JK akihojiwa CNN--" Dynamic leader, dynamic country "....Toa maoni yako

JK akihojiwa CNN--" Dynamic leader, dynamic country "....Toa maoni yako

At least kampita Balozi Amina Salim Ali.

What lowered expectations!
 
Kikwete amewahi kutoa one on one interview ndani ya Tanzania?

Amewahi kuulizwa swali hata moja na mwandishi mzalendo?

Wapi, lini, nani alimuuliza, na alijibu nini?
Mkuu ndio maana nasema kuwa hata wengi wetu ambao tumo humu ndani ya JF tuko nje ya nchi,wengine wamelowea huku kwa miaka mingi sana,na hivyo kupoteza ile touch,ukweli ni kwamba mwananchi wa kawaida pale bongo akiingia humu anaweza kudhani labda ni maigizo,hakuna reality,watu wanaongea vitu visivokuwepo na kufagilia issue zisizomgusa Mtanzania wa kawaida.

Kwasababu hata hayo maswali na majibu yakitafsiriwa ili mwananchi wa kawaida ayasome yatampa mwangaza ama kumsaidia kivipi?
La kushangaza,kuna wanaoona kuwa majibu yalikuwa mazuri na hivyo eti wanafagilia na wakati huo huo huwezi kuamini hali halisi ya nchi na migogoro na umasikini tunaokabiliana nao.

Nimeshagundua kuwa hakuna mwanamtandao hapa atakeyekwenda kuleta mabadiliko kwasababu hii comfortability ya CNN haiko bongo,na kama tunapata viongozi based on how wanaweza kujieleza kwenye CNN(kwa maoni ya baadhi) Bila ya kuwa na uwezo wa kujibu mwaswali ya msingi ya wananchi wazalendo,then hakuna haja kabisa ya kulaumu uongozi tulio nao.

Kusema ukweli swali lako ni la msingi kabisa kwasababu hata mimi sijawahi kupata kusikia akijibu hoja za mwandishi mzalendo,bado kusikia ama kuona.

Perfomance ya JK'S interview ni ya kawaida kabisa,na kwasababu kuna wanaoona ni high perfomance,then mimi nashangazwa sana na standards zetu.

Yani nimechoka,kuna wanaosema eti alijibu bila kusita,unaona...Watu hawaangalii contents,tumekwisha,this generation,nuttin.
 
Perfomance ya JK'S interview ni ya kawaida kabisa,na kwasababu kuna wanaoona ni high perfomance,then mimi nashangazwa sana na standards zetu.

Tatizo kubwa watu wako too easily impressed au inawezekana matarajio ya yeye kujieleza yako chini kiasi cha kwamba hata akijibu kawaida tu anaonekana kafanya vizuri kweli kweli.
 
Bluray,Dilunga,

..wananchi tulikuwa tunamcheka na yale MADESA yake, lakini trust me, they helped him a lot.

..yani kuna a major difference kati ya JK aliyetolewa nishai na kina Dr.Kaberuka,Trevor Manuel, Dr.Ekonjo,..na huyu aliyehojiwa na CNN.

..zaidi mimi nashauri ile set-up ya kimdahalo kama ya pale BOT haimfai. hii one on one ndiyo anaweza zaidi.

NB:

..hii habari ya kwenda ktk western capitals na kusema Waafrika tunahitaji msaada bcuz we are not responsible for the global financial crisis mnaionaje?

..mimi naona haijakaa vizuri kwasababu wanaotusaidia ni walipakodi wa magharibi ambao nao hawako responsible na global financial crisis.
 
..zaidi mimi nashauri ile set-up ya kimdahalo kama ya pale BOT haimfai. hii one on one ndiyo anaweza zaidi.

Sidhani kama hata hiyo one on one anaiweza kihivyo maana akikumbana na mtu kama marehemu Russert itakuwaje? Unaona kafanya vizuri sasa hivi kwa vile viswali vilikuwa vi softball.....
 
