ya dakika moja ya kuvumilia, nasikia kabisa mlango unagongwa lakini napuuzia, mara nilisikia kitasa cha mlango kikitenguka - 'klap!'- alafu ikafuatiwa na sauti za bawaba za mlango 'kkrrriiiiiiiiii!' ... sauti zilizoashiria mlango wangu unafunguka alafu sauti hizo zikakoma ghafla na kuwa kimya! Kimya cha kaburi. Kwa kama dakika tatu hivi ni kimya, sikusikia kitu chochote kile, nipo tu kitandani nimemkumbatia mwanangu.

Kwa kipindi chote hicho,sikuwa najua nifanye nini maana ubongo wangu uligeuka kuwa uwanja wa fujo, moyo nao unapiga mpaka nausikia masikioni kana kwamba ngoma za turufu! Jasho nalo linanichuruza nalisikia kabisa likishuka mgongoni chii-chii-chii kuangukia chini.

Sasa baada ya kimya hicho cha muda, nilisikia vishindo vya miguu vikipita sebuleni, vinakatiza hapa na pale, pale na hapa, alafu baada ya sekunde kumi na tano hivi, mlango wangu wa chumbani ukagongwa mara moja, "ngo!" ... Ile 'Ngo' ya kuashiria mgeni ameshafika ndani kisha kukarudi kuwa kimya tena, kimya cha awali.Sasa nikawaza,kama mtu huyu amengia ndani kwangu, je, mimi sina budi kujihami na kitu chochote nilichonacho?

Upesi nikatazama kwenye pembe ya kitanda changu, kule nilazapo miguu, hapo kulikuwa na fimbo moja ndefu nene, nikaichomoa na kuishika mkononi barabara kama lolote likitokea basi nipate kujihami, lakini nilishika fimbo hiyo mpaka nikachoka, hamna nilichokiona wala hamna kilichoingia ndani.

Nilimaliza sala zote ninazozijua, nilimuita Mungu wangu kwa majina yote niliyofunzwa kanisani na mtaani lakini bado nilijihisi niko mwenyewe, dunia imenipa mgongo.

Nilingoja hapo kwa muda ambao niliona unatosha, nikanyanyuka kwenda kuufungua mlango wa chumbani kutazama sebuleni kama kuna mtu niliyemuhisi,kufika huko na kuangaza sioni mtu, lakini nilipotazama mlango wa sebuleni nikauona uko wazi, tena wazi ya kuachama haswa, nikarusha macho huko nje ya mlango, yaani koridoni, napo sikuona kitu wala mtu, lakini kitambo kidogo nikaanza kuhisi naishiwa nguvu katika namna ya ajabu, kichwa kinakuwa kizito na macho yananielemea, sijakaa vema nikaanguka chini, hoi taabani, hata kuusogeza mkono wangu mwenyewe nashindwa, sijiwezi kabisa, kitu pekee nilichokuwa namudu ni kusikia na kuona tu!

Nikiwa hapo chini, nimelala kifudifudi,sijui nini kinaendelea, macho yangu yanatazama kule koridoni, mara nilisikia sauti ya mlango unafunguka, haukuwa mlango mwingine bali mlango wa BIGI, na kitambo kidogo nikamwona mwanaume huyo anatoka sasa akija mwelekeo wangu.

Bwana huyo alikuwa amevalia kaniki nyeusi kiunoni, mithili ya taulo la kwendea bafuni, na kichwa chake amekiveka kiremba kikubwa chekundu, kiremba ambacho baki yake aliilazia kwa nyuma kana kwamba mwanamke mwenye nywele ndefu.

Kumwona bwana huyo akinijia, nikajaribu kwa nguvu zangu zote ninyanyuke lakini sikuweza kabisa kabisa, nilikuwa kama mtu aliyepigwa nusu kaputi kwaajili ya upasuaji, kitu pekee nilichokuwa naweza kufanya ni kugeuza shingo yangu huku na kule, hata nilipojaribu kutoa sauti kupiga yowe nayo hakuna! Nilikuwa mithili ya samaki majini, naachama tu mdomo lakini hamna chochote kinachotoka.

Bwana yule, nikiwa namshuhudia kwa macho yangu, aliingia ndani akaelekea moja kwa moja chumbani, kule ambapo mwanangu alikuwamo, huko sijui akawa anafanya nini, hata mtoto alikuwa kimya, baada ya muda kidogo akatoka akiwa amembeba mtoto begani huyoo anajiendea zake.

