Jiunge nami kusema hapana kwa udhalilishaji na ubaguzi anaoufanya mmliki wa clock tower café Iringa

Hii ndo tabu ya kuishi mikoani mji mdogo karibu watu wote wanajuana sasa wewe umefunga unabanwa vipi na mkojo hahahah
 
Wakili weka mambo sawa hapo ubaguzi warangi yako umeingia vipi ww kakuzuia kwenda kumjazia choo ambacho hakipo kwa ajili ya umma sasa uwarabu na uhindi umeviunganishaje

Wewe ndio utakua mbaguzi
Heshimu biashara Za wenzako wacha ujanja ujanja bwana Wakili
 
Daaa! Kumbe hapo sikuhizi ni Mgahawa? Tunashukuru kwa taarifa Mh. Wakili,lkn kwa maelezo yako mwenyewe unasema ofc yako ni jirani na mgahawa huo,Sasa kwani hapo ofcn kwako hamna choo ya ofc? Na kwanini unaenda kushusha mzigo kwenye choo Cha mwenzio Tena sehem ya biashara? Pia Jambo lenyewe ni fupi ila wewe umeandika maelezo mengi mengi na mengine hayana msingi,utanisamehe aisee ila kwa bandiko hili unatakiwa ujipike sana kwenye melezo/ kuandika ur still poor in this area.
 
Nashukuru kuwa umenipa taarifa juu ya Mgahawa huo Mpya... Nilizoea kwenda Lulu's Cafe
 
huyo mwenye hiyo cafe chama gani ? kama ni chadema hapo Iringa tunaye mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa anaitwa Msigwa , ni suala la kumjulisha tu na hatua zitafuatwa
 
Hahaha mimi nimecheka kwa sababu SIJAUONA UBAGUZI wowote hapo. Huwezi kulazimisha kutumia choo cha mtu mwingine bila idhini yake kwa sababu ya rangi yako. Kwani hapo Iringa kuna choo mahali hapo tu Clock Tower café? Kama kuna nyumba jirani na hiyo Café kwanini hukwenda kuomba kujisaidia huko kama huyo mmiliki wa café kakataa? Kubanwa na haja iwe kubwa au ndogo ni matatizo yako, kama yalivyo binafsi kwa kila binadamu. Lakini huwezi kulifanya hili likawa tatizo la ubaguzi wa rangi, Eti wewe ni mwanasheria, mwanasheria unalazimisha kutumia mali ya mtu bila ridhaa yake? Kwanini usilishitaki jiji la Iringa kukosa VYOO VYA UMMA?! Choo binafsi ni mali ya mmiliki na choo cha umma ni mali ya wote kwasababu kinajengwa kuhudumia umma wote na kwa kutumia pesa za kodi zetu.

Umenishangaza mwanasheria kudai kutumia mali ya mtu kwa lazima, hili limenishangaza sana. choo ni kwa ajili ya wateja wake, wewe siku hiyo hukuwa mteja wake, huwezi kujipa uteja kwanguvu, yeye hawezi kukumbuka wateja wote wa siku za nyuma.
Ulipoingia ulipaswa kueleza shida yako kwao, siyo kama ulivyofanya wewe , uliwasalimia ukapitiliza kwenda chooni, huo siyo ustaarabu. Ustaarabu ni kueleza shida yako kwa mmiliki, kwamba umebanwa na unaomba ujisaidie chooni. Lakini ulijipa uteja kwa nguvu na uliona unahaki kutumia choo cha café kama mali ya umma, hiyo siyo halali. Swaumu yako haina uhusiano na choo chake, na uwakili wako hauna haki kutumia visivyo vyako. Utaratibu ni kuomba, kasha unapewa au kunyimwa.
Acha kulazimisha ubaguzi hata mahala pasipokuwa na ubaguzi.
 
Bwana wakili biashara haitaji mazoea iyo ni kazi kama ilivyo kaz yako mtu hawezi kukurupuka tu , bila utaratibu kisa amekuzoea akakwambia nna kesi yangu twende maakaman ukawe wakili wangu bila utaratibu maalum.
 
