Jizuie kuzaa au kuzalisha ikiwa huwezi kutunza wanao au familia yako

Naunga mkono hoja
 
Mwanamke yeyote aliyepewa mimba katika umri mdogo bila kuolewa/kuwa na supportive partner, yuko katika hati hati ya kutengeneza “mtoto wa mtaani” Unakuta binti amezaa akiwa underage, hana elimu, familia haina kipato, familia iko broken kiasi kwamba hata “mama huyu” akifariki hakuna wakumlelea mtoto, hivyo mtoto anaanza kujilea mitaani na pia ukatili majumbani huwa ni chanzo cha watoto kukimbia makwao hasa katika umri wa miaka 7-12.

Solution: 1. Women empowerment (hii ina mambo mengi sana ndani yake)

2. Wanaume muache watoto wakike wasome msiwachezee wakiwa bado wadogo.

3. Jamii kuwa na culture ya kuwa na strong families kama institution ya kwanza kijamii.

NB: Watoto wa mitaani wengi chanzo chake ni unstable families = mimba za utotoni.

Tukubali tusikubali, Watoto wengi wa mtaani mfano katika jiji la Dar, wengi wametokea mikoani, wamedandia treni hadi wamefika Dar, na hata kama ni wa Dar basi wametokea katika mitaa yetu ile, Je tumeliona tatizo??
 
Hii mistari mizito aseee Mungu atupe nguvu zaidi katika kulea wanetu katka maadili mema alafu kuusu swala la kuchukia swala la single mama kila mtu Yuko na mtizamo wake kwa vile anavyoona yeye huwezi chukia tu from no where chief
 
Hii mistari mizito aseee Mungu atupe nguvu zaidi katika kulea wanetu katka maadili mema alafu kuusu swala la kuchukia swala la single mama kila mtu Yuko na mtizamo wake kwa vile anavyoona yeye huwezi chukia tu from no where chief
kuhusu kuleta watoto naunga mkono, ila kuhusu kuchukia ndio ni mtazamo so kila mtu ana haki ya kuji elezea
 
Ndo maana nasemaga, ninge kuwa mkubwa😊😊
 
Hakuna jambo ambalo tunaweza kufanya pasipo kuwa na matokeo yanaweza kuwa hasi au chanya hivyo lazima tujifunze kukubali na kuyapokea matokeo tunayoyatarajia au tusiyoyatarajia hiyo ndio itakuwa njia pekee ya kukabiliana na hizi changamoto zinazojitokeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…