... hata mimi sijawahi kupata kusikia akijibu hoja za mwandishi mzalendo,bado kusikia ama kuona.

Sasa anaogopa nini kufanya interview nyumbani?

Huyu si tuliambiwa ni mzungumzaji, mtu wa watu mcheshi, he can talk an owl out of a tree, kijana, anaweza kuimbisha wake kwa waume, unaweza kunywa nae chai ukawa comfortable tu, you know, sifa kama za Mwinyi.

Now imagine that, Rais umetawala miaka inaenda minne, hujawahi kukutana na mwandishi nyumbani. Anaogopa?
 
Maswali aliyoulizwa ni yale yale,narudia,ni yale yale kwasababu challenges za waafrika ni zile zile for centuries...Umasikini,ni challenges zile zile zilizokuwepo toka akiwa waziri wa mambo ya nje,same same challenges,same same questions,kilichoongezeka in terms of decades kama tukiachilia mbali centuries,ni UKIMWI,Malaria was there,na hata hapa USA malaria ilikuwepo,wameitokomeza.
Niliposema haya ma interview ambayo yanawapa hao mnaowaita wafadhili picha ya tofauti na hali halisi,na huku sapoti kubwa ikitoka kwa hao wanaojiita wanamageuzi,na wazalendo humu ndani,basi hoja yangu inabaki pale pale tu kuwa this generation ni buree!
Kwa miaka zaidi ya kumi ambayo alikuwa wizara ya mambo ya nje,je kuna anayeweza kuniambia kuwa what is a possibly different question ambayo ameulizwa kwenye interview hii na hakuwahi kuulizwa huko nyuma?
Ambalo labda naweza kusema ni possible kuwa hajawahi kuulizwa ndani Ya miaka yake ya utumishi ni hilo la Humble upbringing and becoming a president pamoja na issue ya credit crunch ambapo pia amekuwa akizungumza the same things toka siku ile alipoalikwa kwenye mkutano wa G20.
Kuna mwenye kuweza kutuambia for certain that these are different questions?
Kazi ipo...Duh!
 
Last edited:
Ashukuru huyu mama anayemhoji ni soft/na hayuko informed na mambo yanayoendelea TZ. Angekutana na Tim Sebastian wa BBC (hard talk) aliyemiterview na kumchimba Mkapa mpaka akakasiria sijui ingekuwaje.
 
.................Alipoulizwa aelezee kuhusu humble upbringing yake na how possible did he get there as a president na ana nini cha kusema kuhusu hilo yeye alidai kuwa Babu yake ndiye alimpenda na akaamua kuishi naye,na pia kwamba babu yake sijui uncle alikuwa chief,then akaendelea kwa kusema kuwa alienda jeshini na akawa pia mwanachama wa ccm na ndio maana akawa rais....Ukweli ni kwamba hilo siyo jibu sahihi,kwasababu hakuelezea kama ali work hard to get there or what,na ni what kind of circumtances zilimwezesha kufikia hapo alipo,sasa kama ni kuwa mjukuu wa chief na kuwa mwana ccm pekee ndivyo vilivyompa uwezo wa kutokea kwenye umasikini hadi urais,then hakuna situation yoyote ambayo inaweza kumweka kwenye kundi la watu wa kawaida waliotokea kuwa viongozi wakuu wa nchi,tayari alikuwa na lots of priveledges na ndio maana alijibu alivyojibu..................

kwi kwi kwi kwi....................it was interesting to know though.......safari hii amejitahidi kuwa focused japo still alikuwa shallow........
 
Sasa anaogopa nini kufanya interview nyumbani?

Huyu si tuliambiwa ni mzungumzaji, mtu wa watu mcheshi, he can talk an owl out of a tree, kijana, anaweza kuimbisha wake kwa waume, unaweza kunywa nae chai ukawa comfortable tu, you know, sifa kama za Mwinyi.

