KING MIDAS
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 8,589
- 16,936
Raia wa Burkina Faso, Iron Biby, majina halisi, Cheick Ahmed al-Hassan Sanou aweka rekodi ya mtu mwenye nguvu zaidi duniani 2024.
Hii ni baada ya Iron Biby kubeba chuma kilo 231 na kuvunja rekodi ya dunia wakati wa mashindano ya Dunia ya kuinua Magogo 2024 (WLLC)yaliyofanyika Birmingham, Uingereza.
Mnyanyuaji huyo bora zaidi katika historia na pia mtu mwenye mikono kubwa zaidi, aliwaacha wengi vinywa wazi licha ya kushiriki kama mgeni maalum katika mashindano hayo kufuatia ubingwa wake wa awali wa mashindano ya kubeba chuma duniani 2023, ambapo alibeba kilo 230.