Jiunge nami kusema hapana kwa udhalilishaji na ubaguzi anaoufanya mmliki wa clock tower café Iringa

Jiunge nami kusema hapana kwa udhalilishaji na ubaguzi anaoufanya mmliki wa clock tower café Iringa

Nioneshe niliposema Id mpya.... Ukinionesha naomba ban ya mwaka mzima. Nyie vilaza mliruhusiwa vipi kujiunga humu? Ndo mnakuja kulia lia kwa mambo ya kipuuzi unadai wewe wakili. Huelewi hata tofaut ya public na choo cha sehemu ya kazi ya mtu.

Kwa hiyo unataka uwe unaenda tu kujisaidia sababu unamfaham? Halafu unaambiwa unadai ubaguzi. Kuna ubaguzi gani hapo?nenda kafungue kesi basi.
Bado ana kariri mambo ya USA, na vile aliepambana nae ni muarabu , akajua ni racism
 
Inaonekana mara kadhaa umejisaidia hapo na hasira zimempanda hata hukuwasalimia aidha kwa kuwa ni msomi au ulikuwa umebanwa sana (yote yanawezekana)

Kuhusu Ulaya na sehemu zingine utaratibu ni huo huo kama sio mteja wana haki ya kukukataza kujisaidia hilo halina mjadala (for customer only)
Sioni ubaguzi hapo kabisa kwani kama ni ubaguzi usingekuwa unaenda hapo, mbaguzi halafu kila siku mnaongea nae na unamjua miaka mpaka baba yake.

Siku nyingine hata kama umevaa suit yako ni wajibu ukiwakuta watu uwasalimie na kuomba kuwa unaenda kujisaidia
 
Umeandika/Umecopy Mkeka mrefu sanaa
Jinsi wabongo walivyo wavivu,watakuwa Wamesoma na ilipofika Juu juu Waka scroll.

In summary

Hilo bandiko Linahusu Ubaguzi (kwa mujibu Wake)
Muandishi Ni mwanasheria/wakili
anaishi Iringa.
Ni mteja mzuri sana wa Mgahawa uliopo Clock Tower Iringa dodoma road.
Akiwa katika harakati Zake za Kuweka mkono kinywaji,alibanwa na haja Sasa kwa Kuwa Ni mteja wa pale na Ni mwez mtukufuku (ramadhani) akaon ngoja nikaji sitili pale (kujisaidia japo hajasema Kama ilikuwa kubwa au ndogo haha yamkini Kubwa).

wakati kashamaliza kuji hajabisha,ghafla mhudumu akamuambia Kuwa "Yeye c Mteja mzuri na anatakiwa asikanyage Tena pale"

na hiyo ndiyo hoja yake Kuwa. aliambiwa asikanyage Tena hapo.bila sababu ya Maana.
so akaona Kuwa ame baguliwa (C unajua Wanasheria tena?!).

Kupitia Ubaguzi wake akatumia ref za wakati wa ukoloni jinsi watu walivyokuwa wanabaguliwa katika nchi yao.

Ni Hayo TU.
Sasa kama mwanasheria analialia mbele za watu je sisi wakulima tutafanyaje?amedhalilisha taaluma yake na ndo hapo nazidi kupata mashaka na wasomi wetu wa Tanganyika
 
Binadamu yeyote ameumbwa na udhaifu, wewe unapoona udhaifu wa mwenzako kupitiliza chooni ni sahihi kupewa maneno makali ya kashfa na kuzuiwa kuingia eneo hilo tena, kuwa ni jambo sahihi kunasiku utajuta kuzaliwa kwa litakalokukuta kwenye hii dunia. Maana unapoweka interest binafsi katika kutetea ujinga ukumbuke dunia ni mzunguko, kunasiku mwanao au mkewako atashikwa na hali mbaya mjini akaingia pasipokupenda katika choo cha watu anapotoka na kukutana na watu wasio na utu wenye itikadi mbaya za ubaguzi kama hao wala usiende kulia kuwa ametukanwa. Kunahekima yakuongea na mtu, daima watakuwepo watu ambao kiburi cha mafanikio ndio kimeijaza midomo yao na hekima imefichwa mbele za mioyo yao wasijue namna yakuteat binadamu aliyeumbwa na Mungu anayewanyweshea mvua matajiri na masikini.
 