Aliuruka mwili wangu akatoka mlangoni kisha moja kwa moja akaenda kwake ... Nimebaki tu namtazama, macho yanavuja machozi ... naona kabisa mwanangu akienda kuuawa na huku sina la kufanya.

Nilifurukuta nikafurukuta ... nilifurukuta tena na tena. Nilifurukuta kwanguvu zangu zote na za akiba, nikatahamaki niko kitandani nimeketi nahema kama mbwa wa mashindano, nikajaribu kuunyanyua mkono wangu wa kulia, mkono ukanyanyuka, nikausogeza mguu, nao ukasogea, nikajiuliza ina maana yale yote niliyoyaona nilikuwa ndotoni?

Nilijikuta nafsi yangu inakataa.

Nilitazama kando yangu nikastaajabu mtoto hayupo, kitanda cheupe pe, nikanyanyuka upesi kama nakimbizwa kwenda kuwasha taa, nikawasha na kuangaza sikuona kitu, chumba kizima nilikuwapo mwenyewe. Nikakimbilia sebuleni kutazama, napo sikuona kitu, hata mlango wake umefungwa na funguo! Sasa nikahisi kurukwa na akili, mtoto yuko wapi?

Hapana! Nilizungumza mwenyewe kama mwehu ... hapana haiwezekani! Nikaufungua mlango wangu nikaenda moja kwa moja mpaka mbele ya mlango wa BIGI, nikaugonga mlango huo kwanguvu BAM-BAM-BAM-BAM! Fungua, namtaka mwanangu! BAM-BAM-BAM!- niliubamiza mlango huo bila huruma na bila kukoma, nafoka na kuchonga, namtaka mtoto wangu!

Kelele hizo zikawaamsha watu walokuwamo kwenye makazi ya Tarimo. Niliona wamewasha taa ndani wakiwa wanazozazoza, bila shaka walikuwa wanajiuliza ni nini kinachoendelea, lakini mimi sikujali, nikaendelea kuubamiza mlango wa BIGI niking'aka, kidogo mlango huo ukafunguliwa akatoka mwanaume huyo mpana akiwa amevalia kaushi yake pana na bukta.

Kabla hajasema kitu nikamwambia, "brother, namwomba mwanangu! Tena namwomba upesi kabla hatujajaza umati wa watu hapa."

Akawa ananitazama, hasemi kitu. Mara nikasikia mlango wa makazi ya Tarimo unafunguka, kutazama ni Mama Tarimo, mama huyo anatoka huku akiwa anatengenezea khanga yake kifuani, nyuma yake yuko dada mmoja hivi ambaye sikuwa namfahamu wana mahusiano naye gani, wote hao wawili nyuso zao zimeparwa kwa maulizo.

Mama Tarimo aliuliza, "Shemeji, kuna nini?" Nami upesi nikamwambia yule bwana BIGI amemchukua mwanangu kimazingara na mimi nimekuja hapo kumfuata. Kwa jazba nilokuwa nayo sikuwa najali chochote kile, niliyamwaga maneno mengi na vitisho, nikiapa siondoki pale mpaka pale nitakapompata mwanangu.

BIGI aliuliza, "Una uhakika mwanao yumo humu ndani?" Nikamwambia ndio, nikamtaka asogee pembeni mimi niingie ndani kutazama. Katikati ya hayo, mara Mama Tarimo akaniita: baba fulani, nilipomgeukia akaniuliza,"yule pale si mtoto?"

Kuangalia kwangu, nikamwona mtoto akiwa amesimama mlangoni ananitolea macho. Nikastaajabu. Nini hiki? Nilimwendea mwanangu upesi nikamkagua na kumuuliza alipokuwapo,akasema ndani, ndani gani na mimi niliangaza kila kona ninayoijua?

Niligeuka kumtazama BIGI, nikamwona bwana huyo ananiangazia, kama kawaida macho yake hayakuwa hata na tone la hisia ndani yake, hakusema kitu, ameegamia tu kingo ya mlango wake, nikaurejesha uso wangu kwa mtoto, nikamwona akiwa amejibana kwangu, amenishikilia nguo, anachungulia kwa woga.

Kidogo bwana BIGI akaingia ndani mwake, pia na Mama Tarimo, mimi nikawa wa mwisho kuufunga mlango.

