Wakuu zangu, ukisoma maelezo yake ni kwamba JK ameikana ahadi yake..Swala halikuwa ahadi hiyo ilikuwepo toka lini kwa sababu hakuna sera duniani unayoweza kuivumbua wewe ikakubalika kwa wananchi ambao hawafahamu lini na wapi iliweza kutumika..Hata huyo Nyerere mwenyewe aliikuta sera ya Maisha bora ikitumiwa nchi nyinginezo..Muhimu ni ahadi yako ktk kupanga priority zako ktk uongozi na ndicho alichotuahidi wananchi..
Majibu ya JK ni ya kihuni kabisa, huwezi kuwaahidi wananchi MAISHA BORA kama Kipaumbele cha sera zako kisha ukaikana kuwa sii sera yako hali umeitumia sera hiyo kama kipaumbele kujipatia kura za wananchi. Kila ahadi aloweka anaanza kuzikana kihuni kihuni sasa nambieni ni sera ipi aloitunga yeye maanake hizo ahadi zimekuwa sii zake, zake yeye ni zipi?