Vyoo vya kulipia viko kibao ungeenda huko.Choo Cha hoteli Ni kwa ajili ya wateja wanaonunua chochote Sasa mtu unaenda tiu kujaza choo ya watu hununui kitu SI sawa wakati unajua anagharimia maji ,wafanyakazi wa kusafisha,kuvuta kikijaa nk SI sahihi .Yuko sahihi choo chake Sio Cha umma
 
Huyu bwana anatangaza kazi yake ya UWAKILI, kiustaarabu ukibanwa haja nenda choo cha Umma hapo stendi ya mabasi
 
Huyu bwana anatangaza kazi yake ya UWAKILI, kiustaarabu ukibanwa haja nenda choo cha Umma hapo stendi ya mabasi
Mwenye cafe choo chake ni haki yake kuamua Nani aingie na nani asiingie.Kwani alimsaidia kujenga? Angeondoka kimya kimya.Analazimisha Kama vile lazima ajisaidie humo.Kujuana Sio leseni ya kutaka kwenda kujisaidia bure..Ile Ni biashara.Principle ya biashara Ni I know you but my business doesn't know you if you are not a customer who buys something!!! Huyu wakili anataka kuchanganya kujuana binafsi na biashara!!!! Biashara ni biashara ukienda kwenye biashara nenda kwa biashara Sio kwenda kujisaidia bure na kutoka bure.No no no.Hayuko pale na wahudumu hawapo pale kuhudumia wajisaidia chooni bure!!! Naungana na mwenye cafe huyo wakili asirudi hapo tena kwenye hiyo cafe.Niko pamoja na mwenye cafe
 
Binadamu yeyote ameumbwa na udhaifu, wewe unapoona udhaifu wa mwenzako kupitiliza chooni ni sahihi kupewa maneno makali ya kashfa na kuzuiwa kuingia eneo hilo tena, kuwa ni jambo sahihi kunasiku utajuta kuzaliwa kwa litakalokukuta kwenye hii dunia. Maana unapoweka interest binafsi katika kutetea ujinga ukumbuke dunia ni mzunguko, kunasiku mwanao au mkewako atashikwa na hali mbaya mjini akaingia pasipokupenda katika choo cha watu anapotoka na kukutana na watu wasio na utu wenye itikadi mbaya za ubaguzi kama hao wala usiende kulia kuwa ametukanwa. Kunahekima yakuongea na mtu, daima watakuwepo watu ambao kiburi cha mafanikio ndio kimeijaza midomo yao na hekima imefichwa mbele za mioyo yao wasijue namna yakuteat binadamu aliyeumbwa na Mungu anayewanyweshea mvua matajiri na masikini.
Kuishi kwa mazoea ndo kumetufisha hapa, kwasababu umeenda kupata huduma sehemu mara moja unaleta uodinary kama hujaomba hata mimi nakubalasa,hakuna sehemu ambayo utatanguliza ustaarabu ukapatiwa maudhi.
 
Duh pole sana wakili, Umeomba watu wakuunge mkono, waone umedhalilishwa, naona wote waliochangia wanakupinga. Hapo ulipofungua ofisi ni muhimu kuwa na Choo, sasa ukiwa na wateja, wakishikwa na haja huwa unawaelekeza waende wapi.
 
Usipende kuhudumiwa chakula kwa mtu ambaye umegundua hakupendi tofauti na hapo sumu ya panya inakuhusu
 
Nyie wanasheria huwa mnajifanya wajuaji sana, lazma utakuwa umezngua huko afu unataka mharbia mwenzako biashara
 
JIUNGE NAMI KUSEMA HAPANA KWA UDHALILISHAJI NA UBAGUZI ANAOUFANYA MMLIKI WA CLOCK TOWER CAFÉ IRINGA.