Nilimpeleka mtoto kitandani nikamtaka alale lakini mimi nikiwa nasumbuka sana na mawazo kichwani, ina maana ni kweli mimi nilikuwa ndotoni? Ina maana yale yote ni mambo tu yaliyotungwa na ubongo wangu?

Sikuridhika...

Nilikagua mazingira ya mule chumbani, na hata sebuleni, nikaamini kabisa sikuwa ndotoni. Yale yote nloshuhudia yalikuwa halisia. Moja, kikombe kile cha maji bado kilikuwapo chini na maji yale bado sikuyadeki, lakini pili jasho nililomwaga nikiwa pale sakafuni sijiwezi kabisa, bado lilikuwapo, sasa halikuwa kimiminika bali limeganda pananata.

Sasa ilikuaje? Sijawahi kuelewa mpaka leo hii.

Baadae Jua lilipochomoza nikalishuhudia kama ukombozi, tena ukombozi nilioupambania kwa muda mrefu, mbali na kwamba nilihisi maumivu ya hapa na pale ya taya yangu ya chini, mimi sikujali sana na nilichofanya, pasipo kupoteza muda, nilidamka nikamwandaa mtoto na mimi pia kisha safari ikaanza kuelekea Massana hospitali, huko nilionana na mke wangu na pia mama yangu ambaye alifika muda si mrefu hapo, nikamwachia mtoto mama yangu nikimtaka aende naye kwake kule Mbezi Beach, Afrikana, mimi nitakuja kumpa habari vizuri nikitoka kazini, uzuri kumbe siku hiyo ndo' ilikuwa siku ambayo mke wangu alikuwa anategemea kutoka hospitali, hivyo basi wakaona ni vema wakienda huko Afrikana kwa pamoja. Mimi niliwaahidi nikitoka tu kazini nitaonana nao.

Baada ya kuachana nao, nilielekea kazini, huko niliweza kufanya kazi kwa kama masaa mawili ya mwanzoni lakini baada ya hapo nikaelemewa. Kichwa kilikuwa kizito kwa kukosa usingizi wa usiku ulopita kiasi nikawa naona kazi ni adhabu. Macho yananiwasha na niko 'slow' sana.

Nilitafuta 'kamuda' fulani, mbali na kubanwa hapa na pale, nikajipumzisha kidogo kwa kuegamia meza, usingizi ukanikomba bila huruma, kuja kuamka nimelala masaa mawili kama utani, na kama si kuamshwa sijui ningeamka saa ngapi? Kutazama simu yangu, naona 'missed call' na ujumbe mmoja, vyote vimetoka namba ngeni.

Ujumbe huo nilipoufungua ulikuwa unasomeka hivi: "Mimi Bembela nimesharudi nyumbani fanya tuongee." Nikapiga namba hiyo mara moja, simu ikaita kidogo na kupokelewa na sauti ya mwanamke, sauti ya Bembela, akanisalimu na kunijuza kuwa amefika nyumbani muda si mrefu, kila kitu amekiweka sawa lakini kuna jambo moja tu amekwama, anataka kuona kama naweza nikawa na msaada.

Alisema: "baba fulani, hapa sasa ili kila kitu kiende sawa, nahitaji nipate kitu kimoja ambacho ni mali ya yule bwana. Kitu kimoja tu, kama vile yeye achukuavyo vyetu na kuvitendea kazi, ndivyo na mimi pia. Je, unaweza nisaidia?"

Nikawaza vile viroba vya BIGI kule korongoni, je, mule hatuwezi kupata kitu? Nilipomweleza hayo akanielezea hofu lake ya kwamba vitu vile havina uhakika kama ni vyake au vya watu wengine, tusije tukawaingiza waso na makosa katika adhabu ya mtu mwingine, hivyo yatupasa kuwa na hakika asilimia zote.

Nilipofikiria vema, nikaikumbuka ile sarafu ya hamsini katika mfuko wangu wa suruali. Nilikuwa na hakika kabisa ile ilikuwa ni mali ya BIGI lakini ubaya ni kwamba sarafu hiyo siku ile nilivyotoka hospitali baada ya kunisababishia majanga sikukumbuka niliiweka wapi haswa, sikuibakiza nguoni mwangu.

Ila kitu kilichonipa moyo ni kwamba mke wangu hakuwapo nyumbani, na mimi sikuwahi kufanya usafi mule ndani chumbani tangu siku ile, hivyo niliamini naweza nikaipata nikiitafuta.

