JK Aikana Sera ya Maisha Bora kwa Kila M-TZ

JK Aikana Sera ya Maisha Bora kwa Kila M-TZ

If you once forfeit the confidence of your fellow citizens, you can never regain their respect and esteem. It is true that you may fool all of the people some of the time; you can even fool some of the people all of the time; but you can't fool all of the people all of the time.- Abraham Lincoln
 
Haya hiyo siyo yake!
Jamani hebu tuorodheza alivyoahidi vyote and then tuhesabu mangapi ameshayakana, mangapi anategemea kuyakana na mangapi yametekelezwa na yepi hayajakanwa wala kutekelezwa na wala kuzungumziwa.
 
Vipi ile ya ajira 1,000,000 nayo aliikana..???? Au bado kwamba tunasubiri akane moja hadi nyingine.... mweeeeeeee.......ama kweli imbombo ngafu...!!!!!!!!!
nahisi atasema hivi uchumi wa dunia utetereka....teh teh
 
Vipi ile ya ajira 1,000,000 nayo aliikana..???? Au bado kwamba tunasubiri akane moja hadi nyingine.... mweeeeeeee.......ama kweli imbombo ngafu...!!!!!!!!!


Haya hiyo siyo yake!


Mbona hii alishaikana...kama sikosei alikuwa nalihutubia Bunge; alisema CCM walimwandalia, yeye akawa na mashaka nayo wakamwambia wewe umewekwa na CCM, usijali Chama kitatekeleza sera bila wasiwasi.
 
Ungekua wewe unge fanyaje...?
Mkuu mbona maswali mengine yanaleta kichefuchefu...Ebu rudia kusoma hotuba ya JK kisha fikiria ungekuwa wewe ungefanya nini!
Kwanza ameanza kwa kuikana ilani ya Maisha Bora akidai ni ya Nyerere na yeye kaikuta, kaiendeleza vipi?..
Huyo huyo JK anamsifia mwalimu kwa kutuletea Uhuru ambao yeye leo hii anauuza kwa wageni.. soma tena maelezo ya JK utaona kila anachokifanya ni kinyume cha wale waliomtangulia..tujivunie ya Nyerere au yake yeye..
Nchi inazidi kudidimia ktk umaskini, tunagawanyika ktk makundi ya matajiri na maskini (gap kubwa), Ukabila na Udini vimeshamiri bado unataka kuuliza mtu mwingine angefanya nini?..JK amekwisha kama team yake ya mpira Newcastle United..
 
Hii ni sera ya ngapi sasa Rais wetu anakana...JK imefika mahali ni rahisi mno kutabiri atafanya nini next..!!

Ni bora aseme tu uongozi wa nchi umemshinda na hivyo hatagombea tena 2010 badala ya kujibaraguzabaraguza tu kila kukicha.Kuna ugumu gani wa kutamka kwamba, "Naipenda sana nchi yangu ipate maendeleo ya kweli kabisa. Muda niliokaa madarakani wa miaka mitano nimeshindwa kuyatimiza yale niliyowaahidi katika kampeni zangu za Urais hivyo nimeamua ili kuinusuru nchi yetu mimi sitagombea tena na hivyo kumpisha mtu mwingine naye ajaribu kusukuma gurudumu la maendeleo ya Tanzania."
 
Ni bora aseme tu uongozi wa nchi umemshinda na hivyo hatagombea tena 2010 badala ya kujibaraguzabaraguza tu kila kukicha.Kuna ugumu gani wa kutamka kwamba, "Naipenda sana nchi yangu ipate maendeleo ya kweli kabisa. Muda niliokaa madarakani wa miaka mitano nimeshindwa kuyatimiza yale niliyowaahidi katika kampenzi zangu za Urais hivyo nimeamua ili kuinusuru nchi yetu mimi sitagombea tena na hivyo kumpisha mtu mwingine naye ajaribu kusukuma gurudumu la maendeleo ya Tanzania."

Bado hatujapata huyu Kiongozi na hamna hata dalili ya kupatikana kiongozi kama huyu!
 
Hivi kweli nyie wote na akili zenu mliingia mkenge na kumwamini wakati anawaambia hayo?
 