1. Mkiwa katika sehemu au eneo ambalo liko confined kama hapo Iringa ni rahisi kukwazana wakati mwingine bila kujua kwa sababu gani, labda
a. Itikadi za vyama
b. Mapenzi
c. Maslahi ya kikazi, inawezekana unamtetea hasimu wake
d. Majungu
e. Marafiki, coincidentally adui yake ni rafiki yako

2. Take it simple, dont complicate so far wewe sio uliolianzisha ni weakness yake yeye SIO WEWE calm down, smile, take it easy, thank God

3. Nahisi ulikosa Courtesy, ulipaswa kwanza usalimie kisha uombe kuingia msalani sidhani kama haya yote yangetokea

4. Ingawa amekuumiza mbele za watu lakini SAMEHE, haigharimu kitu. Sana sana inapunguza kutembea na mizigo ISIYOKUHUSU
 
Baada ya kumkata kelebu wewe unaleta uzi hapa wa kulalamika, kama mambo yenyewe ndio haya tutakuwa watumwa. Mpaka mwisho wa dunia hii, sasa wewe wakili mpeleke mahakamani na umfugulie shitaka la ubaguzi na udhalikishaji.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Hata hii sijamaliza
 
Ilivyokua iringanet cafe mmilik alikua feisal mtoto wa amani store, kama bado mmilik ni yule mwarabu bas mtoa mada atakua sahihi yan jamaa ni mvuta bangi na mlevi had jamii ya kiarabu ilimtenga
 
sijaona hoja ya msingi ,maana ya mfungo unaijua,?mojawapo ni kushinda vishawishi kwa maana hiyo mfungo wako haukua na mantiki kama ulishindwa kukabiliana na hasira kwa kutumia imani yako,katika kipindi cha mfungo wa kweli lazma ukutane na majaribu /vishawishi kupima imani yako,ulipaswa kitumumia hekima kukabiliana na jamaa huyoo..aksante
 
NIMESOMA SIJAONA UBAGUZI HAPO!!😳

Anadai alienda kujisaidia, Ghafula anaambiwa usiingie Tena kwenye hiyo hotel !!!! Inawezekana kweli ndivyo ilikuwa?


Mtoa Mada pamoja na kwamba NI Wakili uwezo wake NI mdogo Sana sijui hata kesi huwa anashinda!!

Kwa mfano kilikuwa na sababu gani kutaja Mambo ya mfungo, meeting Ramadhani na kwenda kujisaidia?

We unafikiri watu wote wanaujua au kuutambua mwezi wa Ramadhani?

Sikuona hoja yoyote iliyokusababusha uanze kuingiza Mambo ya mwezi wa Ramadhani na tendo la kujisaidia!!!

Halafu unadai umebaguliwa !!! Sasa hapo umebaguliwa kutoka kwenye kundi lipi?

MIMI SIUNGANI NA WEWE KABISAA KULAANI HUO UBAGUZI UNAODAI KUFANYIWA, SIJAONA UBAGUZI. HALAFU HATUWEZI KUSIKILIZA UPANDE MMOJA HALAFU TUTOE HUKUMU, WE MWANASHERIA YA WAPI UNAYEMALIZA KESI KWA KUSIKILIZA UPANDE MMOJA? WANASHERIA WENYE MTAZAMO KAMA WAKO NDO MAWAKILI WA SERIKALI MNAOITAABISHA SERIKALI KWA USHAURI MBOVU.
 
Haha kama ni ngoda ni mtata kwa asili niliwahi kupata taarifa za kutaka kumpiga mwenyekiti wa baraza la nyumba na Ardhi hapo Iringa. (District Land and Housing Tribunal ) .

Badilika mkuu Ngoda, it is not that late.
 
Ujumbe wako nmekuelewa Kaka vizuri Sana.Ila tatizo nyie waislam huwa mnawaonaga waarabu Kuwa ni Mungu wenu wa pili Ila wao waarabu wanawadharau watu weusi na kuwaona kituko. Pole Ila nafikiri kuna kitu umejifunza kutoka kwa hawa jamaa. Waarabu na Wahindi ni watu tulioishi nao Tanzania miaka mingi Ila Wana Racism. Mimi niliwahi kusoma na Wahindi flani Thailand walikuwa very Racism.
 
Vatete [emoji28][emoji28][emoji28]
 
Siku nyingine ujifunze kwamba hao watu wenye asili ya (hasa) Asia huwa hawana urafiki wa kweli na wa kudumu. Wanapokuwa wanakuhitaji kwa maslahi yao utaona mema yote. Akimaliza uhitaji hana muda nawe. Halafu kuna maliwato pale Garden, Soko kuu na hata mahakamani kama ndipo ulipotokea.
KUKUKKUMBUSHA:
Iringa net haikuwa Mshindo. Pale ghorofani ni Kitanzini kwa Ngailo karibu na Masiti complex!
BAADAYE
nakupa pole kwa kujiaminisha urafiki na kufahamiana na watu wa sampuli hiyo na hongera kwa kujiongezea elimu ya tabia za wanadamu. Msamehe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…