#SAYNOTOCLOCKTOWERCAFEIRINGAMISTREATMENTOFCLIENTS#
Nimekuwa mteja wa mgahawa wa Clock Tower Café uliopo barabara ya Dodoma/Uhuru Avenue katika Manispaa ya Iringa tangu uanzishwe mwaka jana. Nimekuwa nikipata huduma ya chakula katika Mgahawa wa Clock Tower nikiwa ama peke yangu au nikiwa na wageni au wateja wangu kwa kuwa ofisi yangu ya Uwakili ipo jirani tu na mgahawa huu. Hata hivyo jana tarehe 9 mwezi Mei mwaka 2019 limetokea tukio ambalo limenisononesha na kunifanya nisiwe tena na hamu ya kupata huduma ya chakula katika mgahawa wa Clock Tower Café wa hapa Iringa.

Jana ilikuwa ni siku ya tatu/ya nne ya mwezi wa Ramadhan. Nami nilikuwa katika saumu lakinijana wakati natoka mahakamani wakati napita Clock Tower Café nilijisikia haja nikaona niinge ili nijisaidie. Mnamo saan 4.00 asubuhi hivi niliingia Clock Tower Café. Nilipoingia nilimkuta Mmiliki wa Clock Tower Café, Iringa akiwa na mfanyakazi wake wa muda mrefu tangu enzi eneo hilo lilipokuwa Iringanet ikitoa huduma za mtandao wa internet. Kama ilivyo desturi niliwasalimia na kuingia ndani nikapita chooni.

Wakati nataka kutoka Clock Tower Café, niliwakuta Mmiliki na mfanyakazi wake wakiwa eneo lile lile na Mmiliki alinikabili kwa ujeuri na katika hali ya udhalilishaji na kashfa kwangu. Mbele ya wateja na wafanyakazi wa Clock Tower Café Iringa alinionyesha kwa sauti ya ukali kama vile mimi ni motto mdogo sana poster yenye maneno “Management reserves the right to refuse admission” iliyobandikwa ukutani. Maneno hayo ya Kiingereza yanamanisha: “Utawala unayo haki ya kumkataza mtu yoyote kuingia”. Na kisha kwa maneno makali akaniambia eti mimi ni mteja mbaya na kamwe hataki kuniona nikiingia au kununua chochote katika mgahawa wake wa Clock Tower Café Iringa na kwamba choo chake sio choo cha umma.

Kwa kweli nilifedheheka sana na kuvunjiwa heshima yangu katika jamii kwa tukio hili na sikuamini kinachotokea. Nimekuwa ninamfahamu Mmiliki huyo wa Clock Tower Café Iringa kwa miaka mingi sana name nimekuwa nikimchukulia kwamba ni jamaa yangu na yeye ananifahamu kwa kina na kazi ninazofanya hapa Iringa na hata baba yake namfahamu na tuna mahusiano mazuri tu kwa miaka mingi. Nimemfahamu Mmiliki huyu wa Clock Tower Cafe Iringa tangu mwaka 2015 nilipokuwa nafanya kazi Iringa na nikiwa mteja wa Iringanet tangu ilipokuwa jingo la Ghorofa pale Mshindo hadi anahamia hapa Barabara ya Dodoma. Kwa upole, nilimsihi na kumkumbusha kwamba tuko ndani ya mwezi wa Ramadhani na si vizuri kunifanyia kitendo cha udhalilishaji lakini alibaki na msimamo wake kuwa hanihitaji mimi wakla wananihusu kuwa wateja wa Clock Tower Café na kwamba niondoke na kamwe nisiingie tena Clock Tower Café Iringa. Ilibidi niondoke kwa aibu kimya kimya kwa unyonge mithili ya mbwa aliyemwagia maji akiogopa hata kubwekawa. Na jambo hili lilinishangaza sana kwa sababu sehemu ya biashara ni sehemu ya umma ambapo kila mtu anaweza kuingia na kutoka.

Kwa kweli tukio hili lininsononesha, kunidhalilisha na kunikumbisha si tukio lilimtokea mmoja wa wagombe Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alipoingia katika Hotel moja Mjini Dar es Salaam, Uongozi wa Hotel ulikataa hata kumhudumia maji ya kunywa na pia unakumbusha madhila ya siku za ukoloni ambapo watu waafrika licha ya kuwa ndiyo wenyeji wa nchi hii walikuwa wanabaguliwa kwa rangi na hadhi yao na kukatazwa kuingia katika mahoteli au migahawa ya watu weupe. Pale jijini Tanga ilikuwa rahisi mbwa kuingia Planters Hotel lakini si Mwaafrika. Na marehemu Mzee Erasto Mang’enya katika kitabu chake kimoja anaeleza madhila haya ya ubaguzi kwa waafrika pamoja na elimu yake na kuwa mjumbe wa Mamlaka ya Mji alikuwa haruhusiwi kuingia katika Hotel za watu weupe kwa kuwa tu alikuwa ni Mwaafrika.