Now imagine that, Rais umetawala miaka inaenda minne, hujawahi kukutana na mwandishi nyumbani. Anaogopa?

Mkuu Dillunga ni lazima tufute mentality ya kuomba omba kwasababu tumekuwa tukitayarisha marais ambao wanauwezo wa kuomba ama kujieleza wakati wa kuomba na si watatuzi wa matatizo tulio nayo kama Taifa.

Kama ni kweli nyumbani kungekuwa kunapewa kipaumbele kwenye utaratibu wetu wa presidential recruitment,then ni kwanini tulazimishe sifa kama hizi? Na bado eti sifa ni kuwa waziri wa mambo ya nje na kuwa na exposure,hii ndio the maximity of what we have been building since Mwalimu's era,sasa tumo ndani ya shimo lenyewe.

Ni lazima tuchukue different direction on how we recruit kiongozi mkuu wa nchi maana priorities zetu za sasa hazitaweza kutupatia kiongozi wa aina hiyo chini ya the same system.

Swala la kuwa tegemezi lilitakiwa liwe linapungua with time kama kweli tuko kwenye right track,hilo halipo,so tuko waay wrong.

Utamaduni wetu sisi wabongo ni kuonekana mtu wa maana pale unapojieleza vizuri mbele ya mzungu na kwa lugha ya ufasaha na personality,kamwe haijawahi kuwa matendo na achievements,na hata kama kuna achievements,ni hao hao wanaowahoji ambao wamekuwa impressed kidogo ndo wanamcredit kiongozi wa nchi,na kama na wao wana maslahi,then usitegemee kuwa hawatampamba,wakipamba tu,kinachofutia ni wapambe wa nyumabani wafuata mkumbo na wapambe wenye kunufaika na hujuma hiyo,na kama baba mwenye nchi amerudi na tuvifurushi pamoja na pesa,basi,ngoma ntolee,watu wanasahau madini yanachimbwa na maliasili zinaporwa.Kuna gaps nyingi sana,ama loopholes btn how wananchi understand the reality about their leaders vs what their leaders actually does....Kweli wakiangalia pemebeni sisi ni masikini,lakini spending na uuzaji wa rasilimali viko pale pale na wao hawapati habari hizo,pengine wanasubiri hotuba ambazo zinaendana na uwezo wao wa kufikiri,ni bora liende,wenye kula wanakula,wenye kufa njaa wanakufa njaa,porojo mbele.

Ni kwamba tulishakubalishwa uomba omba,na kama tukiweka msisitizo kwenye uzalendo kama unavyosema,basi issue za rasilimali zetu kutunufaisha ndo ingepewa kipamumbele,na maswali kama hayo mkabauru hawezi kuuliza.

Ni ubovu uliokithiri,ni tatizo kubwa sana tunalo....Ni system mbovu na namna mbovu ya kufikiri ambayo watanzania tumejirithisha.

Tunamlalamikia Rais kila siku kwa kuomba omba na wakati huo huo tunapendelea aweze kujieleza vizuri kwa makaburu,makaburu kweli wana maswali ya yenye kuhusiana na hali halisi ya mwananchi wa kawaida?
Ni uozo uozo!
 
Last edited:
kwi kwi kwi kwi....................it was interesting to know though.......safari hii amejitahidi kuwa focused japo still alikuwa shallow........

Hapana,sijui ni focused ya aina gani hiyo,kusema kweli sijawahi kumsikiliza before.