Whatever!! I cant believe this guy, I feel more than a dumb for supporting him back in 2005. Is he from Mars???
 
kazi ipo kweli kweli sisi tunataka zile nyimbo za mwaka 2005 zijirudie tena za maisha bora za Tanzania
 
Hi si mara ya kwanza na wala si mara ya mwisho kwake yeye kukana sera za chama chake.Alipokuwa anaongea na wananchi kwa njia ya simu alisema "bahati mbaya mgombea urais kwa tiketi ya CCM huwa hatungi/haandiki ilani ya uchaguzi bali kuna kamati inayoandika bila kujali ni nani watamchagua kuwakilisha chama..,hivyo ingekuwa mimi hii ya MAISHA BORA KILA MTANZANIA NISINGEIWEKA".
My take:CCM HUWA INAANDAA ILANI YA KUWAHADAA WANANCHI.
Kikwete ni RAIS WA TZ SIO WA CCM,AFANYE KIZURI AU MAZURI ANAYOWEZA BILA KUVUNJA KATIBA YA NCHI POTELEA MBALI AKIVUNJA KATIBA YA CCM.
 
Mbona hii alishaikana...kama sikosei alikuwa nalihutubia Bunge; alisema CCM walimwandalia, yeye akawa na mashaka nayo wakamwambia wewe umewekwa na CCM, usijali Chama kitatekeleza sera bila wasiwasi.
ha ha ha,teh teh hii kali kweli huyu prez ni mtupu kiasi hiki?nahisi homa kabisa hapa,sijui sisi watz tutaonewa mpaka lini?nadhani sasa iliyobaki nayeye kaona hapa ni kukanusha tuu kila atakachoulizwa sasa afanyeje,kwani tutampeleka au kumshtaki wapi.hilo ndo changa la macho tushapigwa na mpaka ifike 2015 nadhani bongo itakua tayari kama zimbabwe
 
Not admitting fault is like the 1st commandment for being a "good politician". Hakuna mwanasiasa anaye kubali kosa. Lazima atafute jinsi ya ku-suga coat. Lets not forget that JK is 1st and for most a politician.
 
Msanii tu huyu! Alipotwambia kwamba "Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana." alitaka ionekane ni sera yake na ilikuwa ni sera yake sasa baada ya miaka minne baadaye na kuona kavurunda vibaya sana katika sera hiyo na 2010 ndiyo inajivuta taratibu anaaza kupata kigugumizi na kuikimbia! atazikimbia sera nyingi sana kabla ya 2010 maana hakuna hata moja aliyofanikiwa.
 
Jamani JK ameweza kutekeleza baadhi ya sera alizoahidi 2005 na nyingine bila shaka ataweza kuzitekeleza.

Ameweza kutengeneza mabilionea 100 kama alivyoahidi. (Karamagi, Chenge, Liyumba,Mkapa, Mama Mkapa, Lowasa, Rostam Azizi, Shekifu-mkuu wa mkoa manyara, Mzindakaya, Yona, Mramba, Mgonja, Mkulo, lawrence Masha, Mboma, Epson, Lukaza, Beredi Malegesi na list inaendelea.
 
Hajaikana bali anachosema ni kuwa hii sera ilikuwepo - na huenda ilikuwa dormant katika mazungumzo ....hivyo utawala wake uliamua kuifufua na kuiendeleza na watakaokuja wataendelea nayo.
Asichosema ni kwanini toka enzi hizoooooo hatukuwahi kusikia kiongozi akiahidi waziwazi kumpa kila MTZ maisha bora?
Maisha bora ni nini?

Ndicho alichosema wakati wa Kampeni za 2005?Au mwaka huo alikuwa hajui kuwa "sera hiyo ilikuwepo tangu zama za uhuru"?Why now?

Hizi ni dalili za kushindwa majukumu just like CCM,through the same JK,walivyokana suala la Kadhi na kudai aliyelianzisha ni Mrema,na JK hakuwa mtunzi wa manifesto ya CCM 2005.

Ugonjwa uleule wa kutoa mjibu mepesi kwenye maswali magumu.
 
Ari mupyaaa,nguvu mupyaa na kasi mupyaa..bwahahaha!
ndiyo mmeshaliwa mazee muhesabu maumivu mpaka 2015!
 
Back
Top Bottom