Na ni jambo la kusikitisha zaidi kuona kuwa baada ya zaidi ya nusu karne ya nchi yetu ya Tanzania na pia Visiwa vya Unguja na Pemba kuwa nchi huru, bado wapo watu kama Mmiliki wa Clock Tower Café Iringa ambao wanaona wanayo haki ya kumnyanyasa Mtanzania na kwamba Mwaafrika kwao ni mtu dhalili asiye na hadhi au haki ya kupata huduma katika biashara zao. Jambo hili halivumiliki hata kidogo na kamwe siwezi kukaa kimya katika hili kuona mtu kwa sababu yeye ni Mwaarabu au Mweupe anayo haki ya kumnyanyasa mtu mweusi katika ardhi ya mababu zake. Je mtu mwenye rangi nyeupe akiingia Clock Tower Café kwenda choo kujisaidia na kasha kutoka bila ya kupata huduma yoyote, je Mmiliki huyu angemsemesha katika kama alivyonisemesha mie kijeuri?

Kama Mtanzania na Mwaafrika naona fahari kuwa nimepata bahati ya kutembelea au kuishi katika nchi zingine za Afrika Mashariki, Ulaya (Norway) na Marekani (USA) lakini katika kutembea kwangu kote huko sijawahi kukatazwa kupata huduma hata ya kujisaidia chooni katika mgahawa au Hotel yoyote kokote kule duniani isipokuwa hapa Iringa katika mgahawa huu wa Clock Tower Café. Kote nilipopata huduma hotelini au mgahawani nimekuwa nikipata heshaima ya utu wangu kwa usawa bila ya kujali hali yangu, rangi yangu au Utaifa wangu hata kama nilikuwa Mwaafrika pekee mahali hapo. Kamwe sijawahi kutokewa na tukio la kubaguliwa na kuonekana dhalili na nisiye na hadhi yoyote isipokuwa jana mbele ya Mmiliki, wafanyakazi na wateja wa Clock Tower Café Iringa ndani ya Mji na nchi yangu. Jambo hili halivumiliki na ni lazima kwa vitendo tulikemee.

Msimamo wangu ni kwamba tukio lililonitokea jana kamwe lisimtokee mkazi au mtu yoyote anayetembelea Iringa. Rai yangu ni kuwa wakazi na watu wote wanaotembelea Iringa kamwe tusiingie kupata huduma Clock Tower Café Iringa kwani Mmili hatuhitaji sisi anao wateja wake wenye hadhi ya kupata huduma ya chakula chake na sio sisi wakazi na watu wanaotembelea Iringa. Tusimmudhi tuwache Mmiliki huyu awahudumie wateja wake anaowataka kwa raha zake.

Tuungane pamoja kusema hapana kwa udhahlilishaji na ubaguzi anaoufanya Mmiliki wa Clock Tower Café katika nchi yetu na mji wetu!

Tafadhali mhabarishe na mwingine!

ZUBERI HAMISI NGODA
Iringa, Tanzania
Simu: +255 655 200 200
E-Mail: advocate.ngoda@gmail.com
May 10 , 2019

#SAYNOTOCLOCKTOWERCAFEIRINGAMISTREATMENTOFCLIENTS#
SASA bwana wakili ulitaka ukate gogo free of charge kisa mnafahamiana?? Hivi wananchi wote hapo iringa kila mmoja akaenda kukata gogo free of charge hapo si kitajaa ndani ya muda mfupi??

Acha hizo bwana wakili, kwako kwenye umeweka kufuli chooni kwako.
 
Sasa kama mwanasheria analialia mbele za watu je sisi wakulima tutafanyaje?amedhalilisha taaluma yake na nendeleedo hapo nazidi kupata mashaka na wasomi wetu wa Tanganyika
aiseee chalii yangu endeleeni kulima tu na mdhulumiwe mazao yenu
 
Back
Top Bottom