Ni haki yake kulipiwa kwanza amelitumikia taifa hili kuliko huyo Shekhe Yahya ambaye naye alilipiwa na JK kweli Mrema amelitumikia Taifa hili kwa hali na mali uaminifu wake kwa taifa ndio ulimpoza ndugu yangu alifikiri wako wengi wa aina yake serikalini kumbe yupo pekeyake.
hii picha inatia simanzi kubwa... ninachosikitika zaidi ni kwa nini jamaa bado anataka kugombea wakati afya yake mbaya??
Amelipiwa gharama zote na JK ,na hapa sisemi kuwa ni serikali no. Ni JK personaly ndio amelipia gharama zote kuanzia tiketi ya ndege hadi matibabu yake yote akiwa huko.
Taarifa nilizozipata hivi punde Nikiwa hapa mjini Dodoma kutoka kwa source ya kuaminika ni kuwa Agustino Mrema amepelekwa Nchini India kutibiwa .
Aliyemsafirisha ni Rais Jakaya Kikwete.
My take;
Ndio maana alikuwa anampigia filimbi JK kumbe alikuwa anataka kupata malipo?
Akirudi anaweza naye kuwa mtabiri kama Sheikh Yahaya,juu ya urais wa JK?
jk ndio zake hata sheikh yahya alishamlipia...huwa wakirudi wanapaparika sana kumpamba....bado mtikila
nadhani hapa duniani hakuna kitu chenye thamani kubwa kuliko uhai wa binadamu; haununuliki. Kwa hiyo, juhudi zozote za kurefusha uhai wa binadamu yeyote bila kujali itikadi yake ni jambo la muhimu sana. Namshukuru JK kwa hilo ingawa nilisikitika sana kusikia kuwa General Nyirenda hakupewa msaada wa namna hiyo alipokuwa mgonjwa.
Ninadhani kuwa jambo kubwa lisiwe la kuwapeleka hao wateule kutibiwa nje na kuwaacha akina Kichuguu wajifie Mwananyamala bila hata kitanda. Kinachotakiwa ni kujenga huduma za afya nchini ziwe za ubora wa juu kiasi kuwa hata watu wa nje waje kutibiwa kwetu. Tumeona siku hizi wachezaji wa mpira kutoka nje wanakuja kucheza kwenye vilabu vyetu, inabidi hata huduma zetu za elimu na afya pia tuziinue katika viwango vya kukubaliwa kimataifa kusudi watu wa nje nao waje kuzifuata kwetu.
Ningeshauri Mrema astahafu mambo ya siasa maana afya yake pamoja na mimi kutokuwa na ufahamu wa kuwa Daktari hila mzee huyu inaonekana ni mgonjwa sana .
Kumbe JK ana moyo wa kujali utu namna hii, okay. Get well soon mzee wa kiraracha.
Mkuu hata katika maandiko kuna sehemu inasema "....KUWA MWAMINIFU HATA KUFA.." Kama habari hii ni kweli basi Mrema hafai asilani, huwezi kuwa kiongozi mzuri kwa kuukana ukweli ulioupigania miaka mingi eti ili ulipiwe gharama ya matibabu ya kisukari.Kiranja; Mrema akipitisha bakuri la msaada kuwa anahitaji hela za matibabu kwenda India, je watanzania wangapi wako tayari kumsaidia??
just be honesty!
Ni Mrema aliyeandika barua kuomba msaada wa kutibiwa nje na si vinginevyo...Taarifa nilizozipata hivi punde Nikiwa hapa mjini Dodoma kutoka kwa source ya kuaminika ni kuwa Agustino Mrema amepelekwa Nchini India kutibiwa .
Aliyemsafirisha ni Rais Jakaya Kikwete.
My take;
Ndio maana alikuwa anampigia filimbi JK kumbe alikuwa anataka kupata malipo?
Akirudi anaweza naye kuwa mtabiri kama Sheikh Yahaya,juu ya urais wa JK?
Kuna Daktari wa Rufaa huku mbeya, kijana mdogo tu a graduate from muchs 2007 amepigwa RISASI tano na Majambazi, mpaka sasa hivi hali yake ni mbaya kwani Madaktari wamefanikiwa kutoa RISASI nne, wanasema hiyo nyingine labda INDIA ndiyo wanaweza kuitoa na mbaya zaidi Nasikia wameshindwa kumsafirisha kumpeleka Dar kwani hali aliyonayo hawezi kusafirishwa kwa Surface transport. Sasa nauliza hivi Serikali yetu inashindwa kuleta private Jet ili huyu kijana Daktari ( Fide) Asogezwe hapo Dar es Salaam
Mungu amsaidie aweze kupona ili aendelee kuwasaidia walalahoi wa Mbeya ambao hawawezi kwenda kutibiwa INDIA
Ni haki yake kulipiwa kwanza amelitumikia taifa hili kuliko huyo Shekhe Yahya ambaye naye alilipiwa na JK kweli Mrema amelitumikia Taifa hili kwa hali na mali uaminifu wake kwa taifa ndio ulimpoza ndugu yangu alifikiri wako wengi wa aina yake serikalini kumbe yupo pekeyake.