Ama kweli we have a presidaa,huyo dada alipogusia suala la EPA unaweza kuona reaction ya Mh Rais facial expression na body language vimeonyesha wazi hakuwa comfortable na swali.
Pili tatizo la rushwa kwake ni wazi si imminent....Kwani amelizungumzia kama porojo tu na hata facial expression na majibu yake hakuonyesha great concern,sasa tunajuwa kuwa ni kweli kelele za ufisadi kwake zilikuwa kelele za mlango?
Tatu nina imani anajibu maswali honestly lakini yuko wrong,hilo linaweza kuwa ni kutokana na washauri ama wale wanaomzunguka na kuzungumza naye kuhusiana na mambo mbali mbali,be it ya kiuchumi ama ya kijamii,internationally na hata domestic.
Ni vyema tukawa tunauwezo wa kumsikia na kumwona rais,shukran kwa sana Mstahiki.
Alinishangaza sana eti anapo champion Capitalism na wakati swali aliloulizwa lilikuwa ni kuwa atafanya nini wakati mwelekeo wa mataifa makubwa hususan wafadhili kama USA wanaelekea kuizika capitalism kwa ku nationalise baadhi ya makampuni na otheres measures.
Huyu mtu kumbe ndo maana alikuwa rafiki mkubwa sana wa Bush na mwalimu hakumpenda.
Sikufurahishwa na jibu lile,kama anajua kuwa ubepari ndo ulikuwa the main cause ya matatizo hayo ya kiuchumi,na kwamba hata ubepari wenyewe tumeuiga kutoka kwa hao tunaowamba misaada na kuwategemea,ni kivipi yeye asisitizie kuwa they take the same route? na kwamba we are gonna take the same route regardless? Is that realy the right answer from an understanding person? Je span yake ya uelewa kuhusiana na mambo ya kiuchumi ni pana kiasi gani?
Shida ni kwamba kuna anachonufaika nacho kuhusiana na hizo kauli zake za free market,ni wizi mtupu na ujinga wa wananchi unakuwa taken for granted kwa kushirikiana na kina mabepari,na ubepari kwenye nchi yetu ni ujambazi,uporaji, unyang'anyi na utapeli,ubepari umwangushe mmarekani yeye ajidai kuwa eti ni mzuri,hawa ndo kina Mardoff wetu hawa,kwasababu hata hizo mali za Taifa si wanazo wao?Hizo free market zinzo kuwa runned na makampuni feki na huku wananchi wakiwa hawanufaiki na mali zao? Wanacheka tu huku wakidai ni "Free Mrkt" Nasikitika kusema kuwa hawa watu wanaweza kuja kupata matatizo makubwa sana hapo mbeleni kwani hawawatendei wananchi wa kawaida haki na wanawadharau kupita kiasi.
Angesema tu we hope that is the right way to solve the problem ama hata angesema kuwa hizo ni hatua muhimu za kuundoa uchumi wa dunia kwenye matatizo....Akae na watu wenye ufahamu na uelewa,hivi huyu mtu anakaa na nani na nani ni washauri wake?
Na kama ni kweli ana champion free market,then angesema kuwa zile loopholes ndani ya capitalism system ambazo zimesababisha matatizo haya ya kiuchumi zizibwe,kwasababu zipo,kutokuzitaja sababu za kuingia kwenye matatizo ni maana kwamba he's unaware of whats going on....Yeye alibakia tu kusema free market na kufanya comparisons na siasa za mwalimu chini ya Nationalisation...Na kudai kuwa hakuna cha maana kilichoonekana.
Pia anadai kuwa anataka watu waseme ametutoa chini na kutupeleka juu baada ya miaka yake mitano,ameshakaa na mwandishi local na anajuwa kuwa badala ya juu ametupeleka chini zaidi?
Kwa kifupi ni kwamba anajua kwa namna moja ama nyingine anchokifanya na ameridhia,kwani hajui kuwa matatizo hayo ya kina Mardoff na sisi tuna kina Mardoff wetu ambao bado hawajawa accountable? Ama ujambazi wa Kagoda,EPA nk hauhusiani na hiyo free market yake?
Ninasikitika kuwa tunaweza kupata mgogoro mkubwa sana kama asipokuwa makini na kuhakikisha kuwa anakuwa na washauri wa maana.