Na hili ndilo linalotofautisha wenzetu wa nchi za Magharibi na akina sie: kendesha mambo kwa utashi na hisia.Sasa kuna umuhimu gani wa kuwa na kanuni na taratibu?Hivi kuna Watanzania wangapi vijijini wasiojiweza ambao hawapewi favour kama anayopatiwa Mrema?
Kwani kulikuwa na ugumu gani kwa Mrema kupatiwa matibabu Muhimbili,au kama kulikuwa na ulazima wa yeye kutibiwa nje ya nchi,kwanini isningekuwa kupitia utaratibu wa kawaida wa serikali ku-refer wagonjwa nje ya nchi?
Nchi haiendeshwi kishkaji namna hiyo,na kwa nyie mnaopigia kelele huruma,anzeni kwanza kuwahurumia wahanga wa mafuriko Kilosa, victims wa ufisadi,na makundi kama hayo na siyo ku-cherry pick akina Mrema for political gains.