Ukweli ni kwamba alitakiwa aseme kuwa ni kivipi hiyo humble upbringing imemsaidia kuwa rais na inamsaidia vipi kwenye utendaji wake,na ni kwa kivipi humble bringing hiyo inamsaidia kwenye utawala wake na mapenzi yake kwa nchi,na pia ni kwa kivipi ilimsaidia kuupata urais na nini haswa reflection ya upbringing towards good gorvernance,siyo eti kujenga kijijini,kwani wachagga wamenza lini kujenga vijijini kwao wanakotoka?Huo si ni utamaduni wa kawaida kabisa kwa mchagga na labda mababila mengine? Kwani ni lazima uwe rais ili kufanya hivyo? Na kama huo ndo mfano mzuri,mbona hakuna mchagga ambaye keshawahi kuwa rais? Na je kuwa mjukuu wa chief? Mbona hata mimi ni mjukuu wa chifu?

Nilitumia neno "Conceptual" kwa maana mkuu wa nchi anatakiwa atizame issue kama hizo in a broader way na si shallow minded way,na ni kweli uliyosema.

Haya basi mkuu,kajitahidi,ila kama uko concern,realy concerned,then jitihada hizi haziwezi kuhalalisha yasiyo ya kweli yawe ya kweli,ama wrong answers to become the right ones,ama kwamba concerns zetu zimekwisha simply kwasababu kwa maoni ya wengi JK amejieleza vizuri kuhusiana na yeye kutokea kwenye umasikini hadi kula maraha kwa jasho la wananchi kwa kigezo cha kuwatumikia via begging.
 
J-Mushi,

Nimesoma jumbe zako nyingi hapa kuhusu hii interview ya JK na kusema ukweli azimake sense hata kidogo. Mimi nimesema ya kuwa JK amejitahidi ukifananisha na press conference zake za nyuma. Amejitahidi kwa kiasi fulani na ndio maana nimempa B- na sio A+. Mimi naichukia serikali ya CCM na vile inavyoukumbatia ufisadi; lakini mtazamo wangu aunizui mimi kumpa JK fair shake.
 
Ebana vipi Lakers? hihihihihihihiiiiiiii...kule umekimbia kabisa eeeh
 
J-Mushi,

Nimesoma jumbe zako nyingi hapa kuhusu hii interview ya JK na kusema ukweli azimake sense hata kidogo. Mimi nimesema ya kuwa JK amejitahidi ukifananisha na press conference zake za nyuma. Amejitahidi kwa kiasi fulani na ndio maana nimempa B- na sio A+. Mimi naichukia serikali ya CCM na vile inavyoukumbatia ufisadi; lakini mtazamo wangu aunizui mimi kumpa JK fair shake.

Based on uelewa wako haiwezi kumake sense,nazi ni nazi tu na fenesi ni fenesi na si tunda lenye miiba.
Kama mimi na wewe tuna mitizamo tofauti baada ya kusikiliza interview hiyo,then una haja gani ya kutaka nimake sense?
Huwezi kuona hilo kwasababu hata baada ya kutizama interview hiyo hukuona to begin with,vigezo vyako ulivyotumia vya B- ni vyako,nilishweka wazi kuwa sijawahi kumsikia akihojiwa. Na nikasema based on the questions,hakuna jipya aliloulizwa ambalo labda hakuwahi kuulizwa kwenye safari zake akiwa waziri wa mambo ya nje kwani alikuwa akisafiri hivi sasa ni cha mtoto.
Bakia na hoja yako ya B- kwasababu labda nyie ndo mlimchagua maana mnafuatilia na kujua grades za kumpa.
Mimi judgement yangu iko based on this particular interview vs whats going on nchini mwetu.
Kazi ni kubwa.
 
. . . nilishweka wazi kuwa sijawahi kumsikia akihojiwa. Na nikasema based on the questions,hakuna jipya aliloulizwa ambalo labda hakuwahi kuulizwa kwenye safari zake akiwa waziri wa mambo ya nje kwani alikuwa akisafiri hivi sasa ni cha mtoto.
Kazi ni kubwa.

