Sasa anaogopa nini kufanya interview nyumbani?
Huyu si tuliambiwa ni mzungumzaji, mtu wa watu mcheshi, he can talk an owl out of a tree, kijana, anaweza kuimbisha wake kwa waume, unaweza kunywa nae chai ukawa comfortable tu, you know, sifa kama za Mwinyi.
Now imagine that, Rais umetawala miaka inaenda minne, hujawahi kukutana na mwandishi nyumbani. Anaogopa?
Mkuu Dillunga ni lazima tufute mentality ya kuomba omba kwasababu tumekuwa tukitayarisha marais ambao wanauwezo wa kuomba ama kujieleza wakati wa kuomba na si watatuzi wa matatizo tulio nayo kama Taifa.
Kama ni kweli nyumbani kungekuwa kunapewa kipaumbele kwenye utaratibu wetu wa presidential recruitment,then ni kwanini tulazimishe sifa kama hizi? Na bado eti sifa ni kuwa waziri wa mambo ya nje na kuwa na exposure,hii ndio the maximity of what we have been building since Mwalimu's era,sasa tumo ndani ya shimo lenyewe.
Ni lazima tuchukue different direction on how we recruit kiongozi mkuu wa nchi maana priorities zetu za sasa hazitaweza kutupatia kiongozi wa aina hiyo chini ya the same system.
Swala la kuwa tegemezi lilitakiwa liwe linapungua with time kama kweli tuko kwenye right track,hilo halipo,so tuko waay wrong.
Utamaduni wetu sisi wabongo ni kuonekana mtu wa maana pale unapojieleza vizuri mbele ya mzungu na kwa lugha ya ufasaha na personality,kamwe haijawahi kuwa matendo na achievements,na hata kama kuna achievements,ni hao hao wanaowahoji ambao wamekuwa impressed kidogo ndo wanamcredit kiongozi wa nchi,na kama na wao wana maslahi,then usitegemee kuwa hawatampamba,wakipamba tu,kinachofutia ni wapambe wa nyumabani wafuata mkumbo na wapambe wenye kunufaika na hujuma hiyo,na kama baba mwenye nchi amerudi na tuvifurushi pamoja na pesa,basi,ngoma ntolee,watu wanasahau madini yanachimbwa na maliasili zinaporwa.Kuna gaps nyingi sana,ama loopholes btn how wananchi understand the reality about their leaders vs what their leaders actually does....Kweli wakiangalia pemebeni sisi ni masikini,lakini spending na uuzaji wa rasilimali viko pale pale na wao hawapati habari hizo,pengine wanasubiri hotuba ambazo zinaendana na uwezo wao wa kufikiri,ni bora liende,wenye kula wanakula,wenye kufa njaa wanakufa njaa,porojo mbele.
Ni kwamba tulishakubalishwa uomba omba,na kama tukiweka msisitizo kwenye uzalendo kama unavyosema,basi issue za rasilimali zetu kutunufaisha ndo ingepewa kipamumbele,na maswali kama hayo mkabauru hawezi kuuliza.
Ni ubovu uliokithiri,ni tatizo kubwa sana tunalo....Ni system mbovu na namna mbovu ya kufikiri ambayo watanzania tumejirithisha.
Tunamlalamikia Rais kila siku kwa kuomba omba na wakati huo huo tunapendelea aweze kujieleza vizuri kwa makaburu,makaburu kweli wana maswali ya yenye kuhusiana na hali halisi ya mwananchi wa kawaida?
Ni uozo uozo!