Nikamwahidi Bembela na yeye akakata simu tulipomaliza maongezi.

Mbali na kwamba, nilikuwa nimeokoa salio langu la simu kwa simu ile kukatwa na Bembela, nilikuwa pia nimejipunguzia maumivu ya kinywa changu ambacho kilikuwa kinanivuta sana, haswa taya ya chini, kila nilipokuwa nazungumza neno.

Sikufahamu maumivu hayo yalisababishwa na nini na sikudhani kama yangeendelea kuwa makali vile, kipindi nayahisi pale asubuhi niliyachulia kiwepesi tu nikidhani labda nililala vibaya na hivyo yatakoma lakini kadiri muda ulivyoenda nilianza kuhisi hiyo kitu ni 'serious'.

Na kweli ilikuwa ni 'serious'.

Mpaka kufikia majira ya usiku, taya yangu ya chini ilianza kupinda ikielekea upande wangu wa kushoto wa mwili! Kila nilipoivuta kuiweka sawa, nilihisi maumivu makali yasokuwa na mfano!

***
Mnyakatari hii nyingine
 
Nasoma hii story navuta picha nyumba niyohama Goba...mazingira kama yanafanana

Na hiyo nyumba niliyohama Kuna BIG ila yeye ana gari..kumuona ni nadra mtu wa mishe Sana na upande aliopanga unakaribiana na geti la kutoka nje na ukienda mbele kutoka hapo kwetu Kuna kapori halafu Kuna korongo na Kuna mto ....
Hizi story zingine zinafanana na mazingira ya Kweli duuh...
Tatizo Goba vipori na makorongo yapo mengi sana [emoji2]
 
Ndo maana simteteagi Steve wakati anapigwà mapande na dr namugari ,hii Ng'ombe ishatuona kama sisi ni wadwanzi wanzake,..kulikuwa na haja gani ya kusema kuwa ataleta post nyingine usiku mkubwa kama hakuwa na uhakika wa muda na nafasi yake?,...angepiga kimya tu bila kusema ataleta nyingine,....umekaa cku 5 hujaonekana then unajileta na viji excuse vya kidwanzi as if sote umetuona mazoba yako,we kama huna muda potea unakopoteleaga cku ukija weka kijipost chako kimoja then lala mbele bila kuahidi chochote Ng'ombe mmoja ww,cku zote nakucheki tu kwa mbali nakuvungia ila sasa naanza kuwaelewa kina ARV wanavyokumwagiaga ushuzi kengele flan ww
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Yule Jirani yangu wa Goba hakuwa mtu wa kawaida - Bonus ya usiku ulopita.

Katika majira ya saa mbili kasoro usiku, nilitoka kazini nikipanga kwenda kwanza nyumbani, Goba, alafu ndo' niende kule Afrikana kuungana na familia yangu. Sababu ya kufanya hivyo ilikuwa ni kumtimizia Bembela takwa lake kisha nimwache aendelee kufanya kazi yake kwa usiku huo.

Nilipofika nyumbani, nilitafuta ile sarafu ya hamsini pale kwenye droo ya kitanda, sikuiona, nikakung'uta nguo zangu nilizozivaa karibuni, napo pia sikuambulia kitu, zote zilikuwa kavu mifukoni, nikatazama chini ya kitanda tena kwa kumulika na tochi ya simu yangu, sikuona kitu.

Nikaketi nikijaribu kuwaza, wapi nimeweka pesa hiyo ya sarafu? Nilifanya kila kumbukumbu na niligusa kila eneo langu la michezo lakini bado sikufua dafu.

Kidogo wazo likanijia, nikague nguo za mwanangu, haswa zile nguo ambazo alizivaa hapa karibuni, basi nikafanya hivyo kwa upesi, japo kumbukumbu yangu ya nguo zake haikuwa vema sana, nadhani zoezi hilo angelifanya mama yake lingekuwa na ufanisi zaidi kuliko mimi. Nilitazama nguo hizo moja baada ya nyingine lakini napo sikupata kitu! Sasa nikakaribia kukata tamaa. Taratibu nikaanza kuwaza huenda pesa ile haimo ndani.