Jmushi ,

Through the above statement, one can easily conclude that you are contradicting yourself, and worst of all, you are making conclusions based on speculations. Who told you that he was asked those questions when he was a foreign minister? This is preposterous and that was a reason from the 'get-go' I said your argument doesn't make sense! Besides, the issue at the forefront is not how he governs Tanzania but how he performed in that CNN's interviews.
 
Kikwete amewahi kutoa one on one interview ndani ya Tanzania?

Amewahi kuulizwa swali hata moja na mwandishi mzalendo?

Wapi, lini, nani alimuuliza, na alijibu nini?

nakubaliana na wewe

kabla ya kuanza kusema kiingereza sijui kiswahili sijui watu hawampendi

jk lazima ajue kama anawakimbia waandishi wahabari TZ basi akienda safari zake za nje hawezi kuwakimbia
washauri wa kikwete ni wabaya wangetakiwa wanamwambia mkuu kila mara awe na kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa papo na waandishi wa habari bongo, akiweza kujibu kwa kiswahili basi hata akienda nje ataweza kujibu
nimeona waarabu bwana wakiongea kiingereza kibaya kuliko cha JK lakini wakimwaga point kali kuliko za JK
watu mlio kuwa karibu na JK mshaurini jamaa awe anajibu maswali ya waandishi wa habari TZ ili azoee

ile interview ni mbaya sana, imekuwa edited na cnn na inaonekana hivyo je ingekuwa haiko edited, lazima wa edit kwa ajali JK ndio anatumika kuwa mtu wao na kwenda kuwashauri viongozi wengine wa africa hiyo ni strategic decision ya marekani

JK ni mtu mzuri lakini ili TZ iendelee inabidi aache ushikaji na kuwa na roho mbaya na awe mtu mwenye maamuzi
 
du jamaa amechoka sana, jet lag naona...inabidi akapumzike Ngurdoto kidogo
 
Jmushi ,

Through the above statement, one can easily conclude that you are contradicting yourself, and worst of all, you are making conclusions based on speculations. Who told you that he was asked those questions when he was a foreign minister? This is preposterous and that was a reason from the 'get-go' I said your argument doesn't make sense! Besides, the issue at the forefront is not how he governs Tanzania but how he performed in that CNN's interviews.

Duh!
Kweli kazi ipo,maswali aliyoulizwa hayahusiani na umasikini wa Afrika? Na umasikini huo umeanza siku aliyohojiwa na ccn? Sitaki kuzungumza kwa kubeza,lakini mkuu tulia kidogo na usome postings,maswali kuhusu umasikini wa Afrika yana tofauti? maswali hayo yangekuwa tofauti kama causes za umasikini huo zingekuwa za tofauti,nimeandika hapo nyuma kuwa matatizo yetu ya umasikini ni yale yale na causes ni certainly zile zile,tofauti ni tatizo aliloulizwa la UKIMWI ambalo nalo lina age of more than a decade,lakini matatizo mengine yote have been there for centuries,soma uelewe na kama hujaelewa uliza.

Halafu unasema si how he governs,kumbe ndo hivyo kweli mnapima viongozi?

Perfomance nayoizungumzia mimi ni contents na si tabasamu,kujibu haraka ama kwa mkato,mkuu umeniangusha sana.
Na kama matatizo ya Afrika ni yale yale miaka nenda miaka rudi,ulitegemea aulizwe mswali gani ya tofauti ambayo hayagusii uchumi wa Afrika na the suffering of its people?

Mbona mnapenda sifa zisizo za msingi?

Mtu kusafiri kwanza kwa migarama na midege ya kifahari kwenda kuhojiwa kumplease nani na wananchi wanakufa kwa njaa na magonjwa huku mali za Taifa zikiporwa?