Nikiwa hapo nawaza, kama bahati tu nikasikia watu wakiwa wanaongea huko nje, walikuwa ni wanawake katika bomba la maji, sauti ya mmojawapo ikanipatia wazo, nayo haikuwa ya mwingine bali ya Mama Tarimo, upesi nikatoka ndani kwenda nje kuonana naye, nilipomfikia nikamuuliza, japo kwa taabu sana kwasababu ya mdomo wangu kuuma, kama amepata kuona popote pale mwanangu akiwa na sarafu mpya ya hamsini, akanijibu hakupata kuona.

Lakini wakati naondoka, akaniita na kuniuliza kuhusu sarafu hiyo, alistaajabu ni kwanini naitafuta maana haiwezi kunipa chochote kwenye duka la sasa, nikamweleza nilikuwa na kazi nayo fulani, kazi ambayo mimi sikutaka aifahamu kwa muda huo, lakini ajabu, wakati nikiagana naye nipate kwenda, aliniambia: "lakini ninazo sarafu zingine kama hiyo unayoitafuta."

Nikasita nikimtazama, naye akatazama watu wengine kabla hatujasogea kando kidogo tupate kuongea. Huko pembeni akaniambia jambo ambalo lilinistaajabisha kidogo, mama huyo alisema anazo sarafu kama ishirini hivi za shilingi hamsini hamsini, sarafu mpya kabisa kana kwamba zimetoka benki muda huu, mimi upesi nikamuuliza sarafu hizo amezitoa wapi? Kwa sauti ya chini akanijibu alimwona nazo mwanaye mdogo, naye alipomuuliza akasema alipewa na yule mtoto wa BIGI mwenye matatizo ya akili.

Aliniambia, "yule mtoto huwa anakuwa na hizo sarafu kedekede anawagawia wenziwe wakiwa naye, siku ya kwanza niliziona nikazipuuzia lakini kadiri nilivyokuwa naziona tena mara kwa mara, nikaanza kuzitunza, hata sasa ninazo kama za alfu mbili hivi!"

Nikamuuliza kama pesa hizo ameshawahi kuzichanganya na pesa zingine, akaniambia hajawahi kamwe, pesa hizo amekuwa akizitenga mbali kabisa na pesa zake za kila siku kwani alizihofia na hakuziamini kabisa.

Hofu hiyo ikanipa mimi maswali - nini kilimfanya akahisi mawazo hayo? ... Nadhani aliusoma uso wangu wenye maulizo akaamua kufunguka mwenyewe, akaniambia namna mume wake alivyokuwa na mashaka juu ya yule jirani yetu na alishamweleza mambo kadha wa kadha kabla hajapata kulala kwenye kitanda cha hospitali kwasababu ya ajali.

Baada ya maelezo hayo, nikaongozana naye mpaka kwake, akanipatia sarafu tano za shilingi hamsini, sarafu ambazo zilikuwa zinang'aa kana kwamba lulu, kisha akanitakia mema na hicho ninachoenda kufanya nazo, mimi kutoka hapo nikaenda moja kwa moja kwenye mlango wa Bembela, nikagonga na punde mwanamke huyo akanikaribisha mpaka ndani.

Humo nilimkuta akiwa na mwanamke mwingine ambaye mimi sikuwa namfahamu, mwanamke huyo ni mzee wa makamo ya miaka hamsini na kitu hivi, Bembela akanitambulisha kuwa ni shangazi yake, na mwanamke huyo ndiye aliongozana naye kwenda huko Tanga kwa mtaalam hivyo basi mimi niwe huru mbele yake.

Lakini mbali na hilo, kwasababu uso wa mtu haujifichi kama sehemu za siri, Bembela aliniona na alistaajabu kuhusu mdomo wangu ulopinda, alinihurumia sana namna ninavyoongea na namna nilivyohisi maumivu nikifanya hivyo lakini akaniahidi yote yatakuwa sawa muda si mrefu.

Alisema, "najua hii ni kazi ya mikono yake, hamna mtu mwingine, ila mwisho wake sasa umefika, atalipa yale yote aliyoyafanya!"

Mwanamke huyo alinieleza mambo mengi ya pale nyumbani, mambo ambayo alipata kuyaona kule alipokuwa kwa mtaalamu, jinsi gani bwana BIGI alivyofanikiwa kugusa kila mlango wa kila nyumba hata wengine wakiwa hawana ufahamu mpaka sasa, lakini katika yote alokuwa ananieleza, mimi likanigusa sana jambo la bwana Tarimo na la jirani mwingine mmoja ambaye kazi yake ilikuwa ya kiwandani, Twiga Cement, nikaamini kweli hasidi haitaji sababu. Bwana huyo, pamoja na kazi yake kuwa ngumu na ya kutaabika kiwandani, hakuwa anaionja pesa yake hata thumni. Kila alipokuwa akipata ujira wake, matatizo yaliamka kutoka kila kona nane za dunia yakamwandama na kumwacha mtupu!