Eti issue ni interview na si how he govern,kwa hiyo nyie mnachagua rais kama maonyesho ya namna anatakavyoweza kuongea vizuri na wazungu ama content za mazungumzo hayo?
Msimamo wangu uko pale pale especially kuhusu kizazi hiki....Pia nashangazwa unaposema eti issue ni interviews za cnn,we umesoma vizuri heading kuhusu dynamic leader and dynamic country? Ebu tueleze basi...
Kaazi...
 
nakubaliana na wewe

kabla ya kuanza kusema kiingereza sijui kiswahili sijui watu hawampendi

jk lazima ajue kama anawakimbia waandishi wahabari TZ basi akienda safari zake za nje hawezi kuwakimbia
washauri wa kikwete ni wabaya wangetakiwa wanamwambia mkuu kila mara awe na kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa papo na waandishi wa habari bongo, akiweza kujibu kwa kiswahili basi hata akienda nje ataweza kujibu
nimeona waarabu bwana wakiongea kiingereza kibaya kuliko cha JK lakini wakimwaga point kali kuliko za JK
watu mlio kuwa karibu na JK mshaurini jamaa awe anajibu maswali ya waandishi wa habari TZ ili azoee

ile interview ni mbaya sana, imekuwa edited na cnn na inaonekana hivyo je ingekuwa haiko edited, lazima wa edit kwa ajali JK ndio anatumika kuwa mtu wao na kwenda kuwashauri viongozi wengine wa africa hiyo ni strategic decision ya marekani

JK ni mtu mzuri lakini ili TZ iendelee inabidi aache ushikaji na kuwa na roho mbaya na awe mtu mwenye maamuzi

Well said Semilong,hao cnn si ndio hao hao wanaorusha tangazo la kuitangaza Tanzania kila mara? Na unadhani ni pesa kidogo? Lazima wambebe,ndio hao hao walikuja hata wakati wa ule mkutano wa Sullivan,na ndio maana nikasema ni well planned.
Lakini hilo si shida,contents.

Hakuna strategic plan ya kutuondoa kwenye uomba omba na umasikini?
Kwanza hata kuna mtu amefuatilia kujua kama hayo matangazo yanayocost mamilioni ya dola yamelipa? Si amefanywa wakati huu ambapo uchumi wa dunia ni hoi na watu hawasafiri kama ilivyo kawaida?

Ni kweli kabisa kuhusu JK kuwa ni lazima awe mtu mwenye maamuzi ya maana na kamwe i wont buy hizo B- na A+ eti kwasababu amejitahidi zaidi ya interviews zilizopita za kuwa impres mabwana wakubwa.

What matters ni implications zake kwa wananchi waliomchagua na si hii JF grading hapa,hakuna substance,ni sisi wabongo priorities zetu zinasikitisha,i dont care kama tuna rais mzalendo asiyejua kiingereza,tofauti na mataifa mengine ni kwamba sisi kama hujui kiingereza basi ni kwamba hujasoma,jambo ambalo ni kweli kutokana na mfumo wetu wa elimu,lakini haina maana uwezo wa kujieleza ndo uwezo wa uongozi....Na pia maneno peke yake siyo kipimo,kipimo ni matendo.

Ameshamaliza miaka minne kwenye utawala wake,na hivyo alitakiwa ajisifu kuhusu maendeleo aliyoyaleta na mafanikio kwenye kuutokomeza umasikini,kuelezea tu kuwa Bush alisaidi sijui blah blah,nani hajui hayo?
Nani hajui tunasaidiwa toka enzi na enzi? Hata mzungu mbumbumbu asiyejua kitu anajua hilo.

Nakubaliana na pointi kuwa awe anajibu maswali ya wananchi pia kwani ndipo atapoishi akishamaliza kazi yake,Mkapa alisifiwa na wazungu,sifa za uongo kweli kweli,lakini alipomaliza kazi si amerudi hapo bongo na kazomewa kila akipita? Mwenzake naona hajifunzi kutokana na raha za madaraka...Ni vurugu tupu,Uzalendo hakuna.
 
Maisha bora kwa kila Mtanzania. Sijui mwakani watakuja na kauli mbiu gani?
 
Back
Top Bottom