Haikujalisha namna gani alihangaika na kujipanga, hakuwahi kutoka katika huo mtego kamwe.

Akiwa ananieleza hayo, mara kidogo mlango ukagonga na kufunguliwa, kutazama alikuwa ni shoga yake na Bembela, sasa nikaona ni muda wangu sahihi kuondoka, nilisimama kumpisha maana sehemu ya kukaa ilikuwa finyu kisha nikawaaga niende zangu, hapo tayari nishamkabidhi Bembela mzigo wake wa zile sarafu.

Kabla sijatoka, Bembela alinikabidhi kimfuko kidogo cha 'nylon' kilichofungwa fundo moja kubwa, ndani yake kuna unga laini wa kahawia, akaniambia, "kachanganye dawa hii na maji yako ya kuogea, utakuwa unaoga asubuhi na jioni, ni dawa ya kujisafisha na dhalili zote zilizowekwa na mtu mbaya, tena ni vema ukampatia mke wako na mtoto wako."

Nikamshukuru kisha nikaenda zangu. Niliwasha pikipiki moja kwa moja mpaka maeneo ya Afrikana, Mbezi Beach, kabla ya kwenda nyumbani nikaona ni stara kupitia kwenye duka moja la dawa kuchukua dawa fulani za maumivu kwaajili ya taya zangu. Kwasababu nilipitia njia ya 'Kwa Zena' niliingia pale 'Yes Pharmacy', moja ya famasi kongwe eneo lile, nikaeleza hitaji langu, lakini punde mfamasia aliponiona na hali yangu akaanza kunipa maelezo kedekede, maelezo ambayo kwakweli yalinitisha sana.

Aliniuliza kwanza najiskiaje na miguu na mikono yangu,vidole na maungo yangu, kisha akaniuliza tena najiskiaje ninapotembea, nilipomwambia nimekuja na pikipiki akastaajabu sana, aliniambia niende hospitali haraka kwani yawezekana kabisa nipo kwenye hatari ya kupata kiharusi, hemiplegia, basi nikaondoka hapo nikiwa ma msongo wa mawazo kweli.

Nilipowaza pia na nyumbani ninapoenda itabidi nikaanze kutoa maelezo ya nini kimenikumba na huu mdomo, nikachoka zaidi.

Nilipofika nikamweleza mama na mke wangu yale yalonisibu alafu nikapata kwenda kitandani mapema kabisa kabla baba hajarejea maana nilijua ningeanza kurudia tena maelezo ambayo tayari nimeshayatoa, lakini katika yote hayo niliyoeleza sikusema lile la famasi kamwe, niliona itakuwa nongwa kubwa nikilitamka, watu watajawa na hofu kisha wakaniparamisha.

Lakini usiku huo mimi sikupata usingizi kabisa, nilikuwa najigeuza huku na huku nawaza, najigeuza kule kule nawaza, najigeuza hapa na pale maumivu.. najiuliza hali yangu na yale yanayoendelea nyumbani.

Nilikuja kupata usingizi saa kumi na moja alfajiri, nakuja kuamshwa baadae na mke wangu, majira ya saa tatu asubuhi, baada ya simu yangu kuita mara kadhaa na yeye kupokea simu kutoka nyumbani, yani kule Goba.

Aliniambia amepigiwa simu hiyo na jirani Mama Tarimo ya kwamba nyumbani kuna taarifa mbaya. Kusikia hivyo, moyo wangu ukaruka pigo. Nilijikuta akili yangu inafikiria upesi kila kitu cha jana yake, kabla sijaanza kutunga yatakayokuwa yamesibu huko, akaniambia ni taarifa za msiba.

Kuna mtu amefariki usiku wa kuamkia siku hiyo.
Huyo aliyefariki lazima atakua ni Bembela tu
 
"Kuna mtu amefariki usiku wa kuamkia siku hiyo"

HAPA ATAKUWA MKE AU MTOTO WA BIGI AMEONDOKA, BEMBELA KASHAFANYA YAKE.
 
Back